Sitta amjibu Sumaye kuhusu mabehewa mabovu

Sitta amjibu Sumaye kuhusu mabehewa mabovu

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

WAZIRI wa Uchukuzi, Samwel Sitta, amemjibu Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, baada ya kuituhumu serikali ya Rais Kikwete kuwa imewafumbia macho watendaji walioisababishia hasara nchi zaidi shilingi bilioni 220 kwenye ununuzi wa mabehewa yanayotajwa kuwa ni feki.

Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za wizara yake, Sitta amesema watendaji wote waliohusika na kashfa hizo watafikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa baada uchunguzi kukamilika.

Aliongeza kwamba kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo imeshakamilisha kazi yake na kuonesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa shirika la reli (TRL) uliosababisha kununuliwa kwa mabehewa hayo.

Aidha amesema kuwa kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo watengenezaji wa mabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa zabuni ilikuwa haina sifa.

Hata hivyo, Sitta ameongeza kuwa kamati hiyo ilibaini kampuni hiyo haikuwa na sifa na watendaji TRL walikiuka kanuni za manunizi ya serikali kwa kitendo chao cha kutoa fedha zote kwa kampuni hiyo kabla hawajaleta mabehewa.

Viongozi wanaotuhumiwa katika sakata hilo kuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa TRL, Kipallo Kisamfu; Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosowile Ngosomiles; Mhasibu Mkuu Mbaraka Mchopa; Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Kampuni, Jasper Kisiraga; na Meneja Mkuu wa Manunuzi, Ferdinand Soka.
(NA DENIS MTIAMA/GPL)
 
Hebu Sitta aache kutufanya Watanzania wote majuha. Hivi Mkurugenzi Mtendaji pekee na management team yake (kwenye shirika ambalo ni la umma lenye Waziri mwenye dhamana? pamoja na bodi yake ya Wakurugenzi?) ati ana ubavu wa kuidhinisha ununuzi wa mabehema yenye thamani ya TZ shs. 220 billion bila idhini ya Waziri wake? bodi yake?... Halafu bila ya kupitia na kushindanishwa bodi ya manunuzi?

Common Sitta!..talk to us with your sense!
 
Hadi hizo fedha zote zinapotea chanzo kilikuwa ni nini?

Naamini kuna mianya ya kimfumo inayotoa nafasi ya watu kutafuna fedha...

Hadi watu na wabunge wapige kelele ndio waanze kujifanya wanashughulikiana...
 
Mwaka huu watajibu yote. Na hili la waliosafirisha magunia 18 ya madawa ya kulevya kwenda South Africa hawajamaliza uchunguzi ili wawafungulie mashtaka hao wahusika?
 
Tujuzane. Utaratibu Wa kawaida ni upi kstika kununua Mali kama hizo zenye thamani? Sheria ya manunuzi ya umma ikoje kwa hili?
 
My serious note! TRL haina board? Haina katibu mkuu? haina waziri mwenye dhamana ya kuidhinisha hizo 220billion? Mbunge ndo walisubiriwa wanzishe hili sakata? Imagine hizo hela zingetumika kujenga maabara unadhani shule ngapi za kata zingenufaika?
 
Edward Lowasa awajibishwe, huyu ndo aliyehusika kwa kutoa maelekezo ya hayo mabehewa kukuu kununuliwa! Fisadi sana! Wala msimpe kura mpuuzeni!
 
Mwakyembe awajibishwe kisiasa ktk ufisadi wa TRL kama alivyowajibishwa Lowassa katika sakata la Richmond,tuache double standard ili tuthibitishe utawala wa sheria unatekelezwa.
 
Huyu Mu-Six kweli ni Popo! Jana amemualika mtuhumiwa wa Richmond afanye naye mdahalo!

Jua kabla halijachwa anasema atawapeleka mahakamani waliosababisha hasara ya TRL ya tsh 220 bilioni.

Huyu Mu-Six tumueleweje?, he must have to be consistency Kama ni hivyo kwanini hao jamaa wa TRL nao asiwaalike wafanye naye mdahalo badala yake anawapeleka mahakamani? Kwani sheria za nchi hii zina double standard?
 
Hivi kweli Tshs 220 Billion inatolewa bila B. O. T. kujua, au Waziri mhusika kujua?
 
Je Yeye kama wazili alikuwa hajui mpango wa manunuzi hayo? Bila shaka Alijua na ndo mwenye dhamana na Alitia sahihi kubaliki manunuzi yafanyoke na pesa ikwPuliwe .Haoni kama ana hatia ya kujiwajibisha yeye MWe yewe kwa maana bilioni miambili na zaidi zimetumika visivyo?
 
Hawa hawana mpango wa kumpeleka mtu Mahakamani,muda wote walikuwa wapi kusema kuwa wanafanya uchunguzi ukikamilika,wahusika watapelekwa Mahakamani.

Walisubiri mpaka Sumaye awalipue kipindi cha uchaguzi ndio waseme hayo wanayo yasema?hata kama kuna mtu atakayepelekwa Mahakamani vitakuwa ni vidagaa tu,mapapa hakuna hata mmoja atakayegusa Mahakamani na katika kundi la watu 32 la Magufuli sidhani kama wanakosekana.
 
Tatizo la kukimbia hesabu,tunazungumzia bilion 220 anatuambia watu sita wa TRL wakati hilo swala ni pana sana,B.OT,Waziri husika,katibu wa wizara,bodi ya wizara..
 
Back
Top Bottom