Sitosahau nilivyokoswa na risasi nikiwa baa

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
2,011
4,165
Habari wanajamii,

Salam kwenu na natumai nyote ni buheri wa afya, Naona nielekee kwenye hoja husika.

Ilikua ni siku ya mapumziko(weekend) siku ya jumapili tarehe 22 ya mwezi wa 9 mwaka 2007 maeneo ya mbezi beach eneo linafahamika sana kwa jina alimaarufu (Africana) njia ya kuelekea whiteSands au kwa zena, maeneo hayo kuna bar maarufu sana inafahamika kwa jina la highbury hapo ndipo lilikua eneo langu la kupumzisha akili baada ya mihangaiko ya kutwa nzima.

Siku hiyo ilikua ni mapumziko na ilikua ni jumapili nilitoka jioni na kuelekea kwenye hilo chimbo kumwagilia moyo na kampani ya wadau kadhaa kama ilivyokuwa kawaida yetu kujumika pamoja na kupata viburudisho kadhaa na kujiopolea warembo katika bar hiyo na walikua wazuri kweli kweli, Sasa wakati tukiendelea kumwagilia moyo hapo mdaa uliendelea kusonga hadi ilipofika majira ya saa nne(4) usiku ziliingia gari mbili aina ya land cruiser nyeusi na walishuka mababiloni nane(8) wakiwa wamevalia makoti marefu meusi na kofia aina ya Pama huku wakiwa wamefunika nyuso zao na walishikilia silaha aina ya mtutu(A.K.A 47) ghafla ulisikika mlio mkali wa risasi mbili zilizopigwa hewani na kuamuru watu wote tulale chini na tutoe kila tulichonacho tuweke pembeni, Sasa mimi wakati wa hamaki zikiendelea na purukushani za watu kujihami na vurumai zile nikaona nikimbilie counter kwakuwa nilijua kuna mlango wa nyuma nilifanikiwa ila huu ndio ungelikua mwisho wangu wa maisha kwani kati ya wale majambazi alifyatua risasi iliyonikosakosa usawa wa kichwa na kwenda kupiga nguzo za counter na kuacha tundu(shimo) kubwa sana.

Nashukuru nilifanikiwa kuokoa maisha yangu siku hiyo maana ilikua ni hatari sana hata kupelekea wahudumu wawili kufariki palepale baada ya kupigwa na risasi siku hiyo na baadhi ya wateja waling’olewa meno kwa kupigwa na vitako vya mtutu wakati wa uporwaji wa mali walizokua nazo siku hiyo.

Hili tukio sitakuja kulisahau maishani mwangu kabisa na huwa namshukuru mungu kwa ujasiri alionipa siku hiyo.
 
Hela inatafutwa, uhai ni mara moja: Kuna jamaa yangu au bocy wangu back in the day nikiwa Arusha, alikuwa wa mererani.

Mtu mwema sana, ila akilewa alikuwa anapenda sana kushika shika bastola yake, mimi nikishamwona mtu ni limbukeni huwa nakaa mbali.

Nikaondoa social life na yeye kabisa, ukishakuwa mtu mzima na watoto lazima uishi maisha mazuri na yanayoeleweka sana, ukocheza, unaacha watoto wanateseka.
 
Ilitokea hapo Kino meridian, hawakua na nia kupora walevi ila wamekimbizana na mtu wao huko kaingia mle mbio karuka kaondoka nyuma kuna chimbo pale.
WaCuba tunajua.
Hatujakaa vizuri jamaa hawa hapa vyuma viko juu zikapigwa mbili juu ta ta aah ukiskia hivyo lala chini tu sio kukimbia ka mwehu.
Acha simu counter nilikua nimekaa hapo na Deborah ananihudumia.
Jamaa wamemtafuta wamkosa aliruka ukuta mi namuona.
Aah wakarudi huku wakasachi kila mtu wakatimka.
Nilikua na Nokia vile vidogo nusu keypard nusu screen wakalamba
enzi hizo ndo smart Phone.
 
Back
Top Bottom