Sitasahau siku niliyonusurika kutolewa sadaka

Mbinu zao sio mkuu na Lengo lao kuonesha wamekamata mwanafunzi akiuza mtihani
Dah!!mkuu ningekuwa ni mimi,basi wangenikamata zamani sana..

Wangenipa advance,then baada ya kazi wamalize pesa.
 
Kila napokumbuka lile tukio namchukia sana yule jamaa alikuwa anataka kumipotezea maisha hivi hivi
Dah!!mkuu ningekuwa ni mimi,basi wangenikamata zamani sana..

Wangenipa advance,then baada ya kazi wamalize pesa.
 
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya ijumaa nikitafakari namna ya kupata pesa ya matumizi pale shuleni nilipokuwa nasoma maana "pocket money"ilikuwa ishakata.
Ilikuwa ni shule ya boarding maarufu na inafanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya taifa. Ilipofika saa kumi na mbili jioni kengele ya msosi ilikuwa inapigwa na wanafunzi kuanza kusogea bwaloni ili kupata chakula cha jioni.
Sasa wakati natoka bwenini kwenda bwaloni nikakutana na mwanafunzi mwenzangu akiwa ameongozana na jamaa nisiyemfaham na waliponifikia yule mwanafunzi mwenzagu akaniambia "kuna mgeni wako" na akamgeukia yule mgeni na kumwambia "fdizzle mwenyewe huyu hapa"
Yule mgeni akanichangamkia sana huku mimi nikiwa simjui na akniambia ana shida anaomba tuongee vizuri hivyo twende cafeteria amabayo ipo karibu na shule tukaongee vizuri.
Sasa wakati tunaenda ndipo akaanzisha mazungumzo huku tunatemebea akaniambia hivi; "Unajua bwana fdizzle kiukweli mimi sikujui ila nilipofika hapa maeneo ya chuo nikajaribu kumsimamisha yule jamaa nikamtajia jina kwa kumung'unya maneno yule mwanfunzi mwenzako akauliza unamtaka fdizzle nami nikajibu ndio, na ndio maana akanleta kwako"
Binafsi mpaka kufikia hapo nkawa bado sijapata jibu ikumbukwe tupo njiani kwenda cafeteria na giza lishaanza kuingia. Kwa mbele yetu kidgogo kukawa na dada mmoja hivi mimi kwa macho yangu nikliona ni kimsichana fulani hivi.
Yule jamaa akaendelea kusema "Dhumuni kuu la kukutafuta wewe ni kwamaba kuna dili nataka tufanye, ntakupa laki mbili"
Dah kusikia laki mbili moyo ukalipuka ikumbukwe hiyo ni miaka ya 2005 hivi laki mbili ni pesa ndefu kwa mwanafunzi enzi hizo na ukizingatia hapo nilikuwa nawaza ntapata wapi ela sasa imejileta yenyewe Mungu kasikia maombi yangu. Ngoja nisiskilize hilo dili sasa.
Dili lenyewe sasa
Yule jamma huku tukiwa tunatemebea na kwa mbali yule dada akionekana akaniambia "umemuona yule dada?"(huku akinyoosha kidole kuelekea alipo yule dada. Nikamjibu "ndio"
Akaendelea "sasa yule dada ni mwanafunzi wangu namfundisha tutiion sasa anataka mtihani hivyo nimeshampanga vizuri tu na kila kitu kimmenda sawa hatua ya mwisho iliyobaki ni kama kumfanya kuwa huo mtihani tumeutolea hapa, hivyo naomba uniandalie maswali matano makali ya uchumi then unipe nitakupa laki mbili ili ionekane tumetoa mtihani hapa" (Ikumbukwe kipindi hicho mtihani wa kidato cha sita wa taifa ndio ilikuwa inakaribia ilikuwa imebaki wiki moja tu)
Moyo ulilipuka kwa woga na wasiwasi nikamwambia jamaa siwezi kuifanya hiyo kazi jamaa aknisisitizia sana mpaka anatia huruma maneno kibao nimsaidie niandike vyovyote navyoweza ili mradi tu ionekane katoa hapo maswali (hapo tulikuwa tushafika cafeteria tayari).
Nikaendelea kumkatalia ila bado alinisistiza sana na sana nikawa nataka kuondoka pale cafe teria akanitolea kitabu cha "cost accounting" akanipa niende nacho huku akinisisitiza nikamuandalie maswali matano ya uchumi nimletee.
Tukatoka pale cafeteria akiendelea kunisisitizia mbele nikamuona tena yule dada, cha ajabu akawa anaftemebea kama kutukwepa tusiwe karibu nae.
Yule jamaa akaendelea kunisisitizia ataniongezea pesa mradi niandae tu hayo maswali huku akinisisitizia tukutane nyuma ya mabweni ya shule ambapo kuna vichaka kidogo na giza giza.
Huku moyo ukiwa mzito na pia nikitamani ela sikumjibu kitu nikaenda zangu maktaba nikawaza na kuwazua "mkosi gani huu, sina ela halafu zinakuja dili za kuvunja sheria".
Yule jamaa alinipa namba zake za simu pamoja na kile kitabu cha cost accounting ili nikiwa tayari basi nimpigie tukutane huko nyuma ya mabweni anipe el animpe maswali.
Katika kutafakari kwangu nikiwa libarary huku wenzangu wakiendelea kujisomea nikkazimia kurudisha kitabu na kuachana na ma,bo haya kwani ni kinyume cha sheria za nchi.
Sasa wakat natoka maktaba nikakutana na rafiki yangu suma(sio jina halisi) akaniuliza mbona upo hivyo kulikoni?
Nikanueleza mkasa wote A to Z yule rafiki yangu akaniambia hao ni watu wa usalama sasa fanya hivi we tangulia mimi nipo nyuma nachunguza pia. Nikanjibu poa nikamtext jamaa tukutane cafe kisha nikaanza kwenda huku suma akija kwa mbali akisoma mchezo.
Nikafika mpaka cafe nikaingia na mara yule mtu akafika nae pia, tukakaa na kuanza mazungumzo mara na suma akafika nae akakaa kwa mbali akiendelea kuchunguza pia.
Nikaendelea kumkatalia na kumrudishia kitabu chake huku jamaa akiendelea kunisisitizia mwishoni akaniambia eti "twende kule nyuma ya mabweni tuzungumze vizuri" nikakmakatalia na kumwambia aachane na mimi.
Nikatoka zangu hapo huku akinisisitiza twende tukazungumze kule nyuma ya mabwen nikamkatalia. Baada ya kutoka nikarud class nikakaa kusubiri ripot ya suma.
Suma alipokuja akaniambia "fdizzle ulikuwa upo katika mtego, yule mdada uliemwona sio mdada ni mmama tu mtu mzima na kule cafeteria wakati unazungumza nae wapoo wengine walikuwa wanafuatilia na kukuchukua picha na walikuwa zaid ya watano, kwa ufupi ulikuwa kwenye mtego"
Baada ya kuambiwa hivyo nikachukua hatua ya kwenda kutoa taarifa kwa mwalimu wa zamu nae nikamueleza A to Z mwalimu akanipa hongera kwa kukwepa huo mtego na aknieleza matokeo amabyo ningekutana nayo endapo ningeandika hayo maswali.
Baada ya kutoka kwa mwalimu nilikosa hamu ya kusona hivyo kuns sehem nikaenda kukaa. Na hiyo sehem ni barabara inayotoka huko nyuma ya mabwen kuelekea sehem mbalimbali.
SIkuamini macho yangu nilipomuona yule jamaa aliekuw ananilzaimisha kuandaa maswali wakitokea huko nyuma ya mabweni wakiwa wapo kama watano pamoja na yule mwanamke na askari wawili waliovalia sare wakiwa na bunduki kabisa.
Nilipata wakati mgumu sana nikiwaza mtu yupo tayari kukuharibia future yako ili mradi tu yeye apande cheo. Na pia niliona tamaa ukiziendekeza mabaya utaishia pabaya sana. Na la mwisho niliona jamaa mbinu zao sio kwa kuwa kama ni lengo kutafuta kama kuna uvujifu wa mitihani kwa ile mbinu si sahihi kabisa.
Ni heri wangepandikiza hata mwanafunzi ili kujua kama kuna uvujifu wa mitihani kuliko mbinu ya kumlazimisha mtu aandike maswali kisha kuyatumia hayo kama kielelezo cha kuw akuna uvujifu wa mitihani.
Nimeamua kushare nanyi ili baadhi ya mabo tuwe tunajiongeza wenyewe tusiendekeze tamaa
Niwatakie Paska Njema!


Duuuuh!siredi ofu ze dey
 
Mbona haueleweki.
Sasa wewe kumtungia mtu maswali ya economics inahusiana vipi na uvujishaji wa mitihani hapo shule?
Au wewe ndie mtunzi wa mitihani ya Necta ?
 
Kipindi hicho wanafunzi wa kidato cha sita walikuwa wamebakisha wiki moja ili waanze mtihani wa taifa kwa ufupi jamaa alitaka niandike maswali as if ni Yale yatakayokuwa ktk mtihani wa taifa halafu anilipe laki mbili kwa mujibu wa yeye
Na endapo ningeandika wangetumia hiyo Kama ushahid shule ingefungiwa nami ningefungwa pia
Haya maelezo ni dhaifu sana. Bado haya justify wewe kukamatwa
 
Sio jazba kuna watu akili Hakuna kabisa hivi umesoma post haina ukweli si unaacha tu kusoma unafuata vitu vya ukweli unacomment ili iweje na ukizingatia Hakuna sehem uliyolazimishwa kusoma na kucomment
Mbona unatoa mapovu badala ya kujibu hoja za wasomaji.
 
Watu mnamshambulia mtoa mada bure badala ya kuangalia content ya habari, binafsi nimepata points,usimwamini strange person, kuvunja sheria sehemu yoyote itakucost baadae Kama mtoa mada alivyosema aliogopa kuvunja Sheria pia ni muhimu kuwakataza watoto wenu kuongea na strange people
 
Watu mnamshambulia mtoa mada bure badala ya kuangalia content ya habari, binafsi nimepata points,usimwamini strange person, kuvunja sheria sehemu yoyote itakucost baadae Kama mtoa mada alivyosema aliogopa kuvunja Sheria pia ni muhimu kuwakataza watoto wenu kuongea na strange people
Hivi mtu akikupa kitabu, ukamtungie maswali ni sheria ipi ya nchi unakuwa umevunja?
Mbona mnapenda kujitengenezea hofu/ makosa ambayo hayapo.
kama point ni kutokumuamini mtu yupo sahihi japo scenario aliyoitumia sio sahihi.
 
Mbona haueleweki.
Sasa wewe kumtungia mtu maswali ya economics inahusiana vipi na uvujishaji wa mitihani hapo shule?
Au wewe ndie mtunzi wa mitihani ya Necta ?
Ngoja nkuambie kitu
Una kichwa kigumu sana na kuna mdau mmoja hapo juu amesema wengi wenu mna Psychology Mob na mwingine akachangia kuwa mnaboa.
Uwezo mdogo wa kufikiri hamsomi mkaelewa mnakurupuka tu.
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom