stable woman
JF-Expert Member
- Nov 12, 2013
- 3,884
- 4,484
Mwaka mmoja bado ni mapema sana hata kumshitaki kwao! Kikubwa ujaribu kuongea nae usichoke kumshauri na Kama pia Una imani usichoke kumwombea Mungu pekee ndie awezae kubadilisha tabia ya mtu!
Mpaka lini utakuwa single? Time is macangability
Kwa yesu spade4spade
Hahaaaaa cousin umenichekesha na time is makangability
Ulinitosa
Kumbe nilikosea, nilitaka kusema bila 'ma' afu ningeongeza huko mbele 'o'. Sijui kama lingefanana na jina lako minus 2.
Hapana sijakutosa
Ndio ndoa hizo mama vumilia tu
jina langu zuri sana unajuaa
Natumaini mu wazima! Ni mwaka 1 sasa toka tumefunga ndoa na mwenza wangu na tumejaliwa mtoto mmoja! Na sote ni wafanyakazi. Tatizo huyu mume wangu hanishirikishi katika kila analolifanya, mfano aliwahi kuchukua mkopo bila mimi kujua lakini hakufanyia kitu chochote, alijipangia bussines plan mwenyewe na kumweleza rafiki yake kuwa anataka kufanya kitu flani badala yake huyo rafiki yake kamzidi akili, kafungua biashara alotaka kufungua mume wangu! Kiufupi amenidanganya na kunificha mambo mengi sana ambayo nikikumbuka naumia sana moyoni
sasa jana kuna baba kanipigia simu kuwa anamdai mume wangu hela ndefu tuu, na mume wangu kamwachia huyo baba atm kadi yake ili hela zikiingia akazitoe lakini kila akienda kutoa mwisho wa mwezi hakuti ata cent, akataka niilipe mimi nikamwambia siwezi.
Kiukweli mimi ndo nimebeba jukumu la kulea familia na kila kitu kinachohusu familia lakini mwenzangu hana habari na hajawahi kutoa matumizi yoyote
huwa najaribu kumwelekeza namna ya kuishi lakini ni kama nampigia mbuzi gitaa!
Sasa nahisi kuchanganyikiwa lakini sitaki kuchanganyikiwa naombeni ushauri wenu tafadhali!!
pole sana mdogo wangu.nikwambie kitu hawa wanaume kama sio wa kuijali familia unavyozidi kumuuliza na kumuomba matumizi ndo unazidi kumpa bichwa anakuwa kiburi zaidi.iwapo unajimudu tunza familia yako.anza kuwekeza taratibu.akikuona humfuatifuati kumuomba amini kuwa ataanza kujishtukia mwenyewe! ataanza kujikomba.tena ningekuwa mimi ndio wewe ningempikia vinono balaa senti siombi tabasamu full usoni.mwenyewe atabwaga manyanga ya ukorofi chini.ila usimlipie mkopo katu.labda kacheza dili na huyo mtu ajifanye anamdai ili wakuchune pesa vizuri.
Niambie ukweli unanipenda au unazingua!