Mshauri awataje majina hao mafisadi, kwanini anamung'unya maneno? Ujasiri ni kutoa list yake ya mafisadi kama ile iliyotolewa Mwembeyanga. Unajua kwanini hathubutu kuwataja kwa majina? kwa sababu hao anaodai ni mafisadi wana rekodi yake full mkoko! Kumbuka hata Sitta uspika alipewa na hao anaodai ni mafisadi. Ni Rostam ndiye aliyesuka mpango Sitta awe Spika ili EL apewe U-PM, ambao Sitta bado unamtesa hadi leo!
Atatokaje naye anagawana na mwenye nyumba pasu pasu? Unadhani U$ 7,0000 kwa mwezi mchezo? hataki nyumba za serikali kang'ang'ania kwenye nyumba ya mtu binafsi ili apate mgao....halafu eti anajifanya muadilifu!
Mie nilishaacha longtime kusoma gazeti la Mwanahalisi, as time goes linaelekea kwenye udaku zaidi kuliko uchunguzi...
Ukiangalia kwa macho juu juu unaweza ukadhan wapo pamoja, ila kwa Mambo anayoongea Sitta na yale yanayoendelea nyuma ya pazia, naimani kubwa kuwa hawa ni maadui na kaletwa maksudi kwenye uwaziri ili litakalomtokea ionekane JK hausiki, Ref. Mwakyembe, Mwandosya.Mkuu, naona unaladhimisha habari, heading yako na thread yako vitu wiwili tofauti..
Sitta na Kikwete lao ni mmoja ndiyo maana kamteuwa kuwa waziri
Huyu sitta mimi sina imani naye sana. Yeye kama anataka aonekane ana uchungu basi aungane na kina Slaa.
Tabia ya mtu hubadilika kiongozi, Sitta Spika sio huyu wa leo, huyu wa leo ni kigeugeu, mnafki, msaliti na mzee kifikra na kimwili, unahitaji nguvu ya ziada kuamini anachokisema.Watu walipiga kelele sana sitta alipotemwa uspika. Leo vipi mnamwita mnafiki? Hapa hapa tulimsifia juu ya utendaji wake bungeni usiwo na upendeleo kwa chama tawala.
Nimeipenda. Walishindwa madiani hebu wathubutu kumfukuza sitta waoneWameshindwa kufukuza diwani watamuweza sitta?, hiyo ni ndoto.
Source: dakika 45.
Kasema mafisadi ambao wako tayari kumtoa roho ndio waliobadili utaratibu wa uchaguzi wa spika.
Anasema walishindwa kushindana naye kwenye box la kura wakaamua kuweka kigezo cha jinsia.
My take: kama JK aliridhia naye ni fisadi
Huyu Sitta ajiandae kufukuzwa uwaziri tu.
Kama unasema anachofanya Sitta ni kutoka Kikwette iweje tena ajiandae kufukuzwa uwaziri??Huu siyo muda wa kutafuta ujiko kwa kukemea ufisadi hadharani, tunahitaji hao mafisadi wachukuliwe hatua za kisheria. Sitta anatumiwa na Kikwete ili watu waone kuwa CCM bado kuna watu wenye uchungu. Huwezi ukawa na kadi ya CCM halafu ujifanye unachukia ufisadi, hii ni sawa na kuwa Mkristo lakini humpendi Yesu Kristo.