Sitasahau siku niliyonusurika kutolewa sadaka

Haya maelezo ni dhaifu sana. Bado haya justify wewe kukamatwa
tatizo wengi ni wajuaji mnapokuwa nyuma ya keyboard
Unasema hayajustify mimi kukamatwa nimeandika kuwa walishaweka mtego kule ili nikifika wanidake na kupelekwa kituoni mambo mengine baadae.
Na kingine fahamu kuwa kama ningethubutu kwenda huko nyuma ya mabweni ningekuwa pia nimevunja sheria za shule kwa kuwa hairuhusiwi kuwa huko muda ule;.
Halafu unaandika kirahisi rahisi tu
 
Mbona unatoa mapovu badala ya kujibu hoja za wasomaji.
Nioneshe hoja mojawapo katika hao waliouliza nikujibu.
Wapo waliouliza kistaarabu nimejibu kistaarabu ukiukliza kishenzi nakujibu kishenzi pia
Au kwa upande wako mtu akisema "uongo" "chumvi" nayo ni hoja?
 
Hivi mtu akikupa kitabu, ukamtungie maswali ni sheria ipi ya nchi unakuwa umevunja?
Mbona mnapenda kujitengenezea hofu/ makosa ambayo hayapo.
kama point ni kutokumuamini mtu yupo sahihi japo scenario aliyoitumia sio sahihi.
Kile kitabu akihusiani na kazi aliyonipa yeye ya kutunga maswali. Kitabu alinipa kama uthibitisho kuwa yeye ni mwalimu na anafundisha ndio maana an hicho kitabu cha cost accounting
Na mimi kwa kujiongeza kile kitabu nahisi kilikuwa na recorded device au walichukua finger prints ambapo endapo ningeandaa hayo maswali basi hivyo vitu vingetumika kama ushahid mahakamani.
Labda nikuulize swali; Hivi wale wanodakwa na TAKUKURU unadhani wakifika mahakamani ushahidi gani unatumika kuwatia hatiani?Au unadhani ukisema aliniomba rushwa basi ndio ushahidi huo wa kumtia mtu hatiani?Ni lazima kuwa na ushahidi wa kutosha ikiwemo hayo mabo ya vitabu.
 
Jamaa ni muongo wa kutupwa, mara shule mara chuo mara bwaloni mara duu
 
Ukweli Toka moyoni msitari wa kwanza kabisa ulitosha kunijurisha yakuwa habari ya uongo
nilipo fika paragraf ya pili nikaacha kusoma
maana jamaa yupo boarding wanaenda bwaloni kula tena anaenda karibu na cafeteria iliyokaribu na shule(Hii bweni kwao)
tena wakati huohuo yupo chuo
napitia comment nagundua tena yupo form six
Duuuuu
 
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya ijumaa nikitafakari namna ya kupata pesa ya matumizi pale shuleni nilipokuwa nasoma maana "pocket money"ilikuwa ishakata.
Ilikuwa ni shule ya boarding maarufu na inafanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya taifa. Ilipofika saa kumi na mbili jioni kengele ya msosi ilikuwa inapigwa na wanafunzi kuanza kusogea bwaloni ili kupata chakula cha jioni.
Sasa wakati natoka bwenini kwenda bwaloni nikakutana na mwanafunzi mwenzangu akiwa ameongozana na jamaa nisiyemfaham na waliponifikia yule mwanafunzi mwenzagu akaniambia "kuna mgeni wako" na akamgeukia yule mgeni na kumwambia "fdizzle mwenyewe huyu hapa"
Yule mgeni akanichangamkia sana huku mimi nikiwa simjui na akniambia ana shida anaomba tuongee vizuri hivyo twende cafeteria amabayo ipo karibu na shule tukaongee vizuri.
Sasa wakati tunaenda ndipo akaanzisha mazungumzo huku tunatemebea akaniambia hivi; "Unajua bwana fdizzle kiukweli mimi sikujui ila nilipofika hapa maeneo ya chuo nikajaribu kumsimamisha yule jamaa nikamtajia jina kwa kumung'unya maneno yule mwanfunzi mwenzako akauliza unamtaka fdizzle nami nikajibu ndio, na ndio maana akanleta kwako"
Binafsi mpaka kufikia hapo nkawa bado sijapata jibu ikumbukwe tupo njiani kwenda cafeteria na giza lishaanza kuingia. Kwa mbele yetu kidgogo kukawa na dada mmoja hivi mimi kwa macho yangu nikliona ni kimsichana fulani hivi.
Yule jamaa akaendelea kusema "Dhumuni kuu la kukutafuta wewe ni kwamaba kuna dili nataka tufanye, ntakupa laki mbili"
Dah kusikia laki mbili moyo ukalipuka ikumbukwe hiyo ni miaka ya 2005 hivi laki mbili ni pesa ndefu kwa mwanafunzi enzi hizo na ukizingatia hapo nilikuwa nawaza ntapata wapi ela sasa imejileta yenyewe Mungu kasikia maombi yangu. Ngoja nisiskilize hilo dili sasa.
Dili lenyewe sasa
Yule jamma huku tukiwa tunatemebea na kwa mbali yule dada akionekana akaniambia "umemuona yule dada?"(huku akinyoosha kidole kuelekea alipo yule dada. Nikamjibu "ndio"
Akaendelea "sasa yule dada ni mwanafunzi wangu namfundisha tutiion sasa anataka mtihani hivyo nimeshampanga vizuri tu na kila kitu kimmenda sawa hatua ya mwisho iliyobaki ni kama kumfanya kuwa huo mtihani tumeutolea hapa, hivyo naomba uniandalie maswali matano makali ya uchumi then unipe nitakupa laki mbili ili ionekane tumetoa mtihani hapa" (Ikumbukwe kipindi hicho mtihani wa kidato cha sita wa taifa ndio ilikuwa inakaribia ilikuwa imebaki wiki moja tu)
Moyo ulilipuka kwa woga na wasiwasi nikamwambia jamaa siwezi kuifanya hiyo kazi jamaa aknisisitizia sana mpaka anatia huruma maneno kibao nimsaidie niandike vyovyote navyoweza ili mradi tu ionekane katoa hapo maswali (hapo tulikuwa tushafika cafeteria tayari).
Nikaendelea kumkatalia ila bado alinisistiza sana na sana nikawa nataka kuondoka pale cafe teria akanitolea kitabu cha "cost accounting" akanipa niende nacho huku akinisisitiza nikamuandalie maswali matano ya uchumi nimletee.
Tukatoka pale cafeteria akiendelea kunisisitizia mbele nikamuona tena yule dada, cha ajabu akawa anaftemebea kama kutukwepa tusiwe karibu nae.
Yule jamaa akaendelea kunisisitizia ataniongezea pesa mradi niandae tu hayo maswali huku akinisisitizia tukutane nyuma ya mabweni ya shule ambapo kuna vichaka kidogo na giza giza.
Huku moyo ukiwa mzito na pia nikitamani ela sikumjibu kitu nikaenda zangu maktaba nikawaza na kuwazua "mkosi gani huu, sina ela halafu zinakuja dili za kuvunja sheria".
Yule jamaa alinipa namba zake za simu pamoja na kile kitabu cha cost accounting ili nikiwa tayari basi nimpigie tukutane huko nyuma ya mabweni anipe el animpe maswali.
Katika kutafakari kwangu nikiwa libarary huku wenzangu wakiendelea kujisomea nikkazimia kurudisha kitabu na kuachana na ma,bo haya kwani ni kinyume cha sheria za nchi.
Sasa wakat natoka maktaba nikakutana na rafiki yangu suma(sio jina halisi) akaniuliza mbona upo hivyo kulikoni?
Nikanueleza mkasa wote A to Z yule rafiki yangu akaniambia hao ni watu wa usalama sasa fanya hivi we tangulia mimi nipo nyuma nachunguza pia. Nikanjibu poa nikamtext jamaa tukutane cafe kisha nikaanza kwenda huku suma akija kwa mbali akisoma mchezo.
Nikafika mpaka cafe nikaingia na mara yule mtu akafika nae pia, tukakaa na kuanza mazungumzo mara na suma akafika nae akakaa kwa mbali akiendelea kuchunguza pia.
Nikaendelea kumkatalia na kumrudishia kitabu chake huku jamaa akiendelea kunisisitizia mwishoni akaniambia eti "twende kule nyuma ya mabweni tuzungumze vizuri" nikakmakatalia na kumwambia aachane na mimi.
Nikatoka zangu hapo huku akinisisitiza twende tukazungumze kule nyuma ya mabwen nikamkatalia. Baada ya kutoka nikarud class nikakaa kusubiri ripot ya suma.
Suma alipokuja akaniambia "fdizzle ulikuwa upo katika mtego, yule mdada uliemwona sio mdada ni mmama tu mtu mzima na kule cafeteria wakati unazungumza nae wapoo wengine walikuwa wanafuatilia na kukuchukua picha na walikuwa zaid ya watano, kwa ufupi ulikuwa kwenye mtego"
Baada ya kuambiwa hivyo nikachukua hatua ya kwenda kutoa taarifa kwa mwalimu wa zamu nae nikamueleza A to Z mwalimu akanipa hongera kwa kukwepa huo mtego na aknieleza matokeo amabyo ningekutana nayo endapo ningeandika hayo maswali.
Baada ya kutoka kwa mwalimu nilikosa hamu ya kusona hivyo kuns sehem nikaenda kukaa. Na hiyo sehem ni barabara inayotoka huko nyuma ya mabwen kuelekea sehem mbalimbali.
SIkuamini macho yangu nilipomuona yule jamaa aliekuw ananilzaimisha kuandaa maswali wakitokea huko nyuma ya mabweni wakiwa wapo kama watano pamoja na yule mwanamke na askari wawili waliovalia sare wakiwa na bunduki kabisa.
Nilipata wakati mgumu sana nikiwaza mtu yupo tayari kukuharibia future yako ili mradi tu yeye apande cheo. Na pia niliona tamaa ukiziendekeza mabaya utaishia pabaya sana. Na la mwisho niliona jamaa mbinu zao sio kwa kuwa kama ni lengo kutafuta kama kuna uvujifu wa mitihani kwa ile mbinu si sahihi kabisa.
Ni heri wangepandikiza hata mwanafunzi ili kujua kama kuna uvujifu wa mitihani kuliko mbinu ya kumlazimisha mtu aandike maswali kisha kuyatumia hayo kama kielelezo cha kuw akuna uvujifu wa mitihani.
Nimeamua kushare nanyi ili baadhi ya mabo tuwe tunajiongeza wenyewe tusiendekeze tamaa
Niwatakie Paska Njema!
Shukrani sana mkuu
 
Kwa kuhitimisha
Humu watu wengi mnaleta dharau kwa vile hayajawakuta ila zipo mbinu nyingi zinazoweza kutumika kuwadaka.
Na kingine kitu kama hukijui na hujawahi kukutana nacho ni kheri ukakaa kimya tu kuliko kujifanya unajua kila kitu kumbe mweupe tu kichwani.
Na kwa kuongezea usiombe uingie kwenye radar za hao jamaa ni Mungu tu akiamua kukuponya ila huwezi kujua kama upo kwenye radar za hawa jamaa mpaka siku ukijikuta upo nyuma ya nondo ndio utaelewa nini maana ya hii threads.
Hujalazimishwa kuamini hivyo unaweza kuchukua kama funzo au ukaachana nalo kabisa, bando lako simu yako hakuna wa kukupangia nawe usipangie wenzako
Jamaa ni muongo wa kutupwa, mara shule mara chuo mara bwaloni mara duu
Kichwa kigumu utaelewa vipi
Labda nikuambie tu hapo kwenye chuo ni kosa la kiuandishi tu na sipo hapa kulazimisha kueleweka sawa?kama hujaelewa pita kushoto
 
Kwa kuhitimisha
Humu watu wengi mnaleta dharau kwa vile hayajawakuta ila zipo mbinu nyingi zinazoweza kutumika kuwadaka.
Na kingine kitu kama hukijui na hujawahi kukutana nacho ni kheri ukakaa kimya tu kuliko kujifanya unajua kila kitu kumbe mweupe tu kichwani.
Na kwa kuongezea usiombe uingie kwenye radar za hao jamaa ni Mungu tu akiamua kukuponya ila huwezi kujua kama upo kwenye radar za hawa jamaa mpaka siku ukijikuta upo nyuma ya nondo ndio utaelewa nini maana ya hii threads.
Hujalazimishwa kuamini hivyo unaweza kuchukua kama funzo au ukaachana nalo kabisa, bando lako simu yako hakuna wa kukupangia nawe usipangie wenzako
Jamaa ni muongo wa kutupwa, mara shule mara chuo mara bwaloni mara duu
Kichwa kigumu utaelewa vipi
Labda nikuambie tu hapo kwenye chuo ni kosa la kiuandishi tu na sipo hapa kulazimisha kueleweka sawa?kama hujaelewa pita kushoto
 
Ukweli Toka moyoni msitari wa kwanza kabisa ulitosha kunijurisha yakuwa habari ya uongo
nilipo fika paragraf ya pili nikaacha kusoma
maana jamaa yupo boarding wanaenda bwaloni kula tena anaenda karibu na cafeteria iliyokaribu na shule(Hii bweni kwao)
tena wakati huohuo yupo chuo
napitia comment nagundua tena yupo form six
Duuuuu
Onesha ugunduzi wako wa kuwa nipo form six. Wapi nimeandika nipo form six.
Mimi nilichogundua humu wengi fuata mkumbo uwezo wa kuhoji mdogo sana wewe ukiwa mmoja wapo. Unabisha kitu usichokijua nambie uwongo upo wapi.
Omba Mungu usije kuingia kwenye radar za hawa jamaa hata siku moja utanyenyekewa kama mfalme utabembelezwa kama mtoto mdogo ila ukiingia kwenye tundu tu ndio utaelewa juwa thread hii ni ya uwongo na ulishtuka paragraph ya pili.
 
Nimeisadiki hii story. Wewe utaendelea kua juu naamini ukitoboa na uko juu.
 
Huo ndio ukweli wako kutwa kutazama porn
Hahahahahah
 
Back
Top Bottom