Sitasahau!!!

Mungu ni mkuu hakuna linaloshindikana kwake. Wasamehe wote walio kukwaza kwa njia moja au nyingine kwa sababu mungu amekuinua kutoka kwenye unyonge. Kumbuka adui yako ni adui wa mungu mwachie mungu apambane nae, mungu amesema mpende adui yako, wewe wasamehe then utaona baraka za mungu zitakavyo kushukia. Mimi baba alifariki nikiwa darasa la saba nilipitia changamoto nyingi ila nilimtumaini mungu bila kuwa na kinyongo na mtu yeyote leo hii ni mtu mwenye thamani mbele ya jamii inayo ni zunguka. Nimefurahi sana ushuhuda wako, mungu anapo tubariki ni lizama tusimame na kushuhudia ili kila mwanadamu ajue mungu tunaye mwabudu ni mwema siku zote. Mungu akubariki na akupe roho ya kusamehe ili neema na baraka zake ziendeleekuwa juu yako.

Nimeshawasamehe wote!!! ila namshangaa Mungu anawaadhibu mmoja baada ya mwingine sasa!!
 
nimeona habari ingekuwa ndefu sana!! lakini nitarudi tena na Part II usijali

Namshukuru Mungu kwa ajili yenu kawafuta machozi. Toa hiyo part two ili uwape moyo ambao bado wapo kwenye tanuru la moto ili wajue Mungu husimamia wote wanaoonewa.
Nimefurahi umewasamehe kwani ndo makusudi ya Mungu ili naye apate kupewa utukufu.
Please usisahau kushare vipi ulifanikiwa ili wengi waliopo kwenye majaribu hata kama ni tofauti na wewe wajifunze uvumilivu.
 
hii ni kweli tupu, haina hata chembe ya uongo kaka tena mambo mengi tu sijayaweka humu!!! mambo ya aibu!!




Pole sana maana nilikuwa najiuliza kama mambo hayo hayakukuta,lakini najua kwa uwezo wa mungu alikulinda na mabaya yote..
 
Pole mpendwa wangu kweli bila Neno la Msamaha kujaa ndani yako huwezi kusamehe kabisa,Namshukuru Mungu aliyejaza Neno la msamaha ndani yenu kwani ndiyo mlango wa mafanikio, na kingine Mungu aendelee kuwafanya Kichwa na wala si Mkia.
Abariki kazi ya mikono yenu Kituo chenu mnachokiandaa Kibamba Mungu akitumie kuwafuta machozi yatima wengine.
 
hakika inasikitisha kusoma thread hii.ingawa wengi wetu tumekuwa tukisikia tu,pole sana kwa yaliyokukuta hali ulikuwa na umri mdogo,....lakini inakuwa vigumu kulistop hili tatizo lipo ktk ngazi ya familia.....maybe tulijadili as a special topic ili tupate views za watu i think itasaidia kupunguza tatizo.lkn on the other hand,inasababishwa na umaskini ktk ngazi ya familia,kama wanafamilia wana kila kitu ni vigumu kwao kunyang'anya mali za ndugu zao waliofariki.....
 
Hamna anaesema wote!Hao hawawakilishi kundi zima la wanawake.





Lizzy,katika misamiati iliyomo kichwani kwangu kila nikijaribu kuitizama huwa nakosa msamiati wa LAWAMA,kwa maana hiyo basi katika maisha yangu sina kumbukumbu kama nimewahi kumlaumu mtu na wala sitegemei kumlaumu mtu yeyote kwa kuwa kwangu mimi lawama huwa naiona kama ni ishara ya kushindwa,lakini kutokana na ujumbe alioutoa dada yetu Susy napenda kusema kuwa wasomaji wanaopita hapa wenye tabia kama hiyo wajifunze na wabadilike kwani nina uhakika wa 100% kuwa wamo humu wenye tabia kama hizo na wala tusikatae maana ndio walivyo watu wengi hasa wale ambao hawana shughuli za kufanya zaidi ya kukaanga na kuchemsha. Nadhani mpaka hapo bado sijamlaumu mtu.
 
  • Thanks
Reactions: LD
susy stori yako inatia huzuni sana binadamu sisi ni wabaya sana nashindwa hata cha kuongeza.
 
Binadamu huwa wanasahau kwamba aliyemdogo leo kesho atakuwa mtu mzima na ataweza kujihudumia mwenyewe, ubinafsi na umaskini ni chanzo cha dhuluma kwa watoto yatima na wajane, lakini pia shida hizo huwa zinajenga immunity hakuna litakalokubabaisha ukubwani. pole sana

Kama kuna kitu nilijifunza kutoka kwa mzazi wangu ni kuwaheshimu sana watoto/vijana wadogo. Watu wengi wasio na ufahamu huwadharau sana watoto na kudhania hawatakua au hata wakikua watawasaidia/watawafanyia nini.Kitu tunachosahau ni kuwa hata sisi kipindi fulani na siyo kirefu sana tulikuwa watoto - tukakua na kufikia hapa tulipo! Iweje uone huyu mtoto yatima hatakuwa na kuwa MTU?
Huwa naangalia watu ambao walikuwa watu wenye nafasi zao na sasa si lolote basi hapo najiskia mdogo sana na kuwa humble tu mbele ya MUNGU wangu na kuzidi kuomba neema ya kuwatendea vizuri walio wadogo kwangu kwa kila hali.Huko tunakoelekea hakuna mwenye uhakika tutakuwaje.Tutapanda au kushuka ajuaye ni Mungu tu.Tuwatendee vizuri watoto maana wao ndio watakuja kutukumbuka.Wazungu wana msemo wao - be nice to your children because they will be the ones to choose your old people's home! Kwa mazingira yetu, hata kama una pesa na mali, utakuja kuhitaji hawa watoto wakusaidie hata kukumiminia maji kwenye glasi unywe - hata kama maji, glas na friji ni vyako!
 
MESTOD

usijali, nimekuelewa tupo pamoja nitaandika sehemu nyingine Mungu akitupatia uzima!!
 
:amen:
Pole mpendwa wangu kweli bila Neno la Msamaha kujaa ndani yako huwezi kusamehe kabisa,Namshukuru Mungu aliyejaza Neno la msamaha ndani yenu kwani ndiyo mlango wa mafanikio, na kingine Mungu aendelee kuwafanya Kichwa na wala si Mkia.
Abariki kazi ya mikono yenu Kituo chenu mnachokiandaa Kibamba Mungu akitumie kuwafuta machozi yatima wengine.
 
Pole sana Suzy siku zote tunaishi katika yeye atutiaye nguvu, pia maandiko yanaongeza msaada wetu unatoka wapi? Msaada wetu u katika BWANA ASISINZIAYE ATULINDAYE, pia majaribu ni sehemu ya maisha mtazame AYUBU. Naamini katika yeye atutiaye nguvu Umeshinda. Ntaendelea kuclose my finger tips to pray for you my love.
 
Pole sana Suzy siku zote tunaishi katika yeye atutiaye nguvu, pia maandiko yanaongeza msaada wetu unatoka wapi? Msaada wetu u katika BWANA ASISINZIAYE ATULINDAYE, pia majaribu ni sehemu ya maisha mtazame AYUBU. Naamini katika yeye atutiaye nguvu Umeshinda. Ntaendelea kuclose my finger tips to pray for you my love.

Dia nilitaka kushangaa leo sijakuona kabisa, Da Dena ndio kalia mpk kakimbia kabisa!! Nashukuru sana, maombi yako ni ya muhimu sana katika maisha yangu!!!
 
Dia nilitaka kushangaa leo sijakuona kabisa, Da Dena ndio kalia mpk kakimbia kabisa!! Nashukuru sana, maombi yako ni ya muhimu sana katika maisha yangu!!!

Nipo dear wangu yaani Suzy nimelia na keyboard mpaka basi. Zaburi ya 121 iendelee kukuongoza. Our living GOD HASHINDWI.
 
Suzy pole kwa kupitia yote hayo mamii..Mungu azidi kukutangulia katika maisha yako uzidi kufanikiwa!!
 
Back
Top Bottom