Sitasahau!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitasahau!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Susy, Mar 24, 2011.

 1. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asalam aleikum!!!

  Bwana Yesu asifiwe!!

  Nimesoma thread ya Lizy kuhusu unyanyasaji wa watoto ikanikumbusha mbali sana, hakika imenitoa machozi!!

  Nakumbuka miaka ya nyuma sana wakati nikiwa na miaka 4 tu, mama yangu alifariki kwa ugonjwa wa cancer, hatukukaa hata mwaka baba naye alifariki na ugonjwa wa figo, hapo ndipo nilipotamani dunia igeuke chini juu.

  Nakumbuka dada yangu mkubwa alikuwa ndio kwanza yupo 4m3 na kaka yangu ambaye nafatana naye alikua yupo darasa la pili, tulinyang'anywa mali zote za baba yetu, tena tukarudishwa kijijini kabisa ambapo baba aliweka mifugo yake, baada ya muda bb mdg akaja akachukua ngombe wote wakagawana na watoto wa mama mkubwa.

  Hakuna aliyetujali, tuliachiwa mbuzi tu pale kijijini, nakumbuka kaka yangu ilibidi aache shule aanze kuchunga hao mbuzi kwa taabu, mimi nilikua nachota maji na kufagia, hakuna aliyejua tunakula nini, tunavaa nini wala tunalala vipi. Dada yangu alichukuliwa na dada mtoto wa mm mkubwa na kugeuzwa house girl.

  Nakumbuka wale rafikize baba walipoona hivyo, wakamlipia dada yangu ada tena kwa kuchangiwa na kijiji dada akarudi shule, jirani yetu mmoja akasema tuchanganye mbuzi zetu na zake ili kaka asiende kuchunga tena awe anaenda shule.

  kutokana na baridi ya mkoa ambao tulikuwepo, na hatukuwa na blanket siku moja nilishikwa na naimonia ikiambatana na homa kali, yule bb mkubwa rafikiye baba akamtuma kaka yangu aende kwa ba-mdogo akamweleze, kaka yangu akapanda gari kwenda mjini kumwambia baba mdogo, baba mdogo akamwambia kama baba yake na mama yake wamekufa yeye anafaida gani, mwache afe akupunguzieni taabu!! kaka alirudi kijijini na kuomba msaada kwa yule rafiki yake na baba (ba-mkubwa) ndipo nikapelekwa hospitali na kulazwa, ikimlazimu kufanya vibarua vya kulima wakati akiwa mdogo ili kutupatia fedha za matumizi na kuniuguza.

  kaka yangu mtoto wa m.mkubwa akaoa kule kijijini akatuchukua lakini niliona bora tulivyokuwa tunakaa wenyewe maana wifi alitunyanyasa sana, jina langu lilibadilika ghafla, nikawa naitwa mbwa, nakumbuka alikua ananiita hivi, "we mbwa mkubwa njoo hapa" ukifika tu unakutana na kibao kizito alafu ndio maagizo mengine yanafuatia!!!

  Baada ya muda, wale wote waliotudhulumu alikufa mmoja baada ya mwingine, wale waliotunyanyasa kwa chakula leo ndio wanatuomba chakula, waliotulaza chini leo wanatembea wameinamisha vichwa vyao!!

  "usimnyanyase yatima wala kumuonea mjane, mkono wa Mungu utakuwa juu yako"
   
 2. LD

  LD JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mungu ni baba wa Yatima na ni Mume wa wajane. Poleni sana Suzy. Ila namshukuru Mungu kwa sababu fadhili zake zilikuwa pamoja nanyi. Ndio maana amewaandalia meza machoni pa watesi wenu.

  Songa mbele, na pia kumbuka Mungu aliwapitisha hapo ili mje kuwa msaada kwa Yatima na watu wengine wanaoteseka. Msiache kabisa kufanya utumishi huo.
  UBARIKIWE
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Glory be to God
   
 4. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Daah
  Pole sana mpenzi


  Lakini mpenzi umepitia mengi
  MShukuru Mungu kwa yote
  Na walokutendea hayo yote wasamehe
  Na mwachie Mungu..
  jipongeze kwa hatua uliyofikia

  Girl
  Your so brave to share your story
  Thanx my dear..
   
 5. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  LD namshukuru Mungu kwa sasa tunajenga kituo cha watoto yatima kule kibamba!! hatuwezi kusahau!!
   
 6. w

  wazo mbadala Member

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu yu Mwema
   
 7. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  niliapa kuwa sitawasamehe hasa yule wifi yangu, ila leo Mungu amenifundisha kusamehe!!! nawapenda sana! najua dhahabu safi lazima ipite kwenye moto!!
   
 8. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Pole sana dearest.Haya mambo yanatokea sana kwenye jamii zetu lakini siku zote Mungu huwasimamia wenye machungu na wanaoonewa.
  I believe kupitia experience hiyo mbaya utakuwa umejifunza jinsi ya kuishi na kuwatreat yatima na hivyo uwe mfano wa kuigwa na wengine.
  Ubarikiwe.
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Pole sana Suzy kwa mkasa uliokupata, wengi tumepitia mkasa kama wako na hatupendi kukumbushwa yale ya nyuma kuepusha kutonesha vidonda vilivyopona!
   
 10. sweetdada

  sweetdada JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 540
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hadi machozi.Pole sana sasa Susy.

  Kila kitu hutokea kwa sababu fulani duniani.
  Wanasema malipo ni hapa duniani,ndo yaliyowakuta hao ndugu zenu.

  Jitahidi usahau yaliyopita na ugange yajayo. Mungu yu pamoja nanyi nyote.
   
 11. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hongereni sana na Mungu aendelee kuwabariki
   
 12. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Ameeen!!
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Pole sana mpendwa!Ila yote yale yanabaki kua historia na somo kwako... kwahiyo mshukuru Mungu maana amekutoa huko!Sijui roho mbaya zitatuisha lini wanadamu sie kwakweli!
   
 14. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kuna andiko linasema shuhudia tuone kama unampenda Mungu, lazima niwaeleze nilipotoka na nilipo sasa ni kwa mkono wa Mungu tu!!
   
 15. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Lizy hapa ndipo ninajiuliza kwani kipindi kile chote Mungu alikuwa wapi?? lakini leo nakuja kujua jambo tu, ya kwamba hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea!! na Mungu huinua maadui kwa sababu maalum!!
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wanasema muombee adui yako ili ashuhudie pale utakapobarikiwa!
   
 17. Susy

  Susy JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 1,450
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nilishasahau dia, Lizzy ndio kanikumbusha.
   
 18. M

  Marytina JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Pole sana
  pls yote niweweka kwenye PM
   
 19. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kwa maelezo yako Suzy inaonekana ulipitia ktk hali ngumu ya maisha, lakini bado hujaeleza ilikuwaje ukafanikiwa kutokea.
  Kwa ufupi tena tupe picha inaweza kusaidia watu wengine wenye hali mbaya ili wasikate tamaa!!!!!!!! Ubarikiwe!!


   
 20. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Hicho kikombe cha chai unakunywaga mwenyewe tuu??????? Ubarikiwe!!!!!!
   
Loading...