Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Huenda alitoa sadaka 500 tu na povu la mtoka
 
Nakuunga mkono ndugu.. Kuna baadh ya makanisa haya wanata ya wokovu mpaka sadaka unapangiwa utoe sh ngapi.. Je ndo yesu alivofanyaga?? Wenye sadaka kubwa wanakaa mbele nyie makapuku nyuma... Kumuona mchungaji mpaka ulipie kwa mfano kuna mmoja anajiita nabii et kumuona afanye maombez hapo ni 250000/= tsh na ushahid ninao.. Yan sa hv makanisa haya ya wokovu yamekua ni ujanja ujanja tu.. Rudi kwenye kanisa lako la awali ndgu.. Hawa mtume na nabii ni wengi na ni wapigaji tu.. Binafsi makanisa hayo nilishayakimbia.. Tatizo wakristo tunafuata miujiza na sio neno la Mungu.. Tunatafuta miujiza na hatumtafuti Mungu...
 
Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki, tukiwa watoto mapadri wengi walikua raia wa kigeni. Mapato ya J2 yalikuwa yanatangazwa na kama mleta mada alivyosema pesa nyingi ilisaidia wazee, yatima, na wasiojiweza. Padri aliwahimiza vijana kuweka akiba na pia aliyekua na nidhamu na akiba yake aliongezewa mtaji, kuna sehemu watu wengi walihamia kutoka sehemu mbali mbali kwa kwenda kukata mkonge au ukuli bandarini, kwa mungozo wa mapadri watu wale wengi walinunua mashamba na kujenga nyumba sasa wameloea kabisa. Pale nilielewa maana ya lile neno baba paroko. Sijaelewa kwakua walikua wakipata misaada kutoka Vatcan au ilikuaje.

Makanisa mengi ya Pentekoste yanajitegemea yenyewe, sadaka ndiyo mshahara wa mchungaji na huo ndio umwezeshe kuendeleza kanisa, kutangaza injili, kulipa bills za umeme, maji, huduma za internet, nguo za wanakwaya, vifaa vya kanisa. Pia dini ni imani, kuna watu wanaimani kubwa sana na wako tayari kutoa nusu ya mali walionaya kwa Mungu kupitia kanisa fulani, unapomuona mchungaji anaendesha gari jipya si maajabu sana ikawa gari ile amepewa kama zawadi na mmoja wa waumini au msamaria mwema mwingine.
 
Enyi mlioamini! Hakika wengi katika watawa na makuhani wanakula mali za watu kwa batili na kuwazuilia njia ya Mwenyezi Mungu.
 
Ndugu umepotea ,badili mtazamo wako, unadhani yeye atakuombea mambo yako yanyoke akiwa na msongo wa mawazo? atapateje muda wa kukuombea na kuandaa neno la kukufaa huku watoto wake wamekosa ada ya shule? fikiri nje ya box ndugu . Hata hivyo kibiblia haija mlazimisha kutoa kwa wajane, yatima kwa hiyo anaweza kutoa au asitoe,ila biblia imekulazimisha wewe kutoa sadaka na fungu la kumi. Unapotoa usione unampa mchungaji bali ona umpa mungu hivyo hayo yote hayata kuumiza. Soma biblia malaki 3:8- 11
 
Karibu kanisa Katoliki...Mapato na matumizi ya sadaka yako utasomewa..
Umesema vyema mkuu lakini huku nako mambo si shwari katika baadhi ya parokia na majimbo. Kuna mapadri wanagombania hizo sadaka, kuna wale jamaa wanaohesabu hizo sadaka baada ya misa au jumuiya hupora hizo pesa. Hapa ninavyoandika mama mmoja jirani yangu amegeuza kigango fukani kuwa "sakosi" yake na anachota mapesa jinsi atakavyo.
Vikundi vya dini mashuleni na vyuoni ni miradi ya viongozi wa vikundi hivyo na wanapiga pesa bila aibu.
Mimi kutoa sadaka kanisani nilishaacha japokuwa si completely. Ninapokuwa na hela nawapa masikini zaidi yangu njiani na moyo wangu kujisikia vizuri lakini si kwa katekista, padri wala mchungaji.
 
Duuu teh teh teh! Toa baba mwezi ujao tununue helkopta tajiri kuuona uzima wa milele ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano ushtuki tu
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema
ok. Salam zao.
 
Umesema vyema mkuu lakini huku nako mambo si shwari katika baadhi ya parokia na majimbo. Kuna mapadri wanagombania hizo sadaka, kuna wale jamaa wanaohesabu hizo sadaka baada ya misa au jumuiya hupora hizo pesa. Hapa ninavyoandika mama mmoja jirani yangu amegeuza kigango fukani kuwa "sakosi" yake na anachota mapesa jinsi atakavyo.
Vikundi vya dini mashuleni na vyuoni ni miradi ya viongozi wa vikundi hivyo na wanapiga pesa bila aibu.
Mimi kutoa sadaka kanisani nilishaacha japokuwa si completely. Ninapokuwa na hela nawapa masikini zaidi yangu njiani na moyo wangu kujisikia vizuri lakini si kwa katekista, padri wala mchungaji.
Basi hiyo Parokia Kamati Tendaji na Baraza la Walei ni mfu..
 
Nimejaribu kusoma tena na tena bado sijaona sehemu ambayo umeeleza kuwa mchungaji amenunua magari hayo kupitia hayo matoleo ( Kwa tafsiri ya Padiri wa Parokia yangu kasema tunachotoa ni matoleo, kwani sadaka inahusisha kumwaga damu). Inawezekana huyo mchungaji ana miradi mingine, au kuna wahisani walijitolea kumnunulia hayo mashangingi. Ila usione ukadhani, halafu ukatenda dhambi bure.
 
Mkuu we endelea tu kutoa sadaka ili mchungaji wako aendelee kula bata, wivu wa nini?
 
kama mke wako ni muimbaji katika kanisa hilo au Ana kawadhifa fulani fulani chunguza vizuri pia utabaini mengi ila usijinyonge
 
Na mtaendelea kuibiwa tu mpaka mtakapotambua kuwa KUPELEKA pesa madhabahuni hakuna maana ya kutoa sadaka!

Bora haya makanisa kama KKKT na CATHOLIC.. hawa wanauongozi na majimbo yao..pesa inapelekwa huko na baadae inasaidia japo kwa UDOGO Sana..

Haya jiulize hao wanaofungua MIRADI yao binafsi na kuhubiri kwa KUJIKAKAMUA huko mtaani wanapeleka wapi??

Chukueni PESA zenu pelekeeni YATIMA nayo ni SADAKA..

Saidia wasiojiweza nayo ni SADAKA tena kubwa tu!
 
Hayo makanisa y mtu mmoja unategeneat afanyie nini hela zenu. Kwanza hakuna kutangaza mapato na matumizi
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema
Hamia kanisa katoliki sadaka yako unaiona inavyotumika kujenga makanisa, shule, huduma za afya. Huku uwazi na Ukweli ni banda na unaabudu Mungu wa kweli. Hili ndo kanisa la ulimwengu. Katoliki means a ulimwengu au kwa kiingerza universal. Karibu sana. Hili ndo kanisa la kristo aliloliacha.
 
Back
Top Bottom