Toa fungu la kumi wewe, utabarikiwa!!!!
Nimecheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeka
Toa fungu la kumi wewe, utabarikiwa!!!!
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.
Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.
Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.
Asanteni nawatikia EID njema
Huenda alitoa sadaka 500 tu na povu la mtoka
Bila kusahau na michepuo kibao.Unashangaa bmw na Brevis,watu wana ndege huko
Waafrika tuna imani zetu, nzuri tu. Hata Wahindi, Wachina nao wanaimani zao. Tatizo pana imani zinazotumia misuli mno kujitangaza.Mungu hataabudiwa tu Roma, KKK , agalikana. Mungu ni Roho, wamwabuduo imewapasa kumwabudu ktk Roho na kweli, we endelea kutoa sad aka; wala usife moyo.
Na huu usemi waumini wa kilokole umewapofusha...Kwani unatoaga shilingi ngapi? Ukiacha kutoa watatoa wengine kwani vyamadhabauni.uliwa na wamadhabauni
Hili somo la sadaka ni pana sana usipoangalia usipokua makini utampa sadaka asie hitaji sadaka yako ila nijuavyo mm unapoona kifungu kimeandikwa toa inamaana Mungu anawalazimisha mtoe wote bila kujali wewe ni nan manake hata mtumishi anatakiwa atoe halafu mkisha toa inaangaliwa nan wakupewa hapa moja kwa moja inaenda kwa wasiojiweza na kuijenga nyumba ya MunguMdau hili jambo la sadaka si jepesi sana kwa nionavyo Mimi. Huu ni mtazamo wangu,Sadaka ni swala la imani zaidi na pale itolewapo kwa imani inamaana kunatarajio unalo baada ya utoaji Wako. Kwa hakika ukitoa na ukapata tarajio lako huwezi acha toa sadaka.
Pia kunanamna unaweka nadhiri ( sadaka unayoitoa kwa ahadi kabla ya kuwa nayo mkononi ) kwamfano Yesu ukinisaidia nikapata kazi nitakutolea mshahara wangu wa kwanza wote,au Yesu ukinisaidia nikapata mtoto katika ndoa yangu baada ya miaka sita kupita bila mtoto nitafadhili mtoto yatima katika elimu ya kiwango flani na Yesu Kristo aliyehai akakufanikisha utatakiwa kufanya kama ulivyokiwa umeweka nadhiri yako kinyume cha hapo unawezapata shida,sasa katika hali kama hii si rahisi kukimbia jambo hili la sadaka.
Namalizia hivi sadaka unampa Mungu kadiri ya atakavyokuongoza lakini mpokeaji ni mtu ( mtumishi wake ) ,na sadaka isipotolewa kama sheria ndo unakuwa huru katika utoaji wako. Usihangaike kujua sadaka uliyotoa imeenda kutumika wapi,vipi na nani lamsingi sana sikuzote tafuta je nimepata matunda niliyokuwa nayakusudia ,hii itakufanya uendelee kutoa na kutoa aina tofauti za sadaka kadiri utakavyobarikiwa na kuongozwa,usiacha kumtolea Mungu aliyehai .
Kasome kitabu chote cha Malaki kitakusaidia.
Wasalaam
Haya makanisa yanayojiotea hawatangazi sadaka hata uwashikie bisibisiUna Hoja Mleta Mada Ila Jaribu Kuchunguza Kwanza ....... Yani Ufanye Kama Research Katika Kanisa Lako Sadaka Zinaenda Wapi
Maana Taratibu za Makanisa Sadaka Huwa Zinatangazwa Na Matumizi yake sasa Labda Hilo kanisa lenu
Ingawa Sadaka Maana Yake Umetoa Htakiwi Kuangalia Nyuma.. Atajuana na Mungu wake anayeitumia Sadaka Vibaya
Makanisa yanasajiliwa kama taasisi. Ili usajili kama taasisi ni lazima ufuate na kuzingatia vigezo na masharti likiwemo sharti la kuwa na bodi ya wadhamini. Kimsingi hakuna kanisa la mtu mmoja.Hayo makanisa y mtu mmoja unategeneat afanyie nini hela zenu. Kwanza hakuna kutangaza mapato na matumizi