Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Hiyo ni roho ya wivu,choyo na kijicho wewe mchungaji akibarikiwa kuna shida gani.Hupaswi hata siku moja kuacha kumtolea Mungu ya mchungaji atajua yeye na Mungu wake na pia kusaidia yatima si jukumu la mchungaji tu kwa sadaka zako pia unatakiwa usaidie yatima regadless umetoa na sadaka Mungu anakubariki wewe peke yako unapotoa kubariki wengine kwani wewe hupendi kumsaidia mtu akafanikiwa?Hiyo roho uliyojiwekea ni ya kuzimu mbona watu wanatoa sadaka watoto wao na ndugu zao wawapendao bila kulalamika kuwa watapata wapi wengine sembuse wewe hiyo elfu kumi ambayo utaitafuta na kuipata ingine .Kwani unadhani ni hela yako pekee ndo inamnunulia mchungaji gari?Acha kutoa uone kama hataendelea kubarikiwa.Neno la Mungu linasema nitambariki akubarikie na nitamlaani akulaanie na heri kutoa kuliko kupokea.Kwenda mbinguni si mchezo na wala hakuhitaji philosophy bali ni kufanya atakalo muumba wako.Kasema toeni zaka kamili glalani sasa wewe unaedhani zaka ni kumtajirisha mchungaji endelea kulikumbatia hilo pepo laumaskini niulize nikwambie.Watu wanatoa mpk magari kwa watumishi sembuse hiyo elfu moja yako.Shame on you.
usipotoshe wenzako bwana wale ni wapiga dili. kila mchungaji ana Mungu wake na kiwango cha sadaka hivi lini Mungu alidemand certain sum?
 
"Sadaka unatoa kanisani maskini anakufa mtaa/ huo ni unafki wa kidini na siyo imani kabisaa/" ..Motra the future
Mtu anaenda kutoa milioni kwa Mzee wa upako halafu njiani kampita ombaomba ambaye angeshukuru hata shilingi mia.
 
Makanisa ya leo mchungaji ndio mweka hazina, ndio katibu wa kanisa, n.k Au mama ndio msaidizi na watoto ndio wazee wa kanisa unategemea nini?? Toa wale!

Kwa makanisa yanayojielewa sadaka zina mlolongo ambao sio rahisi mtu kutumia kujinunulia Brevis au helikopta!
 
usiishi kwa kukariri ndugu yangu kwa utafiti wangu mdogo niloufanya japo mimi ni muislam wachungaji wengi wamesoma na wana ujuzi wao ama ajira nyingine tena zenye mpunga mkubwa sana zaidi ya uchungaji, wakristo hasa wa madhehebu makubwa huwa hawatoi nafasi ya uchungaji kwa akila mtu tuu kuna vigezo wana angalia ikiwemo elimu..sasa tuambie ilo kanisa unalo sali wewe nilipi...? usije ukawa uanasali kwenye kanisa la waabudu shetani harafu unatuletea utoto hapa
ila wengi ni wezi wa sadaka. hayo mamilioni ya pesa wanayatoa wapi?
 
Makanisa ya leo mchungaji ndio mweka hazina, ndio katibu wa kanisa, n.k Au mama ndio msaidizi na watoto ndio wazee wa kanisa unategemea nini?? Toa wale!

Kwa makanisa yanayojielewa sadaka zina mlolongo ambao sio rahisi mtu kutumia kujinunulia Brevis au helikopta!
haswaa uzuri ni kwanza there are people who live on the stupidity of others. let them give
 
usipotoshe wenzako bwana wale ni wapiga dili. kila mchungaji ana Mungu wake na kiwango cha sadaka hivi lini Mungu alidemand certain sum?
Hiyo certain sum ni uongo sadaka unatoa chochote ni sawa na unavyosaidia yatima unatoa chochote huko kwa certain sum sijawai sikia anadhani asipotoa ndo huyo mchungaji atakua maskini .?
 
Hiyo certain sum ni uongo sadaka unatoa chochote ni sawa na unavyosaidia yatima unatoa chochote huko kwa certain sum sijawai sikia anadhani asipotoa ndo huyo mchungaji atakua maskini .?
hata sisi hatutaki wachungaji wawe maskini ila wasitajirike kwa sadaka.
 
Hata nami niliacha kutoa baada ya kumuona mchungaji wetu kanunua canter mbili za tani mbili mbili,wakati hana Njia nyengine za kujipatia kipato cha kumuwezesha kununua magari hayo.
 
usipotoa wenzako watatoa na soon
Mchungaji wako atamiliki hammer au chopa
 
Naona uende tu huko huko Katoliki maana hakuna namna. Kumbe wewe huenda kumtolea mchungaji?? Kakae chini kwanza ujiulize maana ya sadaka yako. Ati utawapa masikini. Bwana Yesu akasema; Masikini mnao siku zote. Nadhani umeingiwa na ile roho mbaya ya Yuda Iskariote wewe.
Nimekaa nkajiuliza; Mtu huyu alikuwa anatoa kiasi gani hapo kanisani?? Kiasi kwamba uliweza kumfanya mchungaji akanunua migari hiyo ya hali yajuu kwa mkupuo!!!
Mtu weye, chunga sana usemacho kwani nadhani wewe ni wale wenye kukaa na kuhesabu waendao kumtolea Mungu wao. Pesa yako ni yako ikiwa mfukoni mwako. Ukiamua kuitoa kama sadaka maana yake ni kuwa unamtolea Mungu si mchungaji. Laiti ungeliujua maana ya wito. Watu wameacha kazi zao nzuri zenye malipo makubwa wakaja kusotea sadaka hii ya kukejeliwa na watu ka wewe!! Mungu akusaidie tu.
 
Usipotoa sadaka unategemea mchungaji akale wapi?. Wenda ana wafadhili uko nje na marafiki wanamsaidia.
 
hiii utabarikiwa '' daah sauti za wachungaji bwana '' wanatoa mpaka namba za simu ., '' sijui zamani walikuwa wanatoa anuani za nyumba zao? ili ukiwa na sadaka upeleke nyumbani? hatari
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema

Makanisa yaliyo wordwide ndo makanisa, sadaka zao zina mchanganuo mzuri na wanatoa taarifa kwa waumini ...lakini makanisa ya single pastor kila siku injili za utajirisho na uponyaji hilo changa la macho kaka...wanakukamua tu hamna lolote
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema
 
Makanisa yote ya kilokole hayatangazi mapato na matumizi. Wachungani wa Anglican, Lutheran na RC wana maisha yanayofanana na waumini wao.
 
Wewe unaenda kutoa sadaka Makanisa ya Kilokole unategemea nini..??

Makanisa yanayojielewa kama Katoliki, KKKT na Anglican ni mahala pa kutoa sadaka...Maana huko Mashule, vituo vya watoto yatima, hospitali zinajengwa..

Siku hizi wote wako sawa. Hakuna tofauti kati makanisa yanayojielewa na ya makanisa ya kilokole katika pesa. Hayo mashule, na hospital yamejengwa kwa misaada ya mashirika ya kidini kutoka nje ya nchi. Na ndio maana kila mara tunasikia migogoro katika makanisa. Tofauti iliyopo ni jinsi wanavyo ishughulikia migogoro hiyo.
 
Back
Top Bottom