Niliapa kuwa sitakwenda kwa mganga tena

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,650
Habarini wapendwa,

Imenichukua takribani miaka mitatu,kuandika hii historia yangu ambayo inaweza kuwa funzo kwa wengine na hata ya kuhuzunisha kwa baadhi ya watu lakini lengo kubwa ni kuwaelimisha wenzangu juu ya maisha na kumtegemea mungu pekee.

pia naomba itambulike wahusika katika hichi nitachopenda kushare nanyi kuhusu maisha wengi sana walisha kufa na sitojibu dm ya mtu yoyote kuhusu kuungwa au kusaidiwa na wahusika nitakao wataja.

Kwenye familia yetu tumezaliwa watoto watatu,mmoja akiwa ni wakike na wakiume tukiwa wawili tu, Maisha yetu wote yalianzia dar es salaam ambako wazazi wetu walikuwa ni wafanyakazi wa wizara fulani jijini hapo.

Baada ya mdogo wetu wakike kuzaliwa baba alipata barua ya uhamisho na kuamishiwa mkoa wa kigoma manispaa ya kigoma mjini sehemu maarufu ijulikanayo kama bimala.

Hapo palikuwa na ghala kubwa sana la dawa msd(bohari),maisha yetu yalikuwa mazuri sana kipindi hicho kwani ni mkoa ambao chakula kilikuwa kingi na hata mboga kama samaki,hasa hasa migebuka na n.k.

Wakati wazazi wakiwa wamehamishiwa Kigoma,ndugu zetu wengi walikuwa dar hivyo ilikuwa vipindi vya likizo tunaenda na wazee au na ndugu dar kutembea na baada ya likizo ilikuwa tunarudi Kigoma kwa ajili ya kuendelea na masomo yetu.

ilikuwa 2000s,tunatoka dar tunakwenda mkoa wa kigoma kwa wanojua bara bara enzi hizo wanajua ni jinsi gani kulikuwa na matukio ya ujambazi hasa ndani ya mapori ya Tabora,kipindi hicho ilikuwa mkifika baadhi ya sehemu ni ama mlale, na ikifika asubuhi basi mnasindikizwa na escort ya polisi mpaka sehemu fulani then mnaendelea na safari yenu,sijui kwa sasa kama hali iko hivyo au imebadilika.

Wazazi wangu ni watu ambao walipitia jeshi kipindi hicho hivyo walikuwa na ule ujeshi jeshi na kujiamini vile vile,bas tulipofika tabora baada ya kula mzee aliamua tuunge tu moja kwa moja licha ya kupewa tahadhari na askari wa kituo X kuwa huko mbele hali ya usalama siyo nzuri.

Kutokana na nguvu na cheo ambacho alishakuwa nacho huko nyuma,hakutii maagizo hivyo ilibidi tu askari wamkubalke kishingo upande kwani walikuwa hawana njia na ukizingatia hapakuwa na gari ya polisi ya kusindikiza gari moja tu wakati asubuhi kuna gari nyingi ilibidi zisindikizwe.

Safari ilikuwa ndefu na kadri defender yetu station wagon ilivyokuwa inakata pori ndivyo sauti zetu zilikuwa zinazidi kupungua na kusikika mlio tu wa engine ikibadili gear mama na mdogo wangu wakike wakiwa wamelala ,kaka,mimi na mzee tukiwa macho tukiangalia pori huku gari ikichanja mapori.

Tukiwa kwenye mwendo wa kasi bahati haikuwa yetu mida ya saa 7 usiku wakati tupo road tukakuta bara bara imewekwa bonge la gogo barabarani tukasimama umbali wa kama meter 20 tu kwani ilikjwa ukikata tu kona gogo hilo.

Mzee akataka kujitahid aligeuze gari pale pale kwani alikuwa ameshajua nini kinaweza tokea dakika chache zijazo lakini bahati haikuwa yake kwani.

Ghafla tu walitokea watu wakiwa wamebeba bunduk nzito, Naweza kusema ndo kwa mara yangu ya kwanza kuona mtu kashka bunduki huku kajizungushia mkanda wa risasi mwilini bro wangu ile kuwaona tu akakata moto tuliokuwa hatujazmia tulikuwa watatu 4, mimi, mzee na bimkubwa na mdogo wangu wakike.

Niliiona hofu kwa mzee na bimkubwa kwani mda ote alikuwa akilia na kusema chukueni kila kitu niachieni watoto wangu,hakika walikuwa wanatisha kwani walikuwa ni weusi tii na warefu mno na wasiokuwa wanaongea sana wakiwa na bunduki zenye mikanda ya risasi huku wakiwa wameshika na mapanga ambayo mengine yalikuwa yanadamu kabisa iliyogandia.

Basi tulishushwa ote kwenye gari huku ikiwa vile vile inanguruma brother wangu alitolewa na kulazwa chini huku wengine tukipigishwa magoti kwa mstari mnyoofu,mbele ya gari taa zikitupiga usoni na huku wenyewe wakiwa nyuma yetu tukiwaachia migongo.

Tulichezea sana vitasa kwa kupigwa fimbo na bapa za panga wakimfosi tutoe kila tulichokuwa nacho, mzee alidhalilika mno mwisho wa siku walichukua mpka viatu nakumbuka viatu vyangu vya kitoto vya kuwaka taa vile vya superman,then wakaondoka mpka na gari yetu wakimuacha mzee peku na suruali tu.


Tulikaa pale mpka saa 12 asubuhi ndo tukapata msaada kutoka kwenye mabasi ambayo yalikuwa yameanza safari wakatuchukua moja kwa moja huku tukipata msaada wa kandambili na shati kwa mzee.

Tuukaenda polisi but hawakuwa na msaada mkubwa,sababu taarifa zilifika kuwa jana yake tulionywa lakini tukawa kichwa ngumu zaidi tulipewa pole nyingi na kuambiwa taarifa zetu zitafanyiwa kazi

Mzee akapiga simu kigoma ikatumwa nauli tukarudi kigoma safari hii tukitumia usafiri wa treni, tulienda moja kwa moja mpka kwa baba yake(means babu)ambaye yeye alikuwa anakaa sehemu moja inaitwa kasingirima,

Sasa babu yeye kila alivyokuwa anahadithiwa alikuwa anacheka mno hasa akimuangalia bro na ujanja wake ote et kazimia,upande wa baba yeye alikuwa na hasira mno alichokuwa anataka yeye ni wale watu awashikishe adabu hata kufa wafe, japo mzee alimsisitiza sana afikirie hayo maamuzi yake na asitumie hasira zimtawale japo juhudi zote hizo ziligonga mwamba,babu hakuwa na hiyana basi ilivyofika usiku tukaelekea sehemu fulani inaitwa ujiji kwa mzee fulani alikuwa anaitwa Juma njemba.

Mzee Njemba alikuwa ni mganga maarufu ujiji nzima kwa kipindi hicho kuanzia kupanga matokeo ya mipira kwa timu kama za congo na mbanga kwa kipindi hicho na mambo mengine mengi ya kutisha.


Nadhani kwa watu wa kigoma wanaweza kuwa wanamjua baada ya kufika kwa mganga ,akaelezewa kila kitu kisha akasema hicho ni kitu kidogo sana,huku na yeye anacheka kisha akasema kuwa pale kwake kuna mbuzi ambae alikuwa anataka kumchinja sababu ya sherehe ya mwanae hvyo itatubidi tumtafutie mbuzi mwengne amreplace ili iwe kama malipo yake.

baba akakubali,kilichofata akawaita wajukuu zake walete (ubumba) ni udongo fulani hivi wa mfinyanzi kisha akawa anatengeneza kimdoli kidogo cha udongo kama vile vya kitoto toto,baada ya kukitengeneza akaanza kukiandika maneno yake kisha akakisimamisha chini,then akaanza kuongea maneno yake aliongea sana baada kama ya saa 1 akasema mtu yoyote ndani ya hichi chumba haruhusiwi kukimbia wala kupiga kelele kwani kwa kufanya hivyo ndo itakuwa kifo chake.

Basi aliendele kusema maneno yake ghafla yule mdoli pole pole alianza kukua na kuwa mkubwa pole pole,baada kama ya dakika arobaini alikuwa ni mkubwa kama binadamu mwenye mwili mkubwa alikuwa anamkono na kifua kikubwa na mrefu,kwa mara ya pili bro tena akazimia kwa mara ya kwanza mimi mkojo ulishantoka natetemeka kama nmepatwa na dege dege,mwisho yule mdoli akaambiwa shtaka letu kisha akaambiwa nenda hivi vitu vinatakiwa leo leo,then yule mtu akafungua mlango akatoka mbio alikuwa ni mwanaume lakini yupo uchi na ni mweusi tii kama mkaa mpka macho hakuwa na ichi kiini cheupe ye alikuwa na kiini cha moja kwa moja cha weusi,alivyoondoka tukaanza kumpepea na kumwagia maji bro alivyoshtuka yule mzee akatuambia kazi imeshakwisha kesho mtayapata majibu yenu.

Ilivyofika asubuhi tukapigiwa simu nakumbuka enzi hizo kulikuwa kuna buzz siyo hii tigo na hata simu zilikuwa za mezani,tukaambiwa kuwa kuna gari imepatikana Tabora yenye namba kama tuliyoripoti pamoja na vitu vingine.

Hivyo tunatakiwa kuripoti kituoni kwa ajili ya utambuzi, tukaanza safari na treni mpka tabora kufika kule tukakuta vitu vyetu na vingne vingi tu ila mzee alisema vyote vilikuwa vyetu hela zilikuwa kama 1m lakini zilipatikana 7m polisi hawakuchukua hata cent na hata walivyopewa walikataa kata kata hakikupotea hata kifungo kisha baada ya kuchukua, mzee kwa akataka kujua vitu hivyo vimepatikana vipi ndo tukaambiwa kuwa hao majambazi waliotuibia walikutwa msituni wakiwa wameuwawa wakasema wanahisi ni wanyama wakali ndo waliwauwa maana walikuwa wanaalama za meno makali milini mwao na kucha.

lakini wakashndwa kuelewa kama ni wanyama ndo waliwashambulia ni wanyama aina gani na kwanini hawakuwapiga hata risasi moja hao wanyama na wakati walikuwa na silaha nzito?

Baada ya maelezo mengi mzee akawasha gari mpka kigoma stend ya kwanza mpka kwa yule mganga tulinunua mbuzi na zawadi nyingne nying lakini mzee aligoma hakutaka chochote zaidi ya mbuzi tu,basi tukampa mbuzi wake, akasema imebaki kazi moja tu na kazi yenyewe ni kumrudisha yule kiumbe(mdoli mtu)ili asitudhuru na sisi maana ni wetu hapo ndipo ilipokuwa mtihani maana kuna msharti mengi tulikosea plus kujisahau sasa akawa anatuandama sisi atuue dah kila mmoja nyumbani anaalama ya yule kiumbe yangu ni kungatwa skio na kula kipande nikipata mda ntawamalizia kisa changu but mpka leo mimi kwenda kwa waganga ni big no,but thanks god tulitoka salama

NITARUDI EID MUBARAK
 
😄😁😄😁 hahahahahahahahhahaahahahhaahahaahahahahahahahahahahahahhahahahhhahaahhaahaaaahahahahaaahaahhahahahahahahahahahahahahahaahahahahaahahahahahahhahahahahahaahahahahahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaaahahhhahahhahahahahahahahahahahahahhahahahahahahahahhah
 
hahahahahahahahhahaahahahhaahahaahahahahahahahahahahahahhahahahhhahaahhaahaaaahahahahaaahaahhahahahahahahahahahahahahahaahahahahaahahahahahahhahahahahahaahahahahahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahhahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahaaahahhhahahhahahahahahahahahahahahahhahahahahahahahahhah
Hehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehhehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehehe

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom