Sitasahau siku nilipoingia matatizoni na mamlaka ya kiserikali bila kutarajia

Shikamooni wakubwa ! Wadogo shauri zenu. Ni muda sasa umepita tangu tukio hili litokee ila nimeamua kuwasimulia mkasa huu vizuri ili iwe funzo kwa wengine, na si mkasa huu tu bali nimeamua kila nitakapopata nafasi nitakua nawasimulia mikasa yangu niliyopitia.

Nakumbuka kuna siku niliwahi kuanzisha thread yenye kichwa cha habari ' NIFANYE KIJAKAZI WAKO SIKU YA KESHO' sina kumbu kumbu kama nimeandika sahihi ila wale wataalam mtanisaidia walau kuiunga ile link ya uzi ule na hiki kisa nitakachowasimulia leo.
Nakumbuka ndani ya ule uzi niliomba mtu yeyote aliekua na kazi yeyote aniite nije nimsaidie kuifanya buuure bila hata malipo ya namna yeyote ( hata nauli ya kwenda huko ningejilipia mwenyewe) ila watu wote waliogopa na wengine wakasema kama kutoa msaada nikatoe kwa watoto yatima, ila niliwajibu kuwa kwa sababu nimeamua kuufanya msaada wangu katika namna hii ni bora waupokee tu kuliko kunishauri kitu ambacho tayari nilishakiwaza kabla, kuna mdau mmoja(sitamtaja) ndio tuliwasiliana pm tukakubaliana ila lengo halikutimia. Nisiwachoshe sana twende kwenye mada halafu nyie mtaunganisha wenyewe mkasa ule na kisha cha mie kuomba kuwa kijakazi wa mtu kwa siku moja tu.

Siku yangu ilianza vizuri na kawaida kama siku nyingine, nakumbuka nilitakiwa nisafiri kesho yake kutoka mkoa nilipokua niende mkoa mwingine lakini sijui nini kiliniwasha, narudia tena kiliniwasha nikaamua kubadili mawazo na kusafiri siku hiyo hiyo, kwa kuwa muda ulikua umeenda sana (ilikua usiku) nisingeweza kupata basi hivyo nikaamua kuvizia gari yoyote ndogo.
Na kweli katika pilika pilika nikafanikiwa kupana NOAH ya jamaa mmoja ambae alikua peke ake kwenye gari hivyo bila kizuizi alikubali tuondoke wote nikapanda safari ikaanza.
Tulitembea safari yetu vizuri japo ile gari baada ya kuipanda niligundua ilikua imechoka sana tu, nakumbuka jamaa alijisifu yeye ni mzoefu wa ile njia maana hupita mara kwa mara. Usiku ulizidi kuwa mnene na sie bila hili wala lile tuliendelea kuchanja mbuga.
Katika safari za usiku kama kawaida ni lazima utakua check points za hapa na pale, basi tulizipita kama tatu lakini moja baada ya kusimamishwa kimbembe ndio kilianza.
Askari alietusimamisha aliuliza tulikua wangapi kwenye gari tukamjibu idadi yetu ni wawili, akawasha tochi akatumulika kweli akaridhika ula akaomba afunguliwe mlango wa nyuma kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha zaidi, hapo nikaona dereva kama ni mwenye wasi wasi akawasha taa za ndani fasta akamwambia afande aangalie tu lakini afande akasema yeye anataka kukagua kule nyuma kabisa anaomba afunguliwe, yule dereva akawa kama yupo njia panda, yule afande akaendelea kukomaa, ikabidi dereva atoe lock ila hakushuka, basi yule kamanda baada ya kufungua mlango alianza kukagua kwa makini sana( nahisi kuna mtu alimpa ramani) mara kidogo nikasikia afande samahani hebu njoo mara moja, kuna afande alikua pembeni kidogo akainuka na kwenda kule nyuma, wakati huo dereva alishazima gari kisha akawa ameufungua mlango kidooogo.
Baada tu ya yule afande kufika kule nyuma huku dereva alikurupuka kwa kasi ya ajabu akatokomea gizani, ndani ya gari nikawa nimebaki peke yangu na mie katika hali ya kupaniki nikajikuta nafungua mlango kwa kasi ya umeme nikimbie, lengo la kufungua mlango lilitimia na nikawa mguu nje, ile namalizia kutoka tu nikasikia kitu kizito kimenipiga kisogoni kisha nikajigonga kwenya mlango kisha nikaanguka chini kama gunia kisha baada ya hapo ikawa ni mvua ya mateke na makofi mpaka mwili wote ukafa ganzi.

Baada ya kile kipigo nilikula pingu kisha nikawekwa pembeni yao( walikua wanne) ubaya ile pingu nilifungwa vibaya kwa sababu upande mmoja ilifunga mkono na upande mwingine ikawa imefunga mguu kwa hiyo nikawa nimelazwa ubavu huku damu zikichuruzika mdomoni na kisogoni.

Baada ya hapo ndo nikaanza kusikia stori zao wakizungumza kumbe ile gari imebeba mrungi wa kutosha na bangi hapo ndo ukisikia jumba bovuuuu ndo hapo, niliwaza sana ni kwa namna gani kile kikombe kitaweza kuniepuka?
Hivi ni nani nitamwambia mie niliomba lift tu kwenye hiyo gari akanielewa?
Hivi ni mahakama gani nikipelekwa maskini mimi nitaweza kujitetea mpaka wakose hatia?
Hivi nitamshawishi nani na kwa kiasi gani mpaka anielewe ule mrungi sio mali yangu?

Baada ya kuwaza sana nikaona hakuna namna yeyote ya kuweza kukiepuka kifungo zaidi ya kukimbia, lakini nitaweza vipi kukimbia ikiwa nina pingu?ukweli ni kwamba haiwezekeni, sasa kama hqiwezekani nitafanya nini? Maana kilichokua kinasubiriwa ni difenda ije kunibeba nipelekwe kituoni.

Hapa niliwaza kitu kimoja, nifanye kisa chochote mpaka pingu ije kufunguliwa
Basi nikaanza kukoroma huku najitupatupa( kumbuka hapo nimelazwa ubavu halafu nimepinda kama samaki fulani huuzwa masokoni ambao hukunjwa mpaka mdomo unakutana na mkia)
Katika kujirusha kule kwa kuwa nilikua navuja damu mdomoni pia nilijaza damu nyingi sana mdomoni ili zitumike kama silaha ya kivita(usicheke)
Baada ya kukoroma sana na kujigeuza huku na kule kuna afande akawasha tochi akanimulika, mie hapo nikaona yes tayari wameanza kuingia king, nikawa nageuza macho juu, aliposimama kuja nikaanza kuimwaga ile damu taratiiiiibu kutoka mdomoni basi akaingiwa na hofu akachukua funguo akaja kufungua pingu kisha akanivuta mpaka pembeni kidogo kisha akawaambia wenzake huyu jamaa anaweza kutufia hapa anageuza macho naona na damu imemtoka sana(mie hapo naongeza juhudi huku akili ikiwaza next step) pigieni jamaa wawahi kuja.
Baada ya kuniweka pale pembeni akaja na maji akawa akamwagia( ndo mara ya kwanza toka nizaliwe kuoga maji ya kilimanjaro maana nililowa kila sehemu)

Baadaya tukio la maji nikaona sana nitulie ili nijipange vizuri ki medani za kivita, kusema ukweli sikua nikisikia maumivu hata kidogo yaani kwa kifupi nilikua poa kabisa yaani hata kama angetokea simba mitaa ile nadhani mie ningekimbia kuliko wao.

Unajua unapotana kufanya tukio ni lazima uwe na mawazo ni namna gani utalitekeleza bila kukuletea shida.
Kwa ukubwa wa tukio lile nilikua na wasiwasi sana juu ya maisha yangu ya baadae hivyo nikaja na mpango wa kutoroka katika namna mbili.

1/ Niwateke wale maafande kisha nichukue silaha zao nizipakie kwenye ile gari kisha niondoke nayo mpaka mbele sana kisha niitelekeze nitokomee zangu.

2/Nisubiri wajisahau nikurupuke kwa kasi ya umeme nitokomee polrini?
............. ntamalizia muda si mrefu.

Mwendelezo....................

Njia ya kwanza ingeweza kunipeleka kwenye matatizo makubwa zaidi, vipi kamq wangenishoot? Baada ya kuwaza sana nikaona ni bora niachane na wazo lq kwanza maana lilikua ni hatari sana kwangu

Wazo la pili nalo lilihitaji namna ya kujipanga na sio kukurupuka tu, katika muda ule ilibidi nipime ni kwa namna gani naweza kukimbia na hata wakisema wanikimbize wasinikamate? Baada ya kuchunguza sana nikagundua gari inapofika hapo mmoja ndie mwenye jukumu la kwenda kukagua gari halafu wawili watasimama mbele ili kuruhusu gari ipite, na mmoja anabaki pale pembeni na mimi.
Baada ya kuona kila kitu kipo sawa ilipokuja gari ile wameenda kuikagua mie nikakurupuka mbio sana na kutokomea gizani. Nilichosikia nyuma ni sauti ya yule tuliebaki nae akisema anatorokaaaa, wakajaribu kunifukuza lakini hawakufua dafu.
Nilikimbia kwa spidi bila kuchoka hata pale nilipohisi hakuna dalili za mtu kunifuata niliendelea kukimbia huku ninapoenda sipajui.
Nilikimbia mpaka nikachokanikaanza kutembea
Nilipochoka kutembea kwa haraka nikaanza kutembea pole pole
Nilipochoka nikasimama na hatimae nikakaa kabisaaaa
Hapo nilipokaa ndio nikagundua kuna limti lilinichoma mguuni na damu inatoka.
Baada ya kuvuta pumzi nikaendelea na safari huku sijui naenda wapi, nilienda sana nikachoka tena ikanibidi nikae tu,
Kulipoanza kupambazuka kuna dogo nilikutana nae akanisaidia sana wakaenda wakanipaka mafuta ya taa kwenye vidonda, sikujua kama ni dawa lakini nilichohitaji ni msaada.

Nilipelekwa mpaka njia kuu tena kwa msaada wa baiskeli, kama unavyojua mbwa hafi akiuona ufuko hatimae nilifanikiwa kufika nilipokua naenda,
Nililia sana baada ya kufanikiwa kufika salama na kujiguza mpaka kupona, nikajisemea mwenyewe ni lazima nifanye kitu maana vipi kama ningeendelea kushikiliwa pale? Je kesho yangu ingekuaje?

Baada ya kupona nilifanya vitu vifuatavyo

Cha kwanza nilinunua chipsi yai kama sahani nane, halafu nikachukua nguo zangu ambazo sikua nikizivaa mara kwa mara na pia nikachagua nguo mbili ninazozipenda nikapeleka pale Morocco mataa karibu na Airtel nikawapa wadogo zetu na ndugu zetu waliokua pale wakishinda wanaomba kwenye magari. Walifurahi sana hawakua wakielewa elewa hasa nini kilinisukuma.

Cha pili nilikua namsaidia yeyote alienifuata na kusema ana shida, hasa kama shida hiyo itakua ndani ya uwezo wangu.
Nakumbuka kuna siku nilikua Sinza kuna madogo wawili wakaniomba niwaelekeze ni wapi wataweza kupata gari ya kwenda mbezi, kwa lengo zuri tu niliwaelekeza na kuwaambia itabidi wapande gari mbili mpaka kwenda huko, nilichokuja kugundua hawakua na nauli, baada ya kupiga nao stori kidogo nikagundua pia ni shida tu inayowapeleka huko,
Nilichofanya niliwapa kiasi fulani cha hela ikawasaidie huko mbele, ninachokumbuka mmoja alianza kulia pale pale, hakuamini kama kweli mtu baki anaweza kukupa hela yote ile, hakikua kiasi kikubwa sana ila hakikua kiasi kidogo pia.

Cha tatu nikaamua kujitolea kufanya kazi ya mtu yeyote bila ujira hata senti, nikaanzisha ule uzi lakini kwa bahati mbaya wazo halikufanikiwa, lakini kwa kweli bado naendelea sana kujitoa kwa watu wenye uhitaji ulio ndani ya uwezo wangu.

Aksanteni
Na pia mnisamehe kwa kukatisha uzi.
Nilifanya hivyo kwa kuwa simu yangu tayari ilikua imeishiwa chaji sasa wasiwasi wangu ukawa unaweza ikazima halafu kazi yoooote niliyoifanya ku type ikawa imepotea. Nikaona bora niukatishe then nikifika mahala kwenye power niumalizie.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Pole sana,, ila pia umenifurahisha ulipo sema ndo mara yako ya kwanza kuogea maji ya kilimanjaro
 
Mimi nakumbuka siku nilipompiga mdada kwa kunizushia masuala Fulani kumbe sikujua alikuwa awala wa marine force , Sasa akaenda kunishtaki kambini kwa huyo jamaa yake daah! Si muda nimesiti geto napika ugali wangu nasikia ghafla! Ndio huyu hapa huyo mdada akiwaonyesha hao masoja watatu aliokuja nao duuuh! Nilihisi akili imeyeyuka ila nikajua mi kidume kudadeki ndani ya sekunde zero zero nipata plan B ya ajabu na hapo kumbuka napanga hayo ndani ya ubongo ikiwa bado nimekaa na jamaa wanaekekea kunikamata alafu kumbuka wakibugi maanake walinifuata geto . Kiukweli mpaka Leo sikuamini kama Mimi Kama naweza kuwana na ujasiri huo apo pembeni kulikuwa na mawe makubwa mawili ya kushikiza mlango pale ufungukiwapo siunajua nilikuwa nimeketi kwenye ngazi ghafla nilivurumisha jiwe la kwanza kama kuwatishia Hilo jiwe sikuwalenga ila nilirusha kuelekea walipo nikaligonganisha na ukuta wa jirani yangu kwa Kasi isiyo ya kawaida wale jamaa wakawa na hofu kidogo wakasambatika uku wakiinama nadhani walihisi Mimi sio simple Kama walivyo dhani maana walikuja na pingu tu . Mara ya Tena kikarusha jiwe la pili huku na mimi nikitafuta upenyo wa kutoroka Lile jiwe jiwe kiukweli hata Mimi nilijawa na uwogo mno maana nilimlega mjeda kwenye paji la uso Mimi niliona jamaa anaanguka ghafla damu zikichomoka kichwani hapo nakaribia geti la nje tiyari kwa kutoroka akabaki mjeda mmoja mbabe tukifukuzana tiyari kwa kunikamata nafika geti la nje natoa shingo yangu nje haraka s naona slesha ya kufyekea nyasi imesimamishwa karibu na ukuta naikimbilia haraka wepesi wakati huo jamaa ananikaribia Tena kwa spidi ya ajabu na yeye alipo ona nimeshika silaha akasimama gafla nikatishia Kama kumfyeka nikiwa nafanya Kama kujiami jamaa akarudi nyuma Tena akasita nikacheki jiwe jingine Tena nje kubwa nikatupa haraka slesha nikaliokota ile nafanya Kama kumrushia jamaa alirudi mpaka ndani kabisa Tena haraka ndipo fasta nikabana geti kwa nje na chomeko hapo ndio nilifanikiwa kutoroka nilimaliza nusu mwaka naishi mafichoni kwa jamaa zangu bila kurudi geto Hadi msala ulipo Isha yule binti alikuja akahama pale mtaani kwetu hiyo ndo ilikuwa ponea yangu
Hii kali
 
Mmea wetu pendwa ulikuwa hautumii mzee ... Huo ujasiri sio wa kawaida
 
Shikamooni wakubwa ! Wadogo shauri zenu. Ni muda sasa umepita tangu tukio hili litokee ila nimeamua kuwasimulia mkasa huu vizuri ili iwe funzo kwa wengine, na si mkasa huu tu bali nimeamua kila nitakapopata nafasi nitakua nawasimulia mikasa yangu niliyopitia.

Nakumbuka kuna siku niliwahi kuanzisha thread yenye kichwa cha habari ' NIFANYE KIJAKAZI WAKO SIKU YA KESHO' sina kumbu kumbu kama nimeandika sahihi ila wale wataalam mtanisaidia walau kuiunga ile link ya uzi ule na hiki kisa nitakachowasimulia leo.
Nakumbuka ndani ya ule uzi niliomba mtu yeyote aliekua na kazi yeyote aniite nije nimsaidie kuifanya buuure bila hata malipo ya namna yeyote ( hata nauli ya kwenda huko ningejilipia mwenyewe) ila watu wote waliogopa na wengine wakasema kama kutoa msaada nikatoe kwa watoto yatima, ila niliwajibu kuwa kwa sababu nimeamua kuufanya msaada wangu katika namna hii ni bora waupokee tu kuliko kunishauri kitu ambacho tayari nilishakiwaza kabla, kuna mdau mmoja(sitamtaja) ndio tuliwasiliana pm tukakubaliana ila lengo halikutimia. Nisiwachoshe sana twende kwenye mada halafu nyie mtaunganisha wenyewe mkasa ule na kisha cha mie kuomba kuwa kijakazi wa mtu kwa siku moja tu.

Siku yangu ilianza vizuri na kawaida kama siku nyingine, nakumbuka nilitakiwa nisafiri kesho yake kutoka mkoa nilipokua niende mkoa mwingine lakini sijui nini kiliniwasha, narudia tena kiliniwasha nikaamua kubadili mawazo na kusafiri siku hiyo hiyo, kwa kuwa muda ulikua umeenda sana (ilikua usiku) nisingeweza kupata basi hivyo nikaamua kuvizia gari yoyote ndogo.
Na kweli katika pilika pilika nikafanikiwa kupana NOAH ya jamaa mmoja ambae alikua peke ake kwenye gari hivyo bila kizuizi alikubali tuondoke wote nikapanda safari ikaanza.
Tulitembea safari yetu vizuri japo ile gari baada ya kuipanda niligundua ilikua imechoka sana tu, nakumbuka jamaa alijisifu yeye ni mzoefu wa ile njia maana hupita mara kwa mara. Usiku ulizidi kuwa mnene na sie bila hili wala lile tuliendelea kuchanja mbuga.
Katika safari za usiku kama kawaida ni lazima utakua check points za hapa na pale, basi tulizipita kama tatu lakini moja baada ya kusimamishwa kimbembe ndio kilianza.
Askari alietusimamisha aliuliza tulikua wangapi kwenye gari tukamjibu idadi yetu ni wawili, akawasha tochi akatumulika kweli akaridhika ula akaomba afunguliwe mlango wa nyuma kwa ajili ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha zaidi, hapo nikaona dereva kama ni mwenye wasi wasi akawasha taa za ndani fasta akamwambia afande aangalie tu lakini afande akasema yeye anataka kukagua kule nyuma kabisa anaomba afunguliwe, yule dereva akawa kama yupo njia panda, yule afande akaendelea kukomaa, ikabidi dereva atoe lock ila hakushuka, basi yule kamanda baada ya kufungua mlango alianza kukagua kwa makini sana( nahisi kuna mtu alimpa ramani) mara kidogo nikasikia afande samahani hebu njoo mara moja, kuna afande alikua pembeni kidogo akainuka na kwenda kule nyuma, wakati huo dereva alishazima gari kisha akawa ameufungua mlango kidooogo.
Baada tu ya yule afande kufika kule nyuma huku dereva alikurupuka kwa kasi ya ajabu akatokomea gizani, ndani ya gari nikawa nimebaki peke yangu na mie katika hali ya kupaniki nikajikuta nafungua mlango kwa kasi ya umeme nikimbie, lengo la kufungua mlango lilitimia na nikawa mguu nje, ile namalizia kutoka tu nikasikia kitu kizito kimenipiga kisogoni kisha nikajigonga kwenya mlango kisha nikaanguka chini kama gunia kisha baada ya hapo ikawa ni mvua ya mateke na makofi mpaka mwili wote ukafa ganzi.

Baada ya kile kipigo nilikula pingu kisha nikawekwa pembeni yao( walikua wanne) ubaya ile pingu nilifungwa vibaya kwa sababu upande mmoja ilifunga mkono na upande mwingine ikawa imefunga mguu kwa hiyo nikawa nimelazwa ubavu huku damu zikichuruzika mdomoni na kisogoni.

Baada ya hapo ndo nikaanza kusikia stori zao wakizungumza kumbe ile gari imebeba mrungi wa kutosha na bangi hapo ndo ukisikia jumba bovuuuu ndo hapo, niliwaza sana ni kwa namna gani kile kikombe kitaweza kuniepuka?
Hivi ni nani nitamwambia mie niliomba lift tu kwenye hiyo gari akanielewa?
Hivi ni mahakama gani nikipelekwa maskini mimi nitaweza kujitetea mpaka wakose hatia?
Hivi nitamshawishi nani na kwa kiasi gani mpaka anielewe ule mrungi sio mali yangu?

Baada ya kuwaza sana nikaona hakuna namna yeyote ya kuweza kukiepuka kifungo zaidi ya kukimbia, lakini nitaweza vipi kukimbia ikiwa nina pingu?ukweli ni kwamba haiwezekeni, sasa kama hqiwezekani nitafanya nini? Maana kilichokua kinasubiriwa ni difenda ije kunibeba nipelekwe kituoni.

Hapa niliwaza kitu kimoja, nifanye kisa chochote mpaka pingu ije kufunguliwa
Basi nikaanza kukoroma huku najitupatupa( kumbuka hapo nimelazwa ubavu halafu nimepinda kama samaki fulani huuzwa masokoni ambao hukunjwa mpaka mdomo unakutana na mkia)
Katika kujirusha kule kwa kuwa nilikua navuja damu mdomoni pia nilijaza damu nyingi sana mdomoni ili zitumike kama silaha ya kivita(usicheke)
Baada ya kukoroma sana na kujigeuza huku na kule kuna afande akawasha tochi akanimulika, mie hapo nikaona yes tayari wameanza kuingia king, nikawa nageuza macho juu, aliposimama kuja nikaanza kuimwaga ile damu taratiiiiibu kutoka mdomoni basi akaingiwa na hofu akachukua funguo akaja kufungua pingu kisha akanivuta mpaka pembeni kidogo kisha akawaambia wenzake huyu jamaa anaweza kutufia hapa anageuza macho naona na damu imemtoka sana(mie hapo naongeza juhudi huku akili ikiwaza next step) pigieni jamaa wawahi kuja.
Baada ya kuniweka pale pembeni akaja na maji akawa akamwagia( ndo mara ya kwanza toka nizaliwe kuoga maji ya kilimanjaro maana nililowa kila sehemu)

Baadaya tukio la maji nikaona sana nitulie ili nijipange vizuri ki medani za kivita, kusema ukweli sikua nikisikia maumivu hata kidogo yaani kwa kifupi nilikua poa kabisa yaani hata kama angetokea simba mitaa ile nadhani mie ningekimbia kuliko wao.

Unajua unapotana kufanya tukio ni lazima uwe na mawazo ni namna gani utalitekeleza bila kukuletea shida.
Kwa ukubwa wa tukio lile nilikua na wasiwasi sana juu ya maisha yangu ya baadae hivyo nikaja na mpango wa kutoroka katika namna mbili.

1/ Niwateke wale maafande kisha nichukue silaha zao nizipakie kwenye ile gari kisha niondoke nayo mpaka mbele sana kisha niitelekeze nitokomee zangu.

2/Nisubiri wajisahau nikurupuke kwa kasi ya umeme nitokomee polrini?
............. ntamalizia muda si mrefu.

Mwendelezo....................

Njia ya kwanza ingeweza kunipeleka kwenye matatizo makubwa zaidi, vipi kamq wangenishoot? Baada ya kuwaza sana nikaona ni bora niachane na wazo lq kwanza maana lilikua ni hatari sana kwangu

Wazo la pili nalo lilihitaji namna ya kujipanga na sio kukurupuka tu, katika muda ule ilibidi nipime ni kwa namna gani naweza kukimbia na hata wakisema wanikimbize wasinikamate? Baada ya kuchunguza sana nikagundua gari inapofika hapo mmoja ndie mwenye jukumu la kwenda kukagua gari halafu wawili watasimama mbele ili kuruhusu gari ipite, na mmoja anabaki pale pembeni na mimi.
Baada ya kuona kila kitu kipo sawa ilipokuja gari ile wameenda kuikagua mie nikakurupuka mbio sana na kutokomea gizani. Nilichosikia nyuma ni sauti ya yule tuliebaki nae akisema anatorokaaaa, wakajaribu kunifukuza lakini hawakufua dafu.
Nilikimbia kwa spidi bila kuchoka hata pale nilipohisi hakuna dalili za mtu kunifuata niliendelea kukimbia huku ninapoenda sipajui.
Nilikimbia mpaka nikachokanikaanza kutembea
Nilipochoka kutembea kwa haraka nikaanza kutembea pole pole
Nilipochoka nikasimama na hatimae nikakaa kabisaaaa
Hapo nilipokaa ndio nikagundua kuna limti lilinichoma mguuni na damu inatoka.
Baada ya kuvuta pumzi nikaendelea na safari huku sijui naenda wapi, nilienda sana nikachoka tena ikanibidi nikae tu,
Kulipoanza kupambazuka kuna dogo nilikutana nae akanisaidia sana wakaenda wakanipaka mafuta ya taa kwenye vidonda, sikujua kama ni dawa lakini nilichohitaji ni msaada.

Nilipelekwa mpaka njia kuu tena kwa msaada wa baiskeli, kama unavyojua mbwa hafi akiuona ufuko hatimae nilifanikiwa kufika nilipokua naenda,
Nililia sana baada ya kufanikiwa kufika salama na kujiguza mpaka kupona, nikajisemea mwenyewe ni lazima nifanye kitu maana vipi kama ningeendelea kushikiliwa pale? Je kesho yangu ingekuaje?

Baada ya kupona nilifanya vitu vifuatavyo

Cha kwanza nilinunua chipsi yai kama sahani nane, halafu nikachukua nguo zangu ambazo sikua nikizivaa mara kwa mara na pia nikachagua nguo mbili ninazozipenda nikapeleka pale Morocco mataa karibu na Airtel nikawapa wadogo zetu na ndugu zetu waliokua pale wakishinda wanaomba kwenye magari. Walifurahi sana hawakua wakielewa elewa hasa nini kilinisukuma.

Cha pili nilikua namsaidia yeyote alienifuata na kusema ana shida, hasa kama shida hiyo itakua ndani ya uwezo wangu.
Nakumbuka kuna siku nilikua Sinza kuna madogo wawili wakaniomba niwaelekeze ni wapi wataweza kupata gari ya kwenda mbezi, kwa lengo zuri tu niliwaelekeza na kuwaambia itabidi wapande gari mbili mpaka kwenda huko, nilichokuja kugundua hawakua na nauli, baada ya kupiga nao stori kidogo nikagundua pia ni shida tu inayowapeleka huko,
Nilichofanya niliwapa kiasi fulani cha hela ikawasaidie huko mbele, ninachokumbuka mmoja alianza kulia pale pale, hakuamini kama kweli mtu baki anaweza kukupa hela yote ile, hakikua kiasi kikubwa sana ila hakikua kiasi kidogo pia.

Cha tatu nikaamua kujitolea kufanya kazi ya mtu yeyote bila ujira hata senti, nikaanzisha ule uzi lakini kwa bahati mbaya wazo halikufanikiwa, lakini kwa kweli bado naendelea sana kujitoa kwa watu wenye uhitaji ulio ndani ya uwezo wangu.

Aksanteni
Na pia mnisamehe kwa kukatisha uzi.
Nilifanya hivyo kwa kuwa simu yangu tayari ilikua imeishiwa chaji sasa wasiwasi wangu ukawa unaweza ikazima halafu kazi yoooote niliyoifanya ku type ikawa imepotea. Nikaona bora niukatishe then nikifika mahala kwenye power niumalizie.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Daanh kisanga nnaku-feel man
 
Back
Top Bottom