Sitasahau 2016, nilipungua kilo sita ndani ya wiki moja

Nilisikiaga story moja inasema , muuzaji wa cheni feki ya dhahabu ,alimuuzia mtu ambaye alitoa fedha bandia kipindi flani hiv pale kariakoo , watu wakasema ngoma dro , or mechi imetoka dro
 
Tuendelee

Sasa akili ilianza kuwaza mambo mengi wakati huo nikiwa naelekea kinondoni biafra nilipofika biafra kiwanjani kuna jamaa nafahamina nae nika muelezea juu ya tatizo la gari jamaa akacheka sana akaniona kama wakuja hasa pale nilipomwambia bei nilionunulia nlikua nimeinunua ml 11 lakin nilimpa ml 10 kesho yake antamilizia akanambia twende nikakuoneshe ist ya bei hio hii umepigwa nikamwambia sawa tukavuka barabara pale biafra kama unaenda Morocco kuna show room zipo tatu sasa ile ya katikati siwezi kuweka jina hapa tukaenda tukamkuta jamaa ambae yeye anafanya kazi pale tukaongea nae akasema leo unaweza kuiona lakini ipo ofisi nyingine tukaenda


Ofisi yao nyingine ipo barabara ya kutoka Morocco kama unaenda victoria sheli ipo upande wa kulia tukaenda aseah ist ilikua nzuri hatari yaani imekaa kisasa yaan ipo poa sana nikaambiwa bei ml 11 dah yaan ilinibidi nijione boya kwakua niliipenda ilinibidi niongee na yule mfanyakazi wao wasiiuze jamaa akanambia inabidi nitoe kishika uchumba nikatoa laki tano ili isiuzwe mida ya saa kumi na moja jioni nikaondoka kurudi nyumbani huku nikiwa na mawazo juu ya kile kimeo nakirudishaje kwa mwenyewe
Usiku kucha nlikua nawaza jinsi ya kuirudisha ile gari ili nipewe pesa yangu nikalipie ile nyingine


Kesho ikafika nikaenda mpaka pale show room magomen mikumi nlipofika ilikua mapema sana saa mbili kasoro nilikaribishwa na dada wa mapokezi katika maongezi yule dada akaropoka kuwa ile gari ilikua inatumika Zanzibar na mdogowake mwenye show room dah apo ndo nikagundua ndo mana ipo vile dah sasa wazo lilikua napataje pesa zangu nikakaa mpaka yule mwarabu mwenye show room akafika alipofika akafurahi tukaingia ofisini baada ya salamu akanambia jamaa yake amefatilia usajiri mpaka saa sita atakua kashakamilisha dah nikaona huu mtihan


Ikanibidi niwe msanii palepale nikaanza kumwambia yule mwarabu kuwa baba wa kambo kachukua mkopo kaweka hati ya mashamba ya mama sasa benki wanataka kuyauza na leo ndo mnada unafanyika inabidi nimuokoe mama maana kazimia mara mbili na mimi ndo mkombozi wake wakati naongea huku machozi yananitoka dah yule mwarabu akaniuliza sasa ulikua unatakaje nikamwambia naomba biashara tuighairishe mwarabu akanambia subiri akampigia jamaa yake wakaongea kisha akanambia gari ishapata namba itabidi hii gari uniuzie maana yake mimi ndo nimuuzie yeye dah kwangu ilikua ngumu sana


Ikabidi tupatane akakubali kuinunua kwa ml 9.5 na mimi nlimlipa ml kumi jana yake basi akanipa ml 9.5 nikaondoka faster mpaka kinondon nikamchukua yule jamaa yangu tukaenda kuilipia ile gari kwa wale wahindi wakanambia kesho nikamalizie ml moja mana jumla ilikua ml 10 nikaondoka kesho yake nikamalizia ml 1 nikachukua gari nikaondoka lakini ile gari ilikua chinichini sana yaan kwenye tuta mpaka ulipande kiubavu kingine shokap zilikua zimechoka sana lakin nikaona sio tatizo kubwa nilivyofika home nikamwita fundi alipocheki zile shokap akanambia izi zinatumia coil spring moja laki mbili na nusu zote nne zinauzwa ml1 nikaona huu mkosi



Nikwapigia wale wahindi kuwaelezea wakanambia niipeleke kweli kesho yake nikaipeleka wakamwita fundi wao fundi wao akaichukua akaenda kuitengeneza nikaambiwa nirudi jioni nikaondoka naomba nitaje jina la mtu alienisaidia sana jamaa anaitwa Hassan mfanyakazi wa wale wahindi ambao show room yao inaitwa chief cars dah yule jamaa alisimama upande wangu kuhakikisha sidhulumiwi

Jioni niliporudi nilkuta gari imebadirika sana imekua na shape mbaya coz kafunga shokap za kawaida ikawa imeondoa ule uzuri wake alafu bampa la nyuma lilikua limemfumuka nahisi alipita njia za mashimo dah ilikua sio ile tena mawazo ya kubadirishiwa yakanijia lakin nitaanzaje nikapewa gari yangu nikaondoka mpaka njia panda ya kagera pale kuna sheli alafu pembeni wanaosha magari nikaiosha nikaondoka mpaka home kesho yake nikaenda kibaruani kuna jamaa akaipenda akataka nimuuzie lakin ilikua imeenda km nyingi sana mpaka jamaa akashangaa ilikua na km149000 akaikataa dah apo sasa mawazo yakanijia lazima nibadilishiwe gari tatizo lingine ilikua inawaka taa ya check engine ata ikiwa inatembea



Jambo la kushangaza tangu niichukue mshale wa mafuta ulikua upo palepale haupandi wala kushuka na mimi cjaongeza mafuta jioni wakati narudi home nilipofika magomen usalama gari ikazima ghafla nikahisi mafuta geji itakua mbovu jamaa wakanisaidia kuisukuma mpaka pembeni nikaweka mafuta ya elfu tatu gari ikawaka nikaondoka uku nikijisemea moyoni kesho nairudisha kiukweli ujalala vizuri usiku huo asubuhi nikaenda pale cheaf cars nikamkuta Hassan nikamweleza kuhusu taa ya check engine kuwaka akanambia tumsubiri boss wake aje boss wake alivyofika nikamuelezea akakasirika akaniona mimi mkorofi naleta vurugu ofisini kwake akaita walinzi wanitoe nikawaambia mimi ninaushahidi kuwa gari haipo sawa wakinisumbua naenda polisi then naenda tra dah muindi kusikia tra akanambia subiri akamwita fundi wake


Fundi alipofika nikamuonyesha video nilioirekodi ya taa ya engine akasema mie muongo yule muhindi akamwambia wapande waitest kweli wakaingia wakaondoka baada ya muda wakarudi wakabaki ndani ya gari huku wanajadiliana mara ghafla gari ilianza kutetemeka ikazima kila akiwasha haiwaki mshale wa gaji ya mafuta upo kati wakashuka yule muhindi akaniuliza mara ya mwisho lini kuweka mafuta nikamwambia jana nimeweka ya elfu ishirini akasema basi gari inashida ingia ndani chagua gari nyingine aseah nilifurahi sana nikachagua spacio new model wakanisajilia siku iyoiyo mida ya saa nane yule fundi kaja kanikuta natoka na gari akanambia we jamaa msumbufu kumbe geji mbovu nikamwambia mwambie boss wako yule Hassan nikampa laki akakataa akasema ametimiza majukumu yake


Namshukuru mungu mpaka mwaka jana nimeiuza haijawai nisumbua chochote hakika nimejifunza sana ilifikia hatua nilikonda na uzito wa mwili ulipungua ndani ya siku sita tu

Nawasilisha
 
Dah hakuna kitu kinaumiza moyo kama kuwa na gari mbovu, yaani muda wote mashaka
 
Kila mtu katika maisha kuna vingi anapitia hatuwezi kufanana katika mapito
Shukuru Mungu wewe ni mkazi wa Dar zilipo hizo yard.

Je ungelikuwa unatokea mikoa ya uswekeni kuja kununua gari na haraka haraka za kugeuza na mchuma, ingekuwaje?

Changamoto uliyosimulia, ndiyo inayowakatisha tamaa wahitaji wa kweli wengi.

Mtu anapotaka kuanza kumiliki gari kwa mara ya kwanza, lazima atumie ngvu kubwa hata kwa gari la bei rahisi kulipata gari zuri na zima.

kwa kweli ni mtihani sana hadi apate watu waaminifu wamsimamie.

Hakuna cha yard hakuna cha mtu binafsi, kwenye manunuzi pote ni majanga, yaani ujanja ujanja tu, hili waTz sijui tutaliacha lini, maana tabia hii inaharibu taswira nzima ya biashara ya magari!
 
Back
Top Bottom