Umeshawahi lala stendi bila kutarajia

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,744
Hii kitu ni mbaya sana hasa kwa safari zetu za watu wa maisha ya chini, na mara nyingi hutokea kwa kupanda gari bovu, au gari kuharibika njiani, au kudanganywa na wakata tiketi,

Kwa mara ya kwanza kabisa nilikuwa natokea singida naelekea kigoma kwa sababu za changamoto za usafiri kutoka kijijini nikajikuta nafika tabora saa 10 ya jioni,

Nikaambiwa kuna gari ipo njiani inatoka dar hivo inaingia sio muda mrefu hapo stendi, basi nika kata tiketi yangu bhana, yaani wale jamaa wajanja sana, ila tu nawaambia mbingu wataisikia tu kama hawajaacha hiyo tabia ya kuwadanganya watu, mpaka inafika saa 4 usiku wakaanza funga milango ya ofisi zao hatimaye nikawa nimekubali matokeo, ya kulala barazani huku mbu wakifurahia damu zetu, nilifanikiwa kupanda gari kesho yake saa 4 asubuhi tena gari bovu kabisa maana tulifika kigoma saa 3 usiku,

Safari ya pili ilikuwa kutoka tabora kuelekea singida baada ya kushuka kwenye tren nikachukua gari ya kuelekea nzega baada ya kufika nzega saa 9 mchana nikakata tiketi ya kuelekea singida iguguno, kama kawaida yao mkata tiketi aliniambia kuna gari ipo njiani inatoka shinyanga kwenda singida, baada ya kukata tiketi, nikasubiria weeeee, mpaka usiku unaingia wakafunga ofisi zao na kuniacha nikiwa nimeegemea ukuta nasinzia, nilikuja kupanda gari kesho yake saa 6 mchana sijui ni yakutoka mwanza,

Safari ya pili ilikuwa ni kutoka dar kwenda singida nilipanda kampuni moja hivi sii taji jina, katika safari hiyo gari yetu ili chemsha ingine morogoro sehemu ambako hakuna makazi hivo wakatafuta pikipiki ya kwenda kuwaletea maji tulikaa hapo kama lisaa 1, tukafika dodoma ikiwa bado kama kilometa20 kufika stendi kuu gari ikaharibika kwa mara ya pili ilikata sijui chuma gani huko uvunguni, ikabidi wafungue hicho chuma wakakichomelee tulikaa hapo kama masaa 2,

Baada ya gari kupona tulifika singida mjini saa 5 usiku muda huo hakuna gari ya kuelekea kijijini, ikabidi nilale stendi huku tukipigwa na baridi la kutosha,

Nilicho jifunza,

Asikudanganye mtu eti kata tiketi gari itakuja imejaa,

Usipande gari inayo ishia mwisho wa safari yako, mf. Unatoka dar unaenda moro, dodoma, au singida panda gari za mwanza, utapunguza kero za kuchelewa safari yako,

Nawasilisha
 
Kote ulipoeleza naona uzembe ni wako mwenyewe....ni mwepesi sana kuwamini watu!
 
Back
Top Bottom