Sitasoma tena gazeti la Mawio

Sitasoma tena gazeti la Mawio

Leo nilinunua gazeti la Mawio ili kupata uchambuzi kuhusiana na CHADEMA kumpokea mkuu wa mafisadi na kumfanya mgombea wa urais kwa tiketi ya UKAWA.

Lakini badala yake nimekutana na habari nyingi zinazoonesha kusifia na kutetea uamuzi wa fisadi huyo kuingia CHADEMA.

Nilikuwa naliamini gazeti hili kama nilivyokuwa naiamini CHADEMA katika mapambano dhidi ya ufisadi. Sasa kuanzia leo sitanunua wala kusoma tena gazeti hili.

Siku fisadi alipopokelewa CHADEMA nilichana kadi yangu ya uanachama na kuitumbukiza chooni! Sitaki kuwa sehemu ya uchafu unaoendelea hivi sasa ndani ya upinzani.
Nunua MZALENDO.
 
Kuhusu mambo ya EL kuingia upinzani vichwa vya kuelewa vimeshaelewa mataahira ndio yanataka eti maelezo kwanini kapokelewa! Na wala waelewa hawahitaji hayo maelezo ya kumsafisha. Aliyemsafi kwa hao CCM aongee umbea wake.

mtu aliyesoma kujitoa mhanga ni vigumu kumuelewa lowasa na chadema maana wao muda wote wataona wataonewa,peeeeples power
 
Usisome gamba ww unanuka mdomo
 
Lakini Usisahau kuwa mwenye gazeti hili ni kinara asiyeyumba katika vita vya kupinga ufisadi. Mimi siamini kuwa na yeye ana bei na amenunulika tayari. Labda hiyo makala uliyosoma ilikuwa haijahitimishwa, endelea kuisoma labda mwishoni atawakemea na kuwalaani mafisadi kama kawaida yake. Lakini Mmmh! kama na yeye kawa rafiki wa Mafisadi, basi UKAWA watakuwa wadogo kama makapi, jamani mwenzenu kusikia UKIWA! Ammah........Tanzania Oyeee!
 
mbn sawa tu ila nadhani ungesubiri uone toleo lijalo litahusu nn na hata hivyo siasa its like any other game. relux
 
Back
Top Bottom