Papa Mopao
JF-Expert Member
- Oct 7, 2009
- 4,166
- 2,670
Kuna siku nilisikiliza Redio One kipindi cha mchana wa saa saba hivi,mtangazaji bila shaka alikuwa Masoud Masoud kama sikosei,kilikuwa ni kipindi cha wasikilizaji kupiga simu kituoni hapo(studioni),sasa kulikuwa na mtoto mdogo(maana nlikuwa nna wasiwasi kama alikuwa ni mtu mzima) alipiga simu kituoni na mazungumzo kati yao yalikuwa kama ifuatavyo;
Mtangazaji: Haloo habari yako?
Msikilizaji: Nzuri,shikamoo!
Mtangazaji: Marhabaa! Kumbe wewe ni mtoto! Unasoma darasa la ngapi?
Msikilizaji: La sita!
Mtangazaji: Ok! Ngoje nikupe swali linaloendana na darasa lako, eeh?
Msikilizaji: Ndiyo!
Mtangazaji: Nitajie maana mbili za neno mbuzi?
Msikilizaji: Mbuzi mnyama tunayemfuga..
Mtangazaji: Eeenhe! Maana ya pili?
Msikilizaji: Mama anamwambia mtu mbuuziii weeweee!!
Nilicheka saaana siku hiyo na hata mtangazaji alicheka laivu redioni. Hiyo ilikuwa mwaka 2000! Kitu hiki kilikuwa cha ukweli kabisa.
Je, kuna yeyote anayekumbuka kituko chochote aongezee hapa! Angalau tupate afya ya kucheka!