Sumaye anashangaza sana na ile heshima kidogo aliyokuwa nayo sasa itapotea!
1) Alichaguliwa Simply kwa uwezo wake mdogo, Mkapa hakutaka, Malechela type au Msuya type ya Prime ministers wenye haiba za Kisiasa na Independent.
2) Analaumu serikali ya Sasa kuwa imeshusha kiwango cha elimu, Wakati ni yeye aliyekuwa mtendaji mkuu wa serikali mwaka 1998 wakati mitihani ya kidato cha nne ikivuja kama njugu, hadi kufikia hatua za Mitihani kubandikwa kwenye mitisimu.
3) Anazungumza Rushwa katika serikali hii, wakati kumbe yeye alipokuwa Waziri mkuu na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, Walitunga Sheria ya TAKRIMA ambayo ni rushwa tupu.
4) Anazungumzia kuhusu Ufisadi, Wakati yeye akiwa Waziri Mkuu tulishuhudia ufisadi mkuu kwenye EPA, Rada, Meremeta, Ndege ya Raisi, Kiwira
5) Anazungumzia kuhusu Haki na Uonevu wakati yeye alipokuwa Waziri mkuu nchi yetu ilizalisha Wakimbizi wa kisiasa, na Mauaji ya Raia watafuta haki huko Zanzibar, ni nani aliyesahau mauaji ya Wazanzibar January ya Mwaka 2001?
Huyu ana Uhalali gani wa kusimama kumnadi mgombea yeyote yule kwa muktadha wa Uadilifu, haki na uwezo?