Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

David Harvey watu kama nyinyi huwa hamtoi sadaka, umetoa sana 1,000. Hata hivyo hata kama hautatoa unadhani huyo mchungaji kuna kitu atapungukiwa atapungukiwa?
 
Ukimtolea Mungu hauapashwi kuumizwa zimetumikaje, kama wanatumia visivyo watajibu kwa Mungu, mi nikitoa Imani yangu inanieleza kuwa nimemtolea Mungu na wahusika wanapasw kufanya kama Mungu alivyoelekeza, wakizielekeza visivyo sio kazi yangu kuwahukumu hiyo ni kazi ya Mungu niliye mtolea. #Period #faith
 
Karibu mi nishaachaga siku nyingi sana afadhali uwape yatima, na wasiojiweza MKUU
 
Ni mfu ndio hata kanisa linakufa kwa sababu limeanza kumomonyoka toka pale Vatican city tena St. Peter's Cathedral. Ulawiti wa watoto unaanzia juu lakini walifumbia macho kitu ambacho kimezikumba parokia nyingi hata huku Afrika; embezzlement nayo imekuwa ni ya kawaida wale waliovaa kofia ya utawa ndo wamekuwa chanzo cha haya yote-mapadri wanagombania matoleo, hela na mazao ya kuwategemeza (mapadri&masista) ndo maana kondoo nao wameona waanze kujipigia pesa maana hata hofu ya Mungu watu imeisha.
Napenda sana watu warudi kwenye mstari ila bahati mbaya wale walioshika usukani wa kuendesha makanisa wengi ni wanyang'anyi kama wanyang'anyi wengine ispokuwa wao wanatumia Psychology, Philosophy na knowledge ya Theology waliyonayo kuwapora masikini wa dunia hii. Mtumishi wa Mungu anadhira kuchukua sadaka kisa anadai wametoa kidogo; kidogo???? wakati hajui huyo mtu aliyetoa kidogo katoa sehem gani ya kipato chake na kaacha kiasi gani kwake.
Sasa wewe naona kuna kitu unakitafuta...
 
Una Hoja Mleta Mada Ila Jaribu Kuchunguza Kwanza ....... Yani Ufanye Kama Research Katika Kanisa Lako Sadaka Zinaenda Wapi

Maana Taratibu za Makanisa Sadaka Huwa Zinatangazwa Na Matumizi yake sasa Labda Hilo kanisa lenu

Ingawa Sadaka Maana Yake Umetoa Htakiwi Kuangalia Nyuma.. Atajuana na Mungu wake anayeitumia Sadaka Vibaya
Atajuana na Mungu wake? Mbona anajuana na mJapan tu
 
Mafundisho anayokupatia huyo mchungaji ni bora zaidi ya hiyo sadaka yako toa sadaka na si imeandikwa kila mtu atalia madhabahuni mwake
Anatoa mafundisho ili apewe pesa anunune BMW??????? Yatima, wajane, wenye njaa wako wapi?
 
Yaani hapo Ndio umemtolea mungu, Toa tu....!
 
Sadaka haina maelekezo ya mtumiaji, ukitoa maelekezo haina tofauti sana na misaada ya nchi za magharibi. Muangalie Mungu unayemtolea, usiangalie anatumia nani na anatumiaje. Yeye ndiye atakayeitolea hesabu kama imefanya kazi iliyokusudiwa na Mungu au imeenda kwenye anasa. Kuna siri kubwa kwenye kutoa sadaka.
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema
Umesema hutatoa tena sadaka. Umekosea sana. Wkati wa Agano la Kale sadaka zilikuwa za kuteketezwa. Ukishatoa sadaka, umefanya wajibu wako. Hesabu imeteketezwa. Matumizi yake yasikusumbue. Mungu atashughulika na watu hawa. Kama una uhakika mahali unaposali kweli yote inafundishwa, wewe endelea kutoa sadaka na fungu la kumi. Mengine yote mwachie Mungu. Hao yatima na wenye uhitaji nao wanahitaji msaada wako. Wasaidie kwa jinsi unavyoona inafaa na Mungu aonaye sirini, atakubariki sana.
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema
Toa wazid ku_enjoy jamani
 
usiishi kwa kukariri ndugu yangu kwa utafiti wangu mdogo niloufanya japo mimi ni muislam wachungaji wengi wamesoma na wana ujuzi wao ama ajira nyingine tena zenye mpunga mkubwa sana zaidi ya uchungaji, wakristo hasa wa madhehebu makubwa huwa hawatoi nafasi ya uchungaji kwa akila mtu tuu kuna vigezo wana angalia ikiwemo elimu..sasa tuambie ilo kanisa unalo sali wewe nilipi...? usije ukawa uanasali kwenye kanisa la waabudu shetani harafu unatuletea utoto hapa
Hiyo elimu ya wapi,wakati mitaaaan tunawaona watu wanaaanzia kwenye nyumba zao,mwishowe anaaanza kuungaunga banda,mpaka linakamilika.
Hiyo elimu kaipata lini,labda elimu ya kupiga pesa,harafu ukiandika rudia kusoma na kutafsir ulichoandika"MNAFIKI WEWE"
 
Back
Top Bottom