Sitta ajitosa mjadala wa posho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta ajitosa mjadala wa posho

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Jun 27, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,785
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Sitta ajitosa mjadala wa posho
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 27 June 2011 09:13 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta

  Lilian Lucas, Morogoro
  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amejitosa kwenye mjadala wa posho ulioanza bungeni hivi karibuni akieleza kuwa suala la kujadili posho za wanasiasa na watendaji wengine linatakiwa kuanzia ngazi ya chini.

  Alisema juzi katika mdahalo ulioandaliwa na Jumuia ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuwa fedha nyingi zimekuwa zikipotea na hata wananchi wanapojaribu kuhoji hakuna maelezo yanayotolewa kwao na baadhi ya watendaji wa serikali zikiwamo za vijiji.

  Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM) alisema kuwa malumbano yanayoendelea bungeni kuhusu posho za wabunge na watumishi wengine wa serikali hayana msingi na badala yake wanataaluma ndio wangetakiwa kulipwa vizuri tena kwa fedha nzuri kuliko wanasiasa.

  Alisema kuwa wanataaluma wangepaswa kulipwa zaidi kuliko wanasiasa kutokana na kuwa wamehangaikia taaluma zao kwa miaka mingi kuliko wanasiasa, akieleza kuwa siasa ni kitu cha kujitolea.

  "Sioni sababu ya wabunge kuendelea kujadiliana na kubishana juu ya suala hili la posho.

  “Kinachotakiwa ni kumlipa vizuri mtu aliyehangaikia taaluma yake tena kwa muda mrefu, inafaa apewe mshahara mzuri kulingana na taaluma yake, lakini kwa nchi yetu wataalamu wanalipwa mishahara midogo ambayo haikidhi hata mahitaji yao ya msingi.

  "Matokeo yake, wengi wakishamaliza elimu yao wanakimbilia nje ya nchi kufanya kazi au kugeukia siasa,” alisema Sitta na kuongeza:

  Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuambia mdahalo huo wa kujadili masuala ya Jumuia ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Jumuia ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuwa hali hiyo haina budi kubadilishwa.

  “Inashangaza kuona fedha nyingi zinapotea kuanzia vijijini na watendaji wake wamekuwa wakijilipa na kufanyia mambo yao bila kushirikisha wananchi na hata kutowasomea mapato na matumizi ya kijiji husika bila ufuatiliaji na wala hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika,”alisema.

  Pia, aliwataka wananchi hususani vijana kuwa wawajibikaji zaidi na kuweka uzito katika mambo ya msingi ya taifa na kuhakikisha wanakemea wala rushwa na wale wanaojitajirisha kwa maslahi yao na kuwanyonya watu wa hali ya chini.

  Alisema ndani ya Serikali ya Tanzania kuna tatizo la uwajibikaji na watumishi wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kujisahau kuwa wanatakiwa kuwahudumia wananchi katika masuala ya kimaendeleo.

  Kwa upande wao, wanafunzi walishiriki mdahalo huo walihoji ni jinsi gani wananchi wa Tanzania walivyoandaliwa katika kuleta ushindani katika Jumuia ya Afrika Mashariki kwani kila mara wameonekana kuwa nyuma katika ajira kwenye jumuia hiyo.

  “Katika hili, wanasiasa wameonekana kuwa ndio wanaoharibu mfumo mzima kutokana na kuweka siasa zaidi mbele badala ya kutenda kazi ya kushirikisha wananchi hasa wa hali ya chini,”alisema Christian Makala, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Kitivo cha Sheria.

  Alisema wanasiasa wengi wanapokuwa majukwaani hasa wakati wa kuomba kura wanaonekana wazalendo, lakini pindi wanapopata madaraka ikiwamo kuingia bungeni hubadilika na kujisahau na kukubaliana na mambo kwa maslahi ya vyama vyao[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  -----wana magamba wampe jamaa ajaribu upreda, ni mara mia yake kuliko yeyote humo CCM sio waziri mkuu huyu wa ajabu kabisa
  hongera sitta umejivua gamba kiuraini katika ili safi sawa
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  HTML:
  Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM) alisema kuwa malumbano yanayoendelea bungeni kuhusu posho za wabunge na watumishi wengine wa serikali hayana msingi ....................................
  Pambaaf!
  Huyu nae anapenda sana senti huyu babu!
  Kwa kauli hiyo anaona wabunge hawastahili kuachilia hizo posho!
  Kwa hili siuungi mkono, hoja ya POSHO ina mashiko sana, na ni ya msingi!
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  toka zamani nilisha sema huyu mzee sina imani ne....na kwa kuupotezea mjadala wa richmond sitamsamehe maisha....hakuna zee nafiki kama hili
   
 5. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi sio huyu Jamaa aliyeongeza mishahara na POSHO maradufu....., kweli ukistaajubu ya Ngereja utaona ya Sitta...
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mbona Sitta kama bado haweka wazi msimamo wake juu ya posho za Wabunge!
  Amezunguka zunguka tuu.
   
 7. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  yeye kasema posho kwa wabunge NO bora wataalamu
  mimi naona tumuhukumu kwa hii kauli yake kulingana na mjadala waposho

  TAIFA KWANZA
   
 8. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM) alisema kuwa malumbano yanayoendelea bungeni kuhusu posho za wabunge na watumishi wengine wa serikali hayana msingi na badala yake wanataaluma ndio wangetakiwa kulipwa vizuri tena kwa fedha nzuri kuliko wanasiasa.
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,785
  Trophy Points: 280
  umejibiwa
   
 10. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  CCJ founder! What do you expect?
   
 11. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ----Hivi makinda angekuwepo kwenye lile bunge kama spika au msekwa angefanya kama SITTA ?
  kamati ya mwakyembe iliundwa na bunge gani kama sio la 9?

  --- tuache unazi na tu[ongeze inapobidi hisia zako binafsi kwa mambo binafsi sio nafasi yake kwa manufaa ya taifa sasa unachukia hata mazuri yake kwa faidi ya nani?
   
 12. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ---manashindwa kuhukumu watu ka CHEYO siku hiyo ya mjadala wa posho alikuwa wanaupigia debe kama ana akili nzuri.
  kwa mfumo wa bunge wa sasa huwezi kumlaumu SITTA watu wamekuja na hoja ya kuongezewa posho na kura wamepiga hoja ikapita sasa yeye hafanyeje na spika hatakiwi kuwa na upendeleo.

  ---- wake wa uspika wake DR SLAA mzee wa ukweli alikuwa kinara wa hoja bungeni kwa sababu hakuwa na hupendeleo,
  hapana kuna wakati hunapaswa kuwakubali baadhi ya wana magamba, UNAFIKI huo manaosema tukipima vizuri ni mbinu ya kila mwana siasa kila vita lazima inafika wakati unarudi nyuma sio kusonga tu unaweza kujikuta kwenye mitego.
  he is playing very well ,
  NITAJIENI MWANSIASA DUNIANI AMBAYE SIO MNAFIKI
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,274
  Trophy Points: 280
  Na ile ofisi ya Spika kujengwa kule Urambo je kuna bunge kule Urambo? au Uspika ni cheo cha kudumu? Hongera sana Mapacha watatu kwa kutuondela huyu msanii, kwani sisi tunahitaji Spika na sio mshehereshaji ( mc )
   
 14. Makoye Matale

  Makoye Matale JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2011
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 6,480
  Likes Received: 450
  Trophy Points: 180
  Sitta ndiye chanzo cha posho batili za wabunge, atuambie alipokuwa Spika alisaidiaje kuboresha maslahi ya wanataaluma.
   
 15. k

  kazuramimba Senior Member

  #15
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  huyu sitta mnafki na mzandiki wa kutupa kamuaibisha lowassa kwa ahadi ya kuwa spika baada ya muhula wa kwanza kuisha bt sasa kapigwa chini anajidai nae ni mkosoaji wizi mtupu.
   
 16. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  makinda ni tofauti na sitta yeye hatakiwi
  sitta ni tofauti na makinda naye hatakiwi

  unajua nini hii nchi ina IMEFIRISIKA kutoka na watanzania wengi kuwa watu
  wa porojo badala ya FACT
  kuna ushabiki sana kwa sasa kuliko hali hivi kila kitu tunataka afanye DR slaa
  REALLY
  ndio maana DR wa ukweli jana amesema hataki mashabiki anataka watu wanao jua nakusimamia ukweli
  kipindi bunge linapandisha posho sisi wananchi tulikuwa wapi?

  huyo ZITTO mwenyewe anayezipinga anaitwa mnafiki na mtafuta umaarufu
  tujadili hoja SITTA kasema posho kwa wasiasa hapana na huu ni mtaji safi kwa CHADEMA
  tunashambulia watu mpaka wanaposema ukweli na mambo muhimu kwa taifa!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  kama tungekuwa na misimo kiasi hiki leo DR slaa angekuwa ikulu
  wote nyie wanafiki wakubwa kuliko sitta ni nani alikwenda kulinda au kupiga kula wakati wa uchaguzi
  au hata kuamasisha majira kufanya hivyo kwa kuchagua viongozi bora?

  SITTA alikuwa na kura ngapi bunge kiasi cha kuongeza posho pekee yake
   
 17. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Matola
  hiyo kitu hata mimi nimewahi kuisikia lakini je hiyo hapa hapo chini umewahi kuiona pia nadhani.
  ili habari yawezekana ilikuwa na makosa yawezekana ile ni offisi ya MBUNGE wa urambo
  hii ni issue ya comon sense tu
  kila mtu anajua haiwezekana SITTA akawa spika kwa maisha

  halafu mbona hizo offisi zijengwe mbili kama mwaka mmoja urambo na DODOMA

  watanzania tujifunzi utafiti wa habari na ukweli wa mambo la sivyo hii nchi itabaki hapa au kudidimia
  ni sisi wananchi ndi tutaikombo nchi sio wanasiasa wao wako kazi
  kama tusipo waiga wazungu kwa kutokuwa mashabiki wa vyama tumeliwa
  kila mtu apewe CREDIT pale anapofanya kwa ufanisi


  [h=1]Mhe. Anna Makinda atembelea ujenzi wa makazi ya Spika mjini Dodoma[/h]BY DULLONET TANZANIA – DECEMBER 27, 2010POSTED IN: HABARI KUU

  [​IMG]Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa makazi ya Spika yanayojengwa Dodoma kutoka Maafisa wa Bunge pamoja na wakandarasi kutoka Wakala wa Ujenzi (TBA). Kulia kwake ni Afisa Tawala wa Bunge, Athumani Kwikima
  [​IMG]Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akisikiliza maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa makazi ya Spika yanayojengwa Dodoma kutoka mtunza vifaa wa kampuni inayosimamia ujenzi huo mjini Dodoma.
  [​IMG]Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akielekeza jambo mara baada ya kutembelea maendeleo ya ujenzi wa makazi ya Spika yanayojengwa Dodoma jana. walioambatana nae ni maafisa toka Ofisi ya Bunge, wakala wa Ujenzi na wakandarasi wa Kampuni inayojenga jengo hilo.
  [​IMG]Jengo la Makazi ya Spika linavyoonekana kwa sasa.(Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge)
   
 18. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu mtu alishawahi kutoa maelezo kuhusu ile Ofisi ya Spika wa Bunge aliyoijenga Jimboni kwake?
   
 19. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  tatizo la watanzania wa leo tunasima kwenye ushabi kuliko ukweli,

   
 20. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Rais Kikwete amefungua ofisi ya Mbunge wa Urambo ambaye hivi sasa ni
  [video=youtube_share;BhaAxQskQAk]http://youtu.be/BhaAxQskQAk[/video]

  hiyo sio ofisi ya SPIKA ni ofisi ya mbunge wa URAMBO mtu yeyote hatakayeshinda basi hiyo ndiyo ofisi yake na huu ni mpango wa serikali kujenga ofisi za wabunge kila jimbo

  OFISI ya spika hiyo hapo chini
  hacheni ushabi wakuu tutapotea
  mimi sio mwana magamba lakini kwenye ukweli nitatetea tunaboa nchi wenyewe baadaye tunalia lia


   
Loading...