Sitasahau!!!

Pole sana Susy,

Hii ndo dunia tunayoishi, it has different tests in different circumstances.

Si wakati wote mambo yanakwenda vizuri, kuna milima, mabonde na pia tambarare.
Thank God umepitia uzoefu mkubwa na umejifunza mengi n' i hope hutamfanyia mtu mwingine hivyo
 
Pole sana Susy kwa yote uliyopitia. Umefanya vizuri kutolipa kisasi, maana Bwana ametuagiza tusilipe kisasi kwani Yeye atalipa kwa kipimo sahihi. Ndicho kilichotokea kwa hao wabaya wako. Hatuna lingine la kumrudishia Mungu bali ni Sifa na Utukufu.
Tunamshukuru Mungu wetu aliye hai aliyekuvusha hadi kufikia hapo ulipo. Mungu akubariki katika ujenzi wa kituo cha yatima. Baraka zake zisikupungukie daima.
 
Suzy Umeniliza ,asante yesu upo mpaka leo na mungu anendelea kuanza maisha yako na family kwa ujumla ,
amin mungu ni mwema na mapito yote tunayopitia ni jambo la kushukuru
 
Susy baba mtu mzima nimelia mpaka basi,yaani uuuwwwwiiii .Pamoja na machungu haya tujifunze kitu kimoja,KUANDIKA WOSIA.Hii ni muhimu sana sana na kama unaona ndugu zako hawaeleweki katika wosia unaweza kumtaja mtu unayemwamini asimamie na kulinda mali zako hadi watoto wa come of age. Wengi tunapuuzia hili,tunaona ni uchuro ,lakini katika mazingira ya Sussy na nduguze ingewasaidia sana.Tafakari ndugu mwana MMU.
 
Susy baba mtu mzima nimelia mpaka basi,yaani uuuwwwwiiii .Pamoja na machungu haya tujifunze kitu kimoja,KUANDIKA WOSIA.Hii ni muhimu sana sana na kama unaona ndugu zako hawaeleweki katika wosia unaweza kumtaja mtu unayemwamini asimamie na kulinda mali zako hadi watoto wa come of age. Wengi tunapuuzia hili,tunaona ni uchuro ,lakini katika mazingira ya Sussy na nduguze ingewasaidia sana.Tafakari ndugu mwana MMU.

bishanga mbona baba yangu alisema yote!! Tena hata msiba wa mama hakuhudhuria alikuwa amelazwa akaaelekeza tu mzikeni sehemu fulani, naona baba aliona kifo chake akamwambia ba mdogo atutunze, atusomeshe, hasa mie niliyekuwa kiziwanda chake, baba alikuwa anakata roho anasema wanangu nawaacha, wanangu nawaacha!!! kumbe ba mdogo analake kichwani!!
 
Nimeshawasamehe wote!!! ila namshangaa Mungu anawaadhibu mmoja baada ya mwingine sasa!![/QUOTE]

MUNGU anajuwa zaidi kuliko sisi. Kuna makosa ya siri, adhabu yake huwa siri, Mungu huyawacha haya mpaka siku ya hesabu. Makosa ya dhahiri na yaliyovuka mipaka Mungu huanza hapa hapa ili kuwaweka wao kama mifano kwa wengine.
 
bishanga mbona baba yangu alisema yote!! Tena hata msiba wa mama hakuhudhuria alikuwa amelazwa akaaelekeza tu mzikeni sehemu fulani, naona baba aliona kifo chake akamwambia ba mdogo atutunze, atusomeshe, hasa mie niliyekuwa kiziwanda chake, baba alikuwa anakata roho anasema wanangu nawaacha, wanangu nawaacha!!! kumbe ba mdogo analake kichwani!!
i can understand Susy lakini kuandika na ku attest properly ni muhimu,mimi naomba lifestory yako liwe fundisho kwetu sisi sote.Again nakupa pole sana,be strong,be forgiving.
 
Wakumwitu

Naufahamu vizuri huo wimbo, natena juzi kaka alikuja kwangu akaniambia dada kwenye harusi yako wimbo huo lazima tutaupiga!! ili wajue kuwa tunawaombea, nilibaki kucheka tu!
noted, single
 
Asalam aleikum!!!

Bwana Yesu asifiwe!!

Nimesoma thread ya Lizy kuhusu unyanyasaji wa watoto ikanikumbusha mbali sana, hakika imenitoa machozi!!

Nakumbuka miaka ya nyuma sana wakati nikiwa na miaka 4 tu, mama yangu alifariki kwa ugonjwa wa cancer, hatukukaa hata mwaka baba naye alifariki na ugonjwa wa figo, hapo ndipo nilipotamani dunia igeuke chini juu.

Nakumbuka dada yangu mkubwa alikuwa ndio kwanza yupo 4m3 na kaka yangu ambaye nafatana naye alikua yupo darasa la pili, tulinyang'anywa mali zote za baba yetu, tena tukarudishwa kijijini kabisa ambapo baba aliweka mifugo yake, baada ya muda bb mdg akaja akachukua ngombe wote wakagawana na watoto wa mama mkubwa.

Hakuna aliyetujali, tuliachiwa mbuzi tu pale kijijini, nakumbuka kaka yangu ilibidi aache shule aanze kuchunga hao mbuzi kwa taabu, mimi nilikua nachota maji na kufagia, hakuna aliyejua tunakula nini, tunavaa nini wala tunalala vipi. Dada yangu alichukuliwa na dada mtoto wa mm mkubwa na kugeuzwa house girl.

Nakumbuka wale rafikize baba walipoona hivyo, wakamlipia dada yangu ada tena kwa kuchangiwa na kijiji dada akarudi shule, jirani yetu mmoja akasema tuchanganye mbuzi zetu na zake ili kaka asiende kuchunga tena awe anaenda shule.

kutokana na baridi ya mkoa ambao tulikuwepo, na hatukuwa na blanket siku moja nilishikwa na naimonia ikiambatana na homa kali, yule bb mkubwa rafikiye baba akamtuma kaka yangu aende kwa ba-mdogo akamweleze, kaka yangu akapanda gari kwenda mjini kumwambia baba mdogo, baba mdogo akamwambia kama baba yake na mama yake wamekufa yeye anafaida gani, mwache afe akupunguzieni taabu!! kaka alirudi kijijini na kuomba msaada kwa yule rafiki yake na baba (ba-mkubwa) ndipo nikapelekwa hospitali na kulazwa, ikimlazimu kufanya vibarua vya kulima wakati akiwa mdogo ili kutupatia fedha za matumizi na kuniuguza.

kaka yangu mtoto wa m.mkubwa akaoa kule kijijini akatuchukua lakini niliona bora tulivyokuwa tunakaa wenyewe maana wifi alitunyanyasa sana, jina langu lilibadilika ghafla, nikawa naitwa mbwa, nakumbuka alikua ananiita hivi, "we mbwa mkubwa njoo hapa" ukifika tu unakutana na kibao kizito alafu ndio maagizo mengine yanafuatia!!!

Baada ya muda, wale wote waliotudhulumu alikufa mmoja baada ya mwingine, wale waliotunyanyasa kwa chakula leo ndio wanatuomba chakula, waliotulaza chini leo wanatembea wameinamisha vichwa vyao!!

"usimnyanyase yatima wala kumuonea mjane, mkono wa Mungu utakuwa juu yako"

"The love God is greater far than tong of men can ever tell,it goes beyond the highest stars and goes below the deepest hell""
Remember " Mungu hawezi kuruhusu majaribu ambayo Neema yake haiwezi kukufunika""
 
"The love God is greater far than tong of men can ever tell,it goes beyond the highest stars and goes below the deepest hell""
Remember " Mungu hawezi kuruhusu majaribu ambayo Neema yake haiwezi kukufunika""
Kweli kabisa bwana ahimidiwe
 
Pole sana Susy, mshukuru Mungu kwa kuwanusuru na majaribu yote hayo.

Usilipize wema kwa ubaya, ukiona ndugu zako waliokutesa wanahitaji msaada ambao uko ndani ya uwezo wako, usisite kuwasaidia.

Thawabu yako utaipata mbinguni

Najua ni ngumu lakini jaribu.
 
habari hii imenihuzunisha sana nilitamani mwishoni ningeambiwa ni hadithi tu, Pole binti maisha ni safari ndefu
 
Oooh! Suzy jamani....!
Pole mpenzi. Mmmh! Mi nikileta ushuhuda wangu hapa nahisi hata kuuandika sitomaliza.
Ila tukumbuke katika kila jambo la shari lina heri ndani yake.
Hatuna budi kumshukuru mungu na kwa changamoto tunazopitia maana ndizo zinazotufanya tuwe imara katika maisha.
Pole susy.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom