KUtoka mwananchi:
NImechukizwa na kukerwa na habari kuwa Rais wetu ameenda nje ya nchi kupimwa akili pamoja na mambo mengine! Hivi hao waliopanga jambo hilo wanamfikiriaje? Kwani ana dalili zozote za kutokuwa mzima akilini? Sitaki kabisa na tena sipendi Rais wetu apimwe akili ugenini; ni kudhalilisha taifa, na kutudhalilishwa wananchi.
Unless walikuwa wanapima kitu kingine zaidi kwenye ubongo! Lakini kama wangeweza kugundua kuwa ana matatizo kwenye akili bado angeweza kuwa Rais?
Watanzania tuacheni mzaha:
JK ni kweli mwenye matatizo ya akili
- Hii ni baada ya kukubali mwenyewe kupimwa akili yake
- Asifiwa kwa kukubali kupimwa akili kwenye hospitali ya wendawazimu huko Caribbean
- Mhe Zitto nae bora akubali kupimwa ili turejeshe tamaa yetu kwake
Tandika, Dar Es Salaam
Bila ya kujali kuwa Bi Waridi wa JF atasema tena kuwa
"hii sio ndio Wamarekani wanaita shit ya ng'ombe dume", Wagagagigikoko walionesha mshangao mkubwa kama walivyopigwa Watanzania wengi kuhusu maneno ya yule Mwenyekiti wa Kijiji cha Butiama kule Tarime ajulikanae kwa pseudonym lake la
Mzee Mwanakijiji, pamoja na ma-nazi wake 35 waliompa "Thank You Baba" pale JF, baada ya Mzee Mwanakijiji kulia hadharani kuwa eti hataki kabisa na wala hapendi tena Rais wetu kupimwa akili, kwani hio inadhalilisha Taifa na kuwadhalilisha wananchi.
Wagagaggigikoko wameshangazwa sana na hii patriotism isiokuwa na mpango na wala muelekeo ya huyu Mzee Mwanakijiji ambae anaheshimika sana pale JF na ambae ametoa jumbe zaidi ya 16,000 kuisifu CCM pale ukumbini..
" La maana ambalo angeweza kulifanya Mzee Mwanakijiji sio mtu mzima kulia hadharani, bali kumuombea dua Rais wetu mpenzi ili huo muondoko wa akili uwe kidogo kidogo ili apate kumaliza na hio miaka 5 ijayo kwa salama na amani. Lakini, kukasirika na kusema kuwa tumedhalilishwa wakati kila mtu anajua kuwa Rais wetu kweli ni mwenye tatizo la akili ni kudharau ushauri mzuri wa kitaalamu unaotolewa na madaktari wa Rais wetu", waliendelea Wagagagigikoko.
" You don't need to be a neuro-surgeon kufahamu kwamba matatizo ya ugonjwa wa akili yanakuja kwa spells (attacks) – kama vile ilivyomtokea Mwanza. Pale mgonjwa anapopata attack ndio wakati mzuri wa mngonjwa kupimwa ili extent ya maradhi yake ijulikanwe. Hii attack inatokea wakati wowote ule na haingojei mpaka urudi safari au mpaka uwepo DSM," kafahamishwa Mzee Mwanakijiji kwenye barua pepe aliyopelekewa huko kijijini kwake kwa kupitia ma-nazi wake wawili ambao wote majina yao ya mwanzo ni
PAKA!
"Kama sio mtu aliyepata hio attack ya akili huko Jamaica, inawezekanaje Rais wa nchi mwenye akili zake timamu akubali kupanda bembea kama mtoto wa shule,
wakati theluthi mbili ya watu wake wanalala na njaa? Mzee Mwanakijiji ni lazima ufahamu kuwa kwa mtu mzima aliejukuu kupanda bembea (baada ya kuwaachia wajukuu zake kupanda) ni dalili ya kuonesha kutokuwa mzima akilini, na kwahivyo usistaajabu kwanini akili zake zikachunguzwa na wataalamu nje ya nchi," alimalizia muandishi wa Wagagagigikoko.
"Ugonjwa wa akili ni sawa na ugonjwa mwengine wowote ule. Ikiwa tunamruhusu Rais wetu kuenda nje kupima moyo wake na afya yake yote in general, sasa kwanini iwe tunadhalilishwa kama anakuenda nje kupima akili yake?" Wagagagigikoko walimuuliza Mzee Mwanakijiji kwa sauti kali sana kama vile alikuwepo mbele yao pale makao makuu yao nyuma ya Kariakoo.
"Kwa upande mwengine, ni vizuri Rais wetu kaenda kucheki akili zake huko nje, kwani sasa nchi za nje wanajua kuwa matatizo yetu ya umaskini nchini sababu yake ni nini, na labda wanaweza kutusaidia zaidi kwa misaada kuliko hapo mwanzo", alielezwa Mzee Mwanakijiji.
"Hii sio dementia na wala sio Alzheimer", alisema Daktari wa Wagagagigikoko na akaendelea, "Mtu akikwambia nipime homa, basi huyo either tayari homa anayo, au tayari anaona baridi baridi na homa inamtambalia karibu karibu. Ugonjwa wa akili upo hivyo hivyo. Mtu mwenye akili timamu hatotaka apimwe akili. Ukimsikia mtu anataka apimwe akili au anashauriwa apimwe akili yake, basi tayari huyo ana matatizo ya akili", kamalizia Daktari huyo.
Memba mmoja wa JF alinukuliwa na Daktari wa Wagagagigikoko kwenye msg yake ukumbini akisema, "
mtu anaenda kupimwa kile alicho na wasiwasi nacho mwilini mwake, sasa mkulu ana mashaka na akili yake hivyo ni haki yake kuamua ipimwe. Nampongeza sana maana hiyo ni dalili nzuri kujishuku", alimaliza memba huyo, huku akimpiga vijembe JK kuwa tayari ni muendawazimu wa kuokota vikopo mitaani..
Kuonekana kwamba JK anayo matatizo ya akili iwe sasa ni fundisho na somo kubwa kwa Watanzania kuwapima ma-Rais wetu kabla ya kuapishwa. "Na huyu mjukuu wake Mzee Mwanakijiji aitwae Zitto nae pia apimwe, kwasababu haya mambo anayoyafanya hayafahamiki kabisa", alieleza mwana-kada mmoja ambae chama chake hakukitaja.
Alivyoshikiliwa aelezee zaidi kwanini anamtia Mhe Zitto ambae hana kosa kwenye balaa hili alisema, " Ninaamini kuwa yeye Mhe Zitto hajaharibikiwa akili kiasi hicho kama Rais wetu, kwani hata bembea bado hajapanda, lakini kule kumsifia Dr Rashid hadharani, pamoja na hii tisha tisha yake kwa Dr Slaa na Mbowe kuwa anatembea na barua ya kuhama Chadema mfukoni mwake huko Ujerumani, na ukijumlisha na yale maneneo yake ya juzi kuwa atachukuwa uamuzi ambao haujafikiriwa na yoyote – mambo kama haya yatamtia mashaka daktari yoyote yule wa akili akiyasikia, na kwahivyo bora nae Mhe Zitto (bila ya kumkusudia vibaya) afuate mfano mzuri wa Rais wetu na aende kwa hiari yake kupimwa akili yake, ili tupate kurejesha tamaa yetu kwake", walimalizia Wagagagigikoko.
Sources: Wagagagigikoko News Network (Wanene)