Sitta akubali kuhusishwa na CCJ: "Mimi ni mtaji wa Urais" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta akubali kuhusishwa na CCJ: "Mimi ni mtaji wa Urais"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 18, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tuesday, 17 May 2011 23:03

  Ramadhan Semtawa

  SIKU moja baada ya kurushiwa kombora la kutaka kukihama CCM na kuanzisha kilichokuwa Chama Cha Jamii (CCJ), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema yeye ni mtaji wa kisiasa na ndiyo maana amekuwa akifuatwa na vyama mbalimbali vikimhitaji ajiunge navyo kuwania urais.Akizungumza kwa simu jana, Waziri Sitta alisema si CCJ tu, bali alifuatwa na vyama vingine ambavyo kwa ukomavu wa kisiasa hawezi kuvitaja ambavyo baadhi, vilimtaka agombee nafasi hiyo ya urais mwaka jana.

  Sitta alisema ni kawaida kwa mwanasiasa mwenye mvuto kufuatwa na vyama vingine vya siasa kwa ajili ya kujiunga navyo na kusema: "Sasa cha ajabu nini kwa CCJ? Mimi ni mtaji wa kisiasa bwana!"

  "Katika demokrasia ya vyama vingi mazungumzo ya kisiasa ni kitu cha kawaida sana na hakuna cha ajabu hapo."
  "Sasa kuanza kusema huyu fulani alikuwa hivi na mwingine vile kisiasa haipendezi, haya mazungumzo ya kisiasa yanaendelea kila siku hata sasa hivi unaweza kukuta wapo watu wanaendelea na mazungumzo. Sasa hii ya huyu bwana (Mpendazoe) inashangaza na kusikitisha."

  Alifafanua kwamba mtu anapofanya mazungumzo ya kisiasa kama kutaka kujiunga na chama kingine na kisha akaghairi, anakuwa ameangalia mambo mengi ya msingi ikiwamo wakati na kuongeza kwamba mazungumzo ya kisiasa na kuanzisha chama ni vitu viwili tofauti.
  "Ndiyo maana siwezi kusema kwamba siwezi kufikiria uamuzi huo au la. Haya ni mambo ya kisiasa unaangalia mambo mengi ya msingi, sitakiwi kujifunga kwamba siwezi kufanya hivi au la," alisema Sitta.

  Akizungumzia uamuzi wa Mpendazoe kuamua kuwataja majina kwamba alishiriki katika kuanzisha CCJ, Sita alisema: "Huyu bwana amenishangaza sana. Nadhani amekasirishwa na sisi kukataa ushauri wake... Mwanasiasa makini hawezi kupata umaarufu kwa njia hii. Katika siasa watu hawasemi kama alivyosema."
  Sitta alisema yeye ni mtaji wa kisiasa hata ndani ya CCM na anajivunia kwamba mabadiliko wanayotaka ndani ya chama hicho sasa yanawezekana.Aliwataka wanasiasa kujadili mambo ya msingi ya maendeleo kuliko kuanza kuzungumza mambo binafsi... "Kama ikiendelea hivyo, tunaweza kuumbuana sana."Alisema alijiunga na TANU Oktoba 3, 1960 hivyo uamuzi wowote wa kuhama CCM anapaswa kuufanya kwa umakini mkubwa.

  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCJ anena
  Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi ameelezea kushangazwa kwake na hatua ya Mpendazoe kuibuka na hoja hiyo sasa wakati chama chenyewe kimeshakufa.

  Mbali ya Muabhi, mwanasheria maarufu nchini na kada mwandamizi wa NCCR Mageuzi, Dk Sengondo Mvungi naye ameibeza hoja hiyo ya kada huyo wa zamani wa CCM.

  Muabhi alisema jambo la CCJ sasa hivi halipo kwani chama chenyewe kimekufa na kuhoji mantiki ya kuanzisha hoja hiyo katika kipindi hiki huku akisisitiza kamwe hawezi kuanza kuibuka na kuzungumzia kitu kisichokuwapo... "Hicho chama chenyewe hakipo, sasa kuanza kuzungumzia CCJ maana yake nini?

  Dk Mvungi na Katiba CCJ
  Dk Mvungi ambaye amekuwa akidaiwa kuwa ndiye aliyeandika katiba ya CCJ, alisema kamwe hajawahi kupewa kazi hiyo huku akisisitiza: "Loh! Kama ningepewa kazi hiyo si ningefurahi. Si unajua sisi Watanzania mtu akifanya kitu anaanza kutangaza ni mimi ndiyo nimefanya."
  Dk Mvungi alisema kamwe hakuwahi kuandika katiba hiyo ya CCJ huku naye akisisitiza: "Lakini, hivi kweli ni hoja kwa sasa kujadili CCJ ambayo imekufa? Tunapaswa kuangalia mambo ya msingi ya sasa, si yasiyokuwepo," Alisema Watanzania wanapaswa kuangalia jinsi CCM kinavyobomoka sasa hivi na si kuangalia kipindi hicho cha CCJ ambacho chama hicho tawala kiliweza kujipanga na kunusurika na mpasuko huo.
  "Sasa hivi CCM ndiyo inabomoka. Hapa ndipo Watanzania walipaswa kupaangalia lakini kuanza kusema huyu alikuwa CCJ, chama chenyewe hakipo, kweli hilo ni jambo la msingi kulizungumzia?" Alihoji Dk Mvungi.

  Alisema sasa hivi Rais Jakaya Kikwete, ametangaza chama kujivua gamba kitu ambacho alisema Watanzania wanapaswa kuonyesha mshikamano kwa kuhakikisha kinafanikiwa ili kuona watu wasio na madili wanang'oka.

  Nape: Nendeni kwa Msajili
  Kwa upande wake, Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa CCM, Nape Nnauye amewaambia wale wanaotaka kujua waanzilishi wa CCJ waende Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye ana rekodi zote.

  Juzi, katika mkutano wake alioufanya Njombe, Mpendazoe aliwataja Sitta, Nnauye na makada wengine wa CCM kwamba walikuwa waanzilishi wa CCJ lakini waliwasaliti Watanzania ili wapate vyeo ndani ya Serikali ya Rais Kikwete.
   
 2. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Sitta kawa mkweli ktk hili....
   
 3. m

  mjombajona JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 262
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jamaa mmoja kwenye comments za gazeti la Mwananchi kwenye hii habari kasema :
  yusuf 2011-05-18 00:41 Mh Sita umekuwa mwungwana kukubali bila ubishi kuwa ulishiriki kuasisi CCJ,maana yake uliwahi kumkana Rais wako ukiwa kiongozi.Unasubiri nini CCM?Kwamba wewe ni mtaji wa CCM na Mh JK, si kweli!Wewe ni mzigo mkubwa CCM.Kumbuka hotuba ya Rais kwenye semina elekezi Dodoma.Umepingana mara nyingi na serikali.Huna uwajibikaji wa pamoja.Unapenda sifa binafsi.Wenye akili wakakutosa kwenye uspika.Enzi zako za uspika ulizima hoja ya RICHMOND kiubabe,sasa imekula kwako.

  My take: Ni mtaji au mzigo kwa wa chama cha magamba ? Karibuni tujadili.

  Quote
   
 4. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Namheshimu sana Sitta, kipindi chake akiwa spika alijitahidi sana kutokuwa bias bungeni. Bunge lilikuwa huru, siyo kama sasa hivi! Anaonyesha ni mtu anayependa mabadiliko, ila chama chake tu ndiyo kinachomwangusha
   
 5. ChescoMatunda

  ChescoMatunda JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,189
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mara nyingi ukipingana na (wavua magamba mti uleule)kisiasa unakuwa mzigo kinachosubiriwa ni muda tuu wa kutua mzigo wenyewe!
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hii sasa ndiyo siasa siyo bwana mdogo Nape naanza ooh ulizeni ilikufaje, mara nenda kwa msajili wa vyama ukitaka kujua waanzilishik ni nani mara ntawajibika...... just endless stories na ndiyo maana hata hao waandishi hawaishi kuuliza jambo hilo Nape need to stand up and just say yes nilishiriki so what? Kuchengesha chengesha kunamfanya aonekana kuna kitu anakwepa au anaogopa life beyond that piece.
   
 7. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  kwa hili six ameonyesha ukomavu wa kisiasa sio kurukaruka ka anavyofanya Nape, nape anahitaji kujifunza he has a lot to learn isije akawa illeterate
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  May 18, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Kila nikiziona hizo herufi za CCJ naanza kucheka. Sijui kwa nini tu lol
   
 9. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hahahaha....kuna watu huku walikurupuka nayo...hadi kuishia kuikashifu Chadema! Kumbe wanaingizwa mjini na mchezo wa kuiga!
  Anyways....Ilionyesha true colours za watu wengi kweli humu!
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  I know why mate!!!!!! hahaha ahaha ahaha!
   
 11. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2011
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Ukisikia upunguani wa akili basi ndio huu. Kwamba CCJ ilishakufa na hakuna umuhimu wa kuijadili sijadhani kama ni sahihi. Julius Kambarage Nyerere, Jomo Kenyata, George Washngton, Osama Bin Laden, DECI, NASACO, UDA nk ni baadhi ya watu na taasisi zilizokufa siku nyingi lakini hadi leo vinajadiliwa kwa sababu vimeleta impact katika historia ya maisha yetu hapa duniani iwe kisasa, kiuchumi na kijamaa.

  Hivyo si sahihi tusiijadili CCJ eti kwa sababu ilishakufa. Ni lazima tuijadili kwa sababu ilichukua muda wetu mwingi kuijadili ikituhadaa kwamba yenyewe ndio mkombozi wa kweli kumbe wapi. Tukifumbia macho mambo yaliyopita ndio chanzo ya kujirudia mambo kama hayio..

  Nimemaliza..
   
 12. Makucha

  Makucha JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kazi nzuri aliyoifanya Sita akiwa Spika haina ubishi kwa wapenda uwazi, ukweli na maendeleo. Ametuamsha na matunda yake yanaonekana na anayebisha siyo kwamba hajui bali ni mbinafsi tu, period. Kila binadamu ana mapungufu yake kwani hakuna binadamu mwenye sifa ya Malaika.
   
 13. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  CDM mfikirie mara mbili kuhusu Mpendazoe, huyu ni mropokaji ipo siku atakuja kuwaumbua kwani siku yeyote atakimbia CDM na kujiunga na chama kingine. Nawashangaa mnampa kipaza sauti na kuropoka maneno mbovu mbofu jukwaani. Siasa za kusema watu binafsi mzikomeshe muanze kutuambia ni namna gani mtatuondoa watanzania katika lindi la umaskini.
   
 14. n

  niweze JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sitta, Mwakyembe kweli kuna michango yenu mmeitoa kwa Taifa lakini kwa jambo hili sina hamu na nyie. Inawezekana kabisa Sitta na Mwakyembe nyie ni wanafiki wakubwa ktk nchi hii yetu. Najua mnataka kuonekana mlionyeshwa na kuendelea kuonyesha kutopendezwa kwenu kuwa ndani ya ccm, ukweli ni kwamba bado mpo ndani ya chungu kinachowaumiza watanzania.

  Kuna mambo mengi ya kuwauliza Sitta na Mwakyembe na moja wapo ni hili, kilichowarudisha ndani ya hili gamba la mafisadi na wezi ni nini? Majibu ya Watanzania wengi kuhusu mwelekeo wenu wa kisiasa ni sawa na huo wa Lowassa na Rostam. Ingawa tunajua mnataka sana tuwafahamu kwamba hamtaki kula hadharani bali mnataka kula nyumba ya mlango wa chumbani na kupuliza wakati huo huo. You can't and you will never serve two master, the devil (ccm) and God himself. Uchaguzi wa Sitta na Mwakyembe kubaki au kurudi kundi la kikwete linaonyesha kweli hawa makada wana uroho wa madaraka na njaa za pesa. Kwa haya yote tumewatambua Sitta na Mwakyembe kama Yuda wa Watanzania na sio kama yeye Sitta alivyotaka tumwone kama anavutia vyama vingi. Sidhani kama Watanzania tuliotaka arudishwe kuwa Spika tungejua haya yote tunge-support harakati za Sitta, Sitta is playing kamali na maisha ya Watanzania....

  Nape kama tunovyojua this is new coming Rostam kinder, the boy anataka utajiri kwa kutumia tactics za Rostam 2011, Nape hujui kama kesho ccm itakuwa shimo la mita ngapi chini ya udongo... soma harakati za wakati wewe, Ridhiwan na January. Just pimping Tanzanians.

  "Change and Revolutions go hand and hand with Sacrifices"
   
 15. M

  Marytina JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nampongeza Sitta kwa hii move
  6 NI MTAJI KWELIKWELI
   
 16. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Haijaniingia kichwani ni jinsi gani Msomi kama Mvungi anadai hakuna haja ya kuongelea mambo ya CCJ kwa sababu ilishakufa. MMh huyu ni mtaalamu wa sheria anaongea hivyo!! Ingekuwa ni hivyo basi tulikuwa hatuna haja ya kudai pesa za EPA kwani zilishaibwa na mhusika mwingine aliyesimamia wizi huo alishachomoka (Balali). Hakieleweki mpaka wasaliti wote wa demokrasia ya Tanzania wametajwa wote.
   
 17. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sasa nimeamini kweli SITTA alimtoa Lowasa kwa chuki binafsi za kukosa uwaziri mkuu.

  Jamaa ni mbinafi huyu ingekuwa enzi ya Mwalimu angeondolewa kwenye chama arudi Tabora akarine asali
   
 18. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi na aliyekuwa mwenyekiti wa CCj baada ya kurudia kulivaa gamba kaishia wapi?
   
 19. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2011
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kwamba watu hawajmuelewa Mpendazoe, yeye hajasema kuwa tatizo ni kuanzisha CCJ , yeye anasema kuwa hao watu sita walimsaliti. kwa maana nikwamba walifyata mkia baada ya kitu fulani!
   
 20. h

  hoyce JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tuonyeshe huo ubinafsi nasi tuuone, la sivyo wewe una chuki binafsi naye, au una mapenzi na EL
   
Loading...