Sitasahau siku niliyonusurika kutolewa sadaka

Hivi mtu akikupa kitabu, ukamtungie maswali ni sheria ipi ya nchi unakuwa umevunja?
Mbona mnapenda kujitengenezea hofu/ makosa ambayo hayapo.
kama point ni kutokumuamini mtu yupo sahihi japo scenario aliyoitumia sio sahihi.
Kuna vitu vidogovidogo unaweza kuvichukulia simple lakini athari yake ni kubwa sana.
Unajua jamaa alikuwa ameongea nini na watu aliokuwa nao?
Atakayejua maswali umetunga tu ni nani kama sio yeye na jamaa tu?
Tunapaswa kuwa makini wakati wote ili kuepusha baadhi ya kadhia.
 
Onesha ugunduzi wako wa kuwa nipo form six. Wapi nimeandika nipo form six.
Mimi nilichogundua humu wengi fuata mkumbo uwezo wa kuhoji mdogo sana wewe ukiwa mmoja wapo. Unabisha kitu usichokijua nambie uwongo upo wapi.
Omba Mungu usije kuingia kwenye radar za hawa jamaa hata siku moja utanyenyekewa kama mfalme utabembelezwa kama mtoto mdogo ila ukiingia kwenye tundu tu ndio utaelewa juwa thread hii ni ya uwongo na ulishtuka paragraph ya pili.
Ha ha ha ha ha ha
Ndugu Angalia hata mwandiko wako tu unaweza kujiweka elimu ipi?
Iwe ukweli iwe uongo ni juu yako mwenyewe
pathetic
 
Ha ha ha ha ha ha
Ndugu Angalia hata mwandiko wako tu unaweza kujiweka elimu ipi?
Iwe ukweli iwe uongo ni juu yako mwenyewe
pathetic
Sasa kama ntajua mwenyewe ni kiherehere gani kimekutuma kucomment hapa. Threads zingine hukuziona?
Utaendelea kuwa na akili za kushikiwa mpaka lini, ukajifanya unajua kumsoma mtu kwa kuangalia mwandiko ukahisi nipo form six! Pumbavu Kabisa
 
Mbona unapata shida sana kaka pilipili isiyokuwasha?
tulia tuli tu hakuna wa kukusumbua, usipate shida hivyo ukabamiza simu yako chini,
usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake ila wewe naona unaendelea kunijibu tuu.
 
Yani jf kwa vile mtu wa kwanza kasema ni chai basi wote mnaunga tela😂😂😂
Mbona mi nimeelewa tu,,. Una bahati kaka ingawa Hiyo mbinu yao ya kijinga

Umeamua kumpa faraja jamaa, ila kuna vitu vingi havi-addup.

  1. Shule ni ya boarding, watu wanaenda kula bwaloni. Lakini hapo hapo kuna cafeteria, kama iko nje ya shule au ndani hajaelezea, ila kama ingekuwa nje ya shule kusingekuwa na haja ya kurudi nyuma ya mabweni, biashara ingeisha huko huko.
  2. 2005 mwanafunzi wa secondary kumiliki simu, you must be special.
  3. Prep za secondary ziko library? Nachojua library za secondary usiku zinafungwa, chuoni ndiko tunaweza kupata muda wa kusomea library usiku (atleast by 2005 sidhani kama shule za secondary zilikuwa na library kwa ajili ya prep).
  4. Baada ya kumweleza Suma, Suma moja kwa moja alimwambia hao ni watu wa usalama, alijuaje?
  5. Mteja wa kununua mtihani kaja naye kutafuta huo mtihani, reasoning rahisi tu, hivi mnunuaji wa mtihani unazunguka naye aone utakaponunua?
  6. Tukio linaanza saa 12 jioni, Giza linaanza, unaenda library, then unatoka, unaenda cafeteria, unatoka halafu usiku huo unampata mwalimu kumwelezea tukio, baada ya muda unaenda kukaa sehemu unawaona wale watu wakiwa ndo wanaondoka, huyo mwalimu alikuwa wapi? Imekuchukua muda gani kumpata kiasi kwamba bado jamaa walikuwa bado wapo?
 
Nimeisoma mpaka mwisho lakini hapa sijakuelewa.
hivyo naomba uniandalie maswali matano makali ya uchumi then unipe nitakupa laki mbili ili ionekane tumetoa mtihani hapa" (Ikumbukwe kipindi hicho mtihani wa kidato cha sita wa taifa ndio ilikuwa inakaribia ilikuwa imebaki wiki moja tu.
Fafanua hapo Mimi mwenyewe mwanafuzi ila sijakuelewa.
Kwa tekniki hii sio kweli, mtihani kuvuja hakukamatwi kwa staili hiyo, huyo jamaa alikua ana nia ya kumshushia jumba bovu tu, au stori ya kutunga
 
Umeamua kumpa faraja jamaa, ila kuna vitu vingi havi-addup.

  1. Shule ni ya boarding, watu wanaenda kula bwaloni. Lakini hapo hapo kuna cafeteria, kama iko nje ya shule au ndani hajaelezea, ila kama ingekuwa nje ya shule kusingekuwa na haja ya kurudi nyuma ya mabweni, biashara ingeisha huko huko.
  2. 2005 mwanafunzi wa secondary kumiliki simu, you must be special.
  3. Prep za secondary ziko library? Nachojua library za secondary usiku zinafungwa, chuoni ndiko tunaweza kupata muda wa kusomea library usiku (atleast by 2005 sidhani kama shule za secondary zilikuwa na library kwa ajili ya prep).
  4. Baada ya kumweleza Suma, Suma moja kwa moja alimwambia hao ni watu wa usalama, alijuaje?
  5. Mteja wa kununua mtihani kaja naye kutafuta huo mtihani, reasoning rahisi tu, hivi mnunuaji wa mtihani unazunguka naye aone utakaponunua?
  6. Tukio linaanza saa 12 jioni, Giza linaanza, unaenda library, then unatoka, unaenda cafeteria, unatoka halafu usiku huo unampata mwalimu kumwelezea tukio, baada ya muda unaenda kukaa sehemu unawaona wale watu wakiwa ndo wanaondoka, huyo mwalimu alikuwa wapi? Imekuchukua muda gani kumpata kiasi kwamba bado jamaa walikuwa bado wapo?
Stori ya kutunga, Riwaya Maridhawa hizi
 
Nitajie mkuu maana kuja hadi bwenini hapo naingiwa na wasi wasi kiufupi hii story sio yako na umeambiwa na mtu aliesomea diploma kama sikosei ya ualimu kule ndio usalama huwepo hususan kipindi cha mitihani
shule mojawapo ambayo haiitaji nguvu kuingia ni moshi technical nimesoma mm hapo ...wapita njia wanakatiza hapo shuleni muda wote so sio kila shule ina uzio
 
Umeamua kumpa faraja jamaa, ila kuna vitu vingi havi-addup.

  1. Shule ni ya boarding, watu wanaenda kula bwaloni. Lakini hapo hapo kuna cafeteria, kama iko nje ya shule au ndani hajaelezea, ila kama ingekuwa nje ya shule kusingekuwa na haja ya kurudi nyuma ya mabweni, biashara ingeisha huko huko.
  2. 2005 mwanafunzi wa secondary kumiliki simu, you must be special.
  3. Prep za secondary ziko library? Nachojua library za secondary usiku zinafungwa, chuoni ndiko tunaweza kupata muda wa kusomea library usiku (atleast by 2005 sidhani kama shule za secondary zilikuwa na library kwa ajili ya prep).
  4. Baada ya kumweleza Suma, Suma moja kwa moja alimwambia hao ni watu wa usalama, alijuaje?
  5. Mteja wa kununua mtihani kaja naye kutafuta huo mtihani, reasoning rahisi tu, hivi mnunuaji wa mtihani unazunguka naye aone utakaponunua?
  6. Tukio linaanza saa 12 jioni, Giza linaanza, unaenda library, then unatoka, unaenda cafeteria, unatoka halafu usiku huo unampata mwalimu kumwelezea tukio, baada ya muda unaenda kukaa sehemu unawaona wale watu wakiwa ndo wanaondoka, huyo mwalimu alikuwa wapi? Imekuchukua muda gani kumpata kiasi kwamba bado jamaa walikuwa bado wapo?
Inawezekana tangia alivokua shule akivoelewa ndo mpka Leo hajareason zaidi, inawezekana hawakutaka mtihani walimtaka yeye,,, na kuwa na simu 2005 mi nilikua form five Huo mwaka na tulikua na simu na walimua walikua wanajua ,,yani inaruhusiwa ,,na ambao hawakua na simu walikua wachache sana
 
Kwa haraka haraka mimi story naipa 30% kuwa kweli, kuna vitu vingi vya kutolea ufafanuzi.

BTW, siyo mbaya, katoa funzo.
 
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya ijumaa nikitafakari namna ya kupata pesa ya matumizi pale shuleni nilipokuwa nasoma maana "pocket money"ilikuwa ishakata.
Ilikuwa ni shule ya boarding maarufu na inafanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya taifa. Ilipofika saa kumi na mbili jioni kengele ya msosi ilikuwa inapigwa na wanafunzi kuanza kusogea bwaloni ili kupata chakula cha jioni.
Sasa wakati natoka bwenini kwenda bwaloni nikakutana na mwanafunzi mwenzangu akiwa ameongozana na jamaa nisiyemfaham na waliponifikia yule mwanafunzi mwenzagu akaniambia "kuna mgeni wako" na akamgeukia yule mgeni na kumwambia "fdizzle mwenyewe huyu hapa"
Yule mgeni akanichangamkia sana huku mimi nikiwa simjui na akniambia ana shida anaomba tuongee vizuri hivyo twende cafeteria amabayo ipo karibu na shule tukaongee vizuri.
Sasa wakati tunaenda ndipo akaanzisha mazungumzo huku tunatemebea akaniambia hivi; "Unajua bwana fdizzle kiukweli mimi sikujui ila nilipofika hapa maeneo ya shule nikajaribu kumsimamisha yule jamaa nikamtajia jina kwa kumung'unya maneno yule mwanfunzi mwenzako akauliza unamtaka fdizzle nami nikajibu ndio, na ndio maana akanleta kwako"
Binafsi mpaka kufikia hapo nkawa bado sijapata jibu ikumbukwe tupo njiani kwenda cafeteria na giza lishaanza kuingia. Kwa mbele yetu kidgogo kukawa na dada mmoja hivi mimi kwa macho yangu nikliona ni kimsichana fulani hivi.
Yule jamaa akaendelea kusema "Dhumuni kuu la kukutafuta wewe ni kwamaba kuna dili nataka tufanye, ntakupa laki mbili"
Dah kusikia laki mbili moyo ukalipuka ikumbukwe hiyo ni miaka ya 2005 hivi laki mbili ni pesa ndefu kwa mwanafunzi enzi hizo na ukizingatia hapo nilikuwa nawaza ntapata wapi ela sasa imejileta yenyewe Mungu kasikia maombi yangu. Ngoja nisiskilize hilo dili sasa.
Dili lenyewe sasa
Yule jamma huku tukiwa tunatemebea na kwa mbali yule dada akionekana akaniambia "umemuona yule dada?"(huku akinyoosha kidole kuelekea alipo yule dada. Nikamjibu "ndio"
Akaendelea "sasa yule dada ni mwanafunzi wangu namfundisha tutiion sasa anataka mtihani hivyo nimeshampanga vizuri tu na kila kitu kimmenda sawa hatua ya mwisho iliyobaki ni kama kumfanya kuwa huo mtihani tumeutolea hapa, hivyo naomba uniandalie maswali matano makali ya uchumi then unipe nitakupa laki mbili ili ionekane tumetoa mtihani hapa" (Ikumbukwe kipindi hicho mtihani wa kidato cha sita wa taifa ndio ilikuwa inakaribia ilikuwa imebaki wiki moja tu)
Moyo ulilipuka kwa woga na wasiwasi nikamwambia jamaa siwezi kuifanya hiyo kazi jamaa aknisisitizia sana mpaka anatia huruma maneno kibao nimsaidie niandike vyovyote navyoweza ili mradi tu ionekane katoa hapo maswali (hapo tulikuwa tushafika cafeteria tayari).
Nikaendelea kumkatalia ila bado alinisistiza sana na sana nikawa nataka kuondoka pale cafe teria akanitolea kitabu cha "cost accounting" akanipa niende nacho huku akinisisitiza nikamuandalie maswali matano ya uchumi nimletee.
Tukatoka pale cafeteria akiendelea kunisisitizia mbele nikamuona tena yule dada, cha ajabu akawa anaftemebea kama kutukwepa tusiwe karibu nae.
Yule jamaa akaendelea kunisisitizia ataniongezea pesa mradi niandae tu hayo maswali huku akinisisitizia tukutane nyuma ya mabweni ya shule ambapo kuna vichaka kidogo na giza giza.
Huku moyo ukiwa mzito na pia nikitamani ela sikumjibu kitu nikaenda zangu maktaba nikawaza na kuwazua "mkosi gani huu, sina ela halafu zinakuja dili za kuvunja sheria".
Yule jamaa alinipa namba zake za simu pamoja na kile kitabu cha cost accounting ili nikiwa tayari basi nimpigie tukutane huko nyuma ya mabweni anipe el animpe maswali.
Katika kutafakari kwangu nikiwa libarary huku wenzangu wakiendelea kujisomea nikkazimia kurudisha kitabu na kuachana na ma,bo haya kwani ni kinyume cha sheria za nchi.
Sasa wakat natoka maktaba nikakutana na rafiki yangu suma(sio jina halisi) akaniuliza mbona upo hivyo kulikoni?
Nikanueleza mkasa wote A to Z yule rafiki yangu akaniambia hao ni watu wa usalama sasa fanya hivi we tangulia mimi nipo nyuma nachunguza pia. Nikanjibu poa nikamtext jamaa tukutane cafe kisha nikaanza kwenda huku suma akija kwa mbali akisoma mchezo.
Nikafika mpaka cafe nikaingia na mara yule mtu akafika nae pia, tukakaa na kuanza mazungumzo mara na suma akafika nae akakaa kwa mbali akiendelea kuchunguza pia.
Nikaendelea kumkatalia na kumrudishia kitabu chake huku jamaa akiendelea kunisisitizia mwishoni akaniambia eti "twende kule nyuma ya mabweni tuzungumze vizuri" nikakmakatalia na kumwambia aachane na mimi.
Nikatoka zangu hapo huku akinisisitiza twende tukazungumze kule nyuma ya mabwen nikamkatalia. Baada ya kutoka nikarud class nikakaa kusubiri ripot ya suma.
Suma alipokuja akaniambia "fdizzle ulikuwa upo katika mtego, yule mdada uliemwona sio mdada ni mmama tu mtu mzima na kule cafeteria wakati unazungumza nae wapoo wengine walikuwa wanafuatilia na kukuchukua picha na walikuwa zaid ya watano, kwa ufupi ulikuwa kwenye mtego"
Baada ya kuambiwa hivyo nikachukua hatua ya kwenda kutoa taarifa kwa mwalimu wa zamu nae nikamueleza A to Z mwalimu akanipa hongera kwa kukwepa huo mtego na aknieleza matokeo amabyo ningekutana nayo endapo ningeandika hayo maswali.
Baada ya kutoka kwa mwalimu nilikosa hamu ya kusona hivyo kuns sehem nikaenda kukaa. Na hiyo sehem ni barabara inayotoka huko nyuma ya mabwen kuelekea sehem mbalimbali.
SIkuamini macho yangu nilipomuona yule jamaa aliekuw ananilzaimisha kuandaa maswali wakitokea huko nyuma ya mabweni wakiwa wapo kama watano pamoja na yule mwanamke na askari wawili waliovalia sare wakiwa na bunduki kabisa.
Nilipata wakati mgumu sana nikiwaza mtu yupo tayari kukuharibia future yako ili mradi tu yeye apande cheo. Na pia niliona tamaa ukiziendekeza mabaya utaishia pabaya sana. Na la mwisho niliona jamaa mbinu zao sio kwa kuwa kama ni lengo kutafuta kama kuna uvujifu wa mitihani kwa ile mbinu si sahihi kabisa.
Ni heri wangepandikiza hata mwanafunzi ili kujua kama kuna uvujifu wa mitihani kuliko mbinu ya kumlazimisha mtu aandike maswali kisha kuyatumia hayo kama kielelezo cha kuw akuna uvujifu wa mitihani.
Nimeamua kushare nanyi ili baadhi ya mabo tuwe tunajiongeza wenyewe tusiendekeze tamaa
Niwatakie Paska Njema!
Hadithi nzuri ila sio ya kweli....
Mwandiko wako tu unaonesha hujasoma while za magari ya njano....boarding ya wapi wanaruhusu watoto kuongea na watuvwasiowajua...tofauti na walezi?

"God is Great"
 
Back
Top Bottom