Sitaki tena, sipendi wampime Rais akili!?

wamekuta ana akili ngapi sasa???
eee! tuambiwe tujjue dereva wetu yupoje!! usikute zimeisha zote!
 
Kwa tatizo hilo hata kama angekuwa nalo hapa nchini hatuwezi kumpima rais wetu mpaka akapimwe nje ya nchi? Kwa mpango huu tutajenga hospitali ya maana hapa nchini kweli? Maana imeshakuwa utamaduni sasa hata mafua ukishakuwa na madaraka lazima ukapimwe nje?

Wataalamu wa afya watusaidie kuhusu hili.
 
Hapana jamani sii kwamba blongata ya mheshimiwa ina mushkeli bali kilishomsukuma kupima akili ni kampeni ya kivitendo ya kuwashawishi mwawaziri wake kupima akili kutokana na kuropoka hovyo sawa na ushauri wa Malecela kwa SS.
 
Wengine walisema oooh anatibiwa kwa waganga wa kienyeji! Sasa tunaomba tuambiwe ni daktari wa hospitali au mlingotini aliyempima akili?
 

Ama kweli Watanzania sio Mabwege tena...Dr. Harrison Mwakyembe
 

Haitakuwa vibaya akatumegea kidogo waliyoyaona katika akili yake maana lazima itakuwa na kasoro ya aina moja au nyingine mpaka kuwa kiongozi dhaifu kiasi hiki.

Ana vyombo vyote vya dola nyuma yake Jeshi, polisi, FFU, Mahakama na Watanzania milioni 40 lakini anashindwa kumchukulia hatua fisadi mkubwa ndani ya nchi yetu papa fisadi Rostam Aziz pamoja na kuwa na ushahidi wa kutosha kuhusika na wizi wa shilingi bilioni zaidi ya 200. Kikwete anaogopa hata kuamuru huyu fisadi ahojiwe tu, hii si dalili ya akili iliyo kamili hata kidogo.

Kama akili yake ni sawa na bado ni dhaifu kiasi hiki pamoja na nguvu kubwa alizokabidhiwa na Watanzania, basi tunahitaji Rais mwenye akili nusu ili afanye kweli dhidi ya mafisadi.
 

wakati mwingine ukweli unauma; lakini nadhani umegusa karibu zaidi na ukweli.
 

na watu bwana kushindwa kuunganisha mambo.... hivi hamjawahi kuuliza kule UAE kuna nini?
 
mtu anaenda kupimwa kile alicho na wasiwasi nacho mwilini mwake, sasa mkulu ana mashaka na akili yake hivyo ni haki yake kuamua ipimwe. Nampongeza sana maana hiyo ni dalili nzuri kujishuku.


watu mna majibu utadhani mnaigilizia!
 


yaani nacheka hapa hadi machozi!
 
Ndugu wananchi mliomo hapa, mimi sina neno lolote zaidi ya kuomba mama yangu mpendwa sana, Sophia Simba ikiwezekana nae aende kupata huduma hii ya kipimo cha Ubongo! Hii itatufanya tumuelewe vizuri zaidi kwenye matamko yake ya huko mbeleni. Na pia anaweza kujiweka vizuri kwenye ulingo wa siasa kama ndio fani bado anayoipenda.

Mungu Ibariki Tanzania, asanteni kwa kunisoma
 
hivi ni yeye mwenyewe au ni washauri wake ndio waliomshauri akacheki akili?
na hasa sijuhi kilikuwa ni kipimo gani, IQ, utahahira au uchizi?

kweli watajulikana kwa matendo yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…