Sitakubali Rais Samia ahujumiwe

Sitakubali Rais Samia ahujumiwe

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
1,348
Reaction score
1,466
Serikali hii ilianza vibaya. Walianza kwa kujitenga na Magufuli bila kujua watanzania wengi walimpenda, na hata ambao hawakumpenda walihuzunishwa na kifo chake kwakua walimzoea.

Hapa tulipofikia, wale waliotakiwa kuridhika na serikali kutokua chini ya Magufuli, hawaridhiki na serikali iliyopo na wale wapenzi wa Magufuli wanaona wamesalitiwa kwa serikali kuanza kurudi nyuma ya alipokua Magufuli.

Mimi sikuridhishwa na teuzi za mh. Raisi, mojawapo ikiwa ya Ummy Mwalimu TAMISEMI. Kuna teuzi zilizonifurahisha kama ya Mchengerwa wa Utumishi, huyu bwana anapenda sana utumishi hata kabla ya kuwa waziri ( nasubiri kupanda daraja mwezi huu).

Jambo ambalo sitakubali ni watu kuanza kumpima Raisi Samia, maagizo ya Rais yametoka kuhusu masuala flani lakini watu wanaenda tofauti kwa kupima uimara wake.

Mnaofanya hivyo mjue Raisi hayupo peke yake, yupo na sisi tulio tayari kufa kwa ajili ya nchi yetu na tutamlinda Rais wetu.

Karne ya 21 hii jamani, binadamu aliyehai leo amestaarabika zaidi kuliko binadamu wa kipindi chochote tangu mwanzo wa ulimwengu.
Kwanini tunaishi kama hayawani wasio na ustaarabu hata kidogo?

Hayawani wao kuzaa na nduguze, mama na baba zao ni sawa tu, sisi tusiwe hivyo. Sisi ni viumbe tuliostaarabika sana.

Sasa kama mtashindwa kuwa wastaarabu, niwaambieni tu. Nchi hii sio ya kwenu peke yenu, tupo wengi ambao tupo tayari kuweka maisha yetu rehani ili nchi yetu ibaki na amani iliyokua nayo.

Raisi Samia piga kazi, watakaokupima utuambie sisi tutawatengua viuno.
 
Usitutishe alisikika marim seph
 
Usitutishe voice for marrim seph huna lolote,kwana hakuna anae mkwamisha miezi 3 nyuma kila MTU alimsifia kasoro mm nilijipa mda kwanza,ajiulize upya anakwama wapi.
 
Hata mwendawazimu anayetembea uchi mtaani hujiona ana akili hata akiambiwa yuko uchi atakataa kata kata.

Akili ninazo ndugu yangu, soma vizuri bandiko. Halina upande, nimegusa pote.
 
Mzee mwigulu muchemba umeona uje upumulie huku utopolo wako. Magufuli alikiwa akisema kesho unarudi nyumbani kwa Basi ujue kesho yake utaenda kweli na v8 la serikali ulipaki na usilishike tena .
 
Huna lolote wewe !! Anachodaiwa ni jambo la kikatiba . After all kujenga uchumi ni swala endelevu . Siyo swala la Samia tu alianza Nyerere mpaka leo , lakini bado uchumi haujawa stable.

Katiba tu watu but wanataka. Mengine hayo ni ya kwake
 
binadamu aliyehai leo amestaarabika zaidi kuliko binadamu wa kipindi chochote tangu mwanzo wa ulimwengu

Raisi Samia piga kazi, watakaokupima utuambie sisi tutawatengua viuno
Hongera kwa ulichokiandika hapa na nilicho quote hapo juu yaonesha wazi kuwaa waafrika wanaitaji ukombozi wa kifikra kama BAK aliyosema ujinga mtupu
 
sio mbaya umeeleweka kiongozi.ila mi naona ni vema wanavomjaribu ili ajipime kiasi gani yuko stable,hii ni kawaida kwa mtu anayeongoza kundi kubwa ,lazma watu wata ku challenge tu.angalizo teuzi zake huenda ndo zikamkwamisha.kuna vifaa alivitengua, baadae atavimisi,Kuna teuzi aliziweka bila kuangalia impact yao kwenye hizo nafasi.japo wapo aliowateua wako vizuri.
 
Kabla sijaendelea naomba unipe ufafanuzi ni namna gani unayapata majibu au matokeo ya ustaarabu
 
Huyu anajihujumu mwenyewe kupitia mapolisi,mwingulu,shaka nk! Kwa kufupi amezungukwa ni watu wasiomtakia heri na fanaka kwy uongozi wake aliopata kibahati flan ivi!
Anatakiwa kufanya reformation na kureoganize timu yake objectively bila mihemko.
 
Back
Top Bottom