Chizi Maarifa
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 10,471
- 23,744
Miaka ya 90. Sikumbuki vizuri ilikuwa Bus gani kati ya Matema au Safina. Tulitoka Dar saa 12 asubuhi kwa mara ya kwanza naelekea Mbeya.
Tulitoka na hilo Bus tukavuka mataa tukaitafuta Kimara Mbezi tukakamata barabara sasa ya Mkoani huko mbele. Hapo ndo nilianza kuona milango ya mbinguni ikifunguka na kufunga.
Sikuwahi kuona Dereva anapiga mti/mpini kama yule jamaa.Gari ilikuwa inakimbia sijapata kuona duniani. Abiria tulikuwa tunaogopa hata kukohoa au kupiga chafya kwa wasiwasi kuwa unaweza mtingisha dereva ukasababisha ajali.
Dereva alikuwa anapiga mkono/mpini balaaa njia nzima nikawa nasali nikitubu dhambi zangu zote na kuomba msamaha maana sikuwa na hakika kama tungefika salama. Nilikumbuka mapambio mbalimbali na nyimbo za kuelezea Ukuu wa Mungu.
Yeye dereva alikuwa kimya akihesabu tu gear zake kama vile anasoma Rozari au Tasbihi na wakati mwingine akibadilishana maneno mawili matatu na konda.
Alipiga mpini kiroho mbaya/ile kinyama sana. Saa saba na robo anaanza kupangua gia kaingia town tupo Mbeya.Aisee siwezi sahau safari ile nilikuwa naona mbingu zinafunguka na kufunga. Nawakumbuka ndugu na jamaa zangu huku machozi ya kitoka ila tulifika.
Ghafla tuliona gari ya Polisi imetuunganishia mitaa fulani hivi kumechangamka.Dereva hakusimama akaendelea kupiga mpini mpaka tumefika stand ....
Tulikuja shtuka tumefika stand watu wamejaaa hawaamini.Nadhani jamaa aliweka historia haikuwahi kutokea hapo nyuma. Tumefika stand bus imesimama akazipangua gia mpaka zero akaiacha gari inanguruma yeye kaegamia usukani. Baada ya dakika kadhaa Polisi wakafika. Wakamfuata dereva mbele wakamwambia ashuke wakamtia pingu. Wakaondoka naye.
Nakumbuka mimi nilifika nyumbani kwa wenyeji wangu wanatenga meza wale chakula cha mchana.lile bus ilikuwa lielekee Kyela alienda nalo dereva mwingine yule jamaa walimweka ndani.
Najiuliza yule dereva aliendelea na upigaji ule wa mpini? Na je kwa sasa yupo wapi?