Sitosahau siku ambayo tulifika Mbeya saa saba mchana. Njia nzima nilitubu dhambi zangu

Inatokea unaweza kuwa 160 akakupita mtu kama vile upo 80 unajiuliza yeye amekanyaga ngapi.... Ndo raha za barabarani hizo...
Nilikimbizana v8 mi niko na chaser toka himo maeneo ya same akikaa mbele anapunguza hadi 140 nikikaa mimi mbele hata niko 160 ananipita, kuna sehemu akawa analipita na nkaunga nyuma amemaliza basi na mi nkamuungia na yeye, kuja kucheki kisahani nipo speed 180 hadi mi mwenyewe nkawa naogopa, kufika livepool pale nimepaki sikuzima gari ila nkafungua boneti nao wakafika, walishuka wote kwenye gari wa4 wakaja kuangalia kwenye engine ya gari, hawakua watanzania wakanionyesha kwa ishara wee ndio unaendesha hii gari nkawaambia ndio, wakawa wanatingisha kichwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
babu hii ni kweli kabisa dar mpaka mbeya magari yalikuwa yanaingia saa 9 hadi saa 10 kwa zile enzi hizo ndio luxury yaani kama Embakassy,Tawaqal, daaa na KISWELE injini nyuma nazani hiyo iliyoweka record yakuingia saa 7 ni kiswele babu yaani enzi hizo tupo shule tunashindana kuchora magari tu ya kiswele au embakassy. watoto wa sikuhizi hawajui haya mambo wanazani story ya kupikwa hii. siku hizi dar mpaka mbeya ni masaa zaidi ya 12 sijui tumekosea wapi aisee.
 
Sio Matema Beach wala Safina iliyoingia Mbeya SAA saba, ni Scania 113 TZH 710 ikiendeshwa na Giriki na kondakta wake alikuwa Ally Bonge.
Nilikuwa ndani ya hiyo gari kuanzia inaanza safari Mnazi Mmoja hadi Mbeya. Na Mimi nilikuwa ni mdau Mkubwa sana wa mabasi enzi hizo Ofisi yangu ukiwa jirani na Ofisi ya mabasi ya Embakassy.
Giriki wa Tawaqal, nitamkumbuka daima. Tulikuwa tunasoma Iyunga Tech. Kipindi cha likizo tunakodi basi kurudi nyumbani Moro na Dar.
Sitasahau tulifika stand ya Moro mjini ambayo sasa hivi I'm at u I am na daladala mishale ya saa tano na roho asubuhi!!
Ilikuwa 1997

Sent using Jamii Forums mobile app
 
story ya uongo hii...! hakuna gari ya kutoka dar 12 asbh ikafika Mbeya 7 mchana..! Hata barabara ingekuwa tambarare ni imenyooka straight na unapita mwenyewe barabarani..!

Hakuna kitu kama hicho

Inawezekana mjomba mimi juzi juzi tu hapa 2013 bus lilini overtake niko speed 160km/hr , bus la njombe linaitwa happy africa


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana na wewe. Nchi yetu imejaa vibao vya spidi ya 50 kwa saa. Maendeleo tutayapata lini kwa mtindo huu? Nchi za wenzetu kama Afrika kusini kuna vibao hadi vya spidi ya 120 kwa saa. Leo hii unatumia masaa 17 Mbeya Dar.
its crazy to drive 800kms for 12hrs,its madness!!! tatizo letu watanzania hatujui kuwa ni wajibu wa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia kuturahisishia maisha,wengi wengi tunanyenyekea serikali kama inatufanyia sisi favour kutujengea miundo mbinu bora wakati ni WAJIBU WAKE.
 
Hata miaka 7 ama nane iliyopita ilikuwa gari linatoka Mwanza saa 9 ama saa 8 na madakika mchana linasoma mitaa ya Dodoma alafu saa 12 kasoro lipo Morogoro by saa 2 kamili ama saa 3 Dar (siku hizi magari yapo nyuma masaa 3 mpaka 5 kwa muda wa zamani alafu ajali enzi hizo ilikuwa za kuhesabu yaani ikitokea ajali ni kilio hasa lakini inakuja inapita miaka kadhaa
Yap, niliwahi kipanda Ally's, ilikuwa December 2010. Tulikuwa na team ya JKT basketball wametoka kuchukua ubingwa wa Tz Mwanza. Toka saa 06:00 asubuhi, saa mbili na dakika kumi usiku watu wanapokelewa kwa na MBrass bend Ubungo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya 90. Sikumbuki vizuri ilikuwa Bus gani kati ya Matema au Safina. Tulitoka Dar saa 12 asubuhi kwa mara ya kwanza naelekea Mbeya.

Tulitoka na hilo Bus tukavuka mataa tukaitafuta kimara mbezi tukakamata barabara sasa ya Mkoani huko mbele.Hapo ndo nilianza kuona milango ya mbinguni ikifunguka na kufunga.

Sikuwahi kuona Dereva anapiga mti/mpini kama yule jamaa.Gari ilikuwa inakimbia sijapata kuona duniani. Abiria tulikuwa tunaogopa hata kukohoa au kupiga chafya kwa wasiwasi kuwa unaweza mtingisha dereva ukasababisha ajali.

Dereva alikuwa anapiga mkono/mpini balaaa njia nzima nikawa nasali nikitubu dhambi zangu zote na kuomba msamaha maana sikuwa na hakika kama tungefika salama. Nilikumbuka mapambio mbalimbali na nyimbo za kuelezea Ukuu wa Mungu.

Yeye dereva alikuwa kimya akihesabu tu gear zake kama vile anasoma Rozari au Tasbihi na wakati mwingine akibadilishana maneno mawili matatu na konda.

Alipiga mpini kiroho mbaya/ile kinyama sana. Saa saba na robo anaanza kupangua gia kaingia town tupo Mbeya.Aisee siwezi sahau safari ile nilikuwa naona mbingu zinafunguka na kufunga. Nawakumbuka ndugu na jamaa zangu huku machozi ya kitoka ila tulifika.

Ghafla tuliona gari ya Polisi imetuunganishia mitaa fulani hivi kumechangamka.Dereva hakusimama akaendelea kupiga mpini mpaka tumefika stand ....

Tulikuja shtuka tumefika stand watu wamejaaa hawaamini.Nadhani jamaa aliweka historia haikuwahi kutokea hapo nyuma. Tumefika stand bus imesimama akazipangua gia mpaka zero akaiacha gari inanguruma yeye kaegamia usukani. Baada ya dakika kadhaa Polisi wakafika. Wakamfuata dereva mbele wakamwambia ashuke wakamtia pingu. Wakaondoka naye.

Nakumbuka mimi nilifika nyumbani kwa wenyeji wangu wanatenga meza wale chakula cha mchana.lile bus ilikuwa lielekee Kyela alienda nalo dereva mwingine yule jamaa walimweka ndani.

Najiuliza yule dereva aliendelea na upigaji ule wa mpini? Na je kwa sasa yupo wapi?
pale iyovi viti havikaliki kwa kona zile
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom