Sitaki kuchanganyikiwa, naomba ushauri wenu wana MMU

Sitaki kuchanganyikiwa, naomba ushauri wenu wana MMU

Pole Sana. Ebu kaa nae kiutu uzima mzungumze na umbane kwa maswali mazito ila usimtaje huyo mzee tajwa. Kama ni mwelewa atakueleza kama si mwelewa bas mweleze juu ya Hilo deni.

Yote kwa yote ndoa Ina mambo mengi si kuzaa watoto tu. Pamoja na hayo, shikilia nafasi yako kama mwanamke shujaa ili uisimamie ndoa yako. Mwaka mmoja Bado sana.
 
sina idea na mambo ya ndoa

japo wanaume muda mwingine wana kama mapepo hivi.....wanafanya mambo yao wenyewe unalala nae,na kula nae lakini ungeweza kufungua kichwa chake na uone anayoyawaza walah UNGEMKIMBIA

they are just like that and that is it

ooooh PASUA KICHWA
 
Huu ni ukweli kabisa, Single anafanya ngono mpaka kero, hadi nimekonda!!

...na ndio maana ni nadra sana kumkuta mwanaume single amenenepa....mtanenepa saa ngapi wakati kutwa kucha mwashindana na mlikotoka.
 
Nikifikiria changamoto za ndoa kichwa kinaumaa
 
pole bibie. huyo alishaacha kuvaa nepi kwa hiyo kubadilika ni ngumu ila inawezekana. Kwamba hukuyaona wakati wa uchumba hayahusiki tena hapa kwa hiyo wa kubadilika ni wewe. Ujue namna utakavyotumia kipato chako kwa uangalifu. Na watu wenye tabia kama ya mumeo akimaliza kukopa kwa watu anahamia kwako, kwa hiyo kaa chonjo maana asipokushurutisha umpe hela atakuibia au ataweka rehani vitu vyenu. Huyo ni mwana anasa wala hakuna cha maana anachofanya na hizo hela.

Pia (samahani kwa hili)shemeji ni tapeli kidogo maana kitendo cha kukopa hela kwa mtu, na kumpa mtu atm card yake eti mshahara ukitoka awe anachukua kumbe kaenda kuhamishia mshahara kwenye akaunti nyingine ni utapeli tu hakuna jina lingine. Nikikwambia umfatilie zaidi ujue ana madeni kiasi gani na hela anapeleka wapi unaweza kuchanganyikiwa wakati we ushasema hutaki kuchanganyikiwa.

Kwamba ufanyeje, dah! mi hata sijui maana nina mtazamo hasi na ndoa ngumu. Mwanaume asiyeweza kutunza wa nyumbani kwake wa nini sasa! Hata Mungu hamwelewi mtu wa aina hii. Nikikwambia uende kwa mwaajiri wake upewe sehemu ya mshahara unaweza hata kunyimwa mgegedo ambao sijui kama hata kama unaufaidi maana wanawake tukiwa na kero moyoni hiyo kitu huwa haipandi.

Kwa vyovyote utakuwa umeshaongea nae sana kuhusu tabia yake. Sasa kilichobaki ni kumpa msimamo wako kuwa uko tayari kumsubiri kwa muda gani aweze kubadilika, na asipobadilika utafanya nini na umaanishe. Kama wasimamizi wako wa ndoa ni wenye hekima basi washirikishe kuhusu hilo tatizo, msimamo wako na deadline. Kama hutaweza basi we piga tu kimya, endelea kuwa single married mom walau mtoto amuone one baba. Au na nyumbani pia anarudi usiku sana? tehe..Zingatia ushauri ulopewa huko juu wa kuzingatia uzazi wa mpango na kujipanga kiuchumi wakati unashughulikia tatizo lako maana hii shughuli ndo ishakuhusu. Pole sana.
 
Pole dada,

Inaonyesha pengine kwa muda mrefu umekua mtu wa kumlaumu mumeo kwamba hajishughulishi au umekua ukitamani awe kama aina fulani ya wanaume unaopenda mambo yao ya maendeleo. Tabia hiyo ndio mnamfanya mwanaume atafute njia zake anazojua yeye afu afanye kitu kikubwa kuliko unachotaka wewe. Sasa huyo wa kwako inaonekana amefeli mpango wake.
Mi nakushauri mtafute. Mtamkie kwamba unamkubali kama alivyo. Na iwe kweli umemkubali. Sio wote wako sharp kwny kutafuta. Mjue wa kwako nenda nae kiaina, jitahidi kumsaidia udhaifu wake.
Kukimbia hakutakusaidia. Wala kulaumu na kutukana haitakusaidia.
Usitake afanane na watu fulani. Mwambie hayo pengine ataelewa. Afu mjipange kulipa ela za watu
 
sina idea na mambo ya ndoa

japo wanaume muda mwingine wana kama mapepo hivi.....wanafanya mambo yao wenyewe unalala nae,na kula nae lakini ungeweza kufungua kichwa chake na uone anayoyawaza walah UNGEMKIMBIA

they are just like that and that is it

ooooh PASUA KICHWA

Sio wanaume tu ata Sie wadada!! Ni akili ya mtu!
 
Pole dada,onyesha kuchukizwa na hyo tabia,coz unataka kujenga familia yenye kuheshmika na bora,iz must both of u,2be transparently in common, itasaidia kushauriana lip jema na baya,mkalishe mpe ukwel na mpe tme interval 4change,if not muitie his parents.
 
Jaribu kuhangaika. Nenda ata kwa waganga...... nadhan umenielewa
 
Mpotezee tu wewe lea familia! Otherwise unatafuta pressure! Muignore tu! Afanya atakavyo!

We Lara familia kwa huyu si baba, mama na mtoto? Kumuacha baba afanye atakavyo wakati mnaishi chini ya paa moja na mnalala kitanda kimoja huku we unagugumia na ugumu wa maisha peke yako kaa mjane ni tiketi tosha ya presha na maradhi mengine yatokanayo na stress. Hivi unamu-ignore vipi mtu mtu analalia mashuka uliyogharamia usafi wewe, anakula chakula ulichonunua wewe, anavaa nguo ulizogharamia usafi na luku, anajiita baba nanii wakati hajui unakula nini ili nanii anyonye akue??!. Huyu shemeji asingekuwa na kazi mi ningemwambia huyu dada amtunze mumewe kwa heshima na mapendo kabisa. Lakini mtu ana kazi??? Na bado anakopa?? Aisee atanieleza! Yaani nitoke huko nilikotoka niishie kwenye tabu in the name of ndoa? Wapi!? Hapo inakuwa ni moja kati ya mawili tu: ashiriki kutunza familia au kuvunja mkataba. Ndoa si kuambatana? au? Tcha!
 
1. wewe ndoa wewe mbona unaumiza watu vichwa?
2. Back to the topic kwa uelewa wangu mdogo sidhani kama ni jambo la busara wanandoa kufichana vitu,inabidi kuambiana kila kitu,kusikia jambo nje kwa mara ya kwanza lazima likuchanganye,anachofanya mumeo si kitu kizuri hata kidogo.
3. Tafuta wazee wa ukoo mkae mliongelee vizuri,pole sana.
 
...na ndio maana ni nadra sana kumkuta mwanaume single amenenepa....mtanenepa saa ngapi wakati kutwa kucha mwashindana na mlikotoka.
Ukiniona mkuu nilivyoisha utanihurumia, watu wanajiuliza, huyu jamaa ana kazi inayolipa vizuri mbona hatakati?
Kumbe mwenzao kila nikivuta kumbukumbu ni siku gani sijafanya mapenzi sikumbukuki, yaani ni daily!!
 
pole bibie. huyo alishaacha kuvaa nepi kwa hiyo kubadilika ni ngumu ila inawezekana. Kwamba hukuyaona wakati wa uchumba hayahusiki tena hapa kwa hiyo wa kubadilika ni wewe. Ujue namna utakavyotumia kipato chako kwa uangalifu. Na watu wenye tabia kama ya mumeo akimaliza kukopa kwa watu anahamia kwako, kwa hiyo kaa chonjo maana asipokushurutisha umpe hela atakuibia au ataweka rehani vitu vyenu. Huyo ni mwana anasa wala hakuna cha maana anachofanya na hizo hela.

Pia (samahani kwa hili)shemeji ni tapeli kidogo maana kitendo cha kukopa hela kwa mtu, na kumpa mtu atm card yake eti mshahara ukitoka awe anachukua kumbe kaenda kuhamishia mshahara kwenye akaunti nyingine ni utapeli tu hakuna jina lingine. Nikikwambia umfatilie zaidi ujue ana madeni kiasi gani na hela anapeleka wapi unaweza kuchanganyikiwa wakati we ushasema hutaki kuchanganyikiwa.

Kwamba ufanyeje, dah! mi hata sijui maana nina mtazamo hasi na ndoa ngumu. Mwanaume asiyeweza kutunza wa nyumbani kwake wa nini sasa! Hata Mungu hamwelewi mtu wa aina hii. Nikikwambia uende kwa mwaajiri wake upewe sehemu ya mshahara unaweza hata kunyimwa mgegedo ambao sijui kama hata kama unaufaidi maana wanawake tukiwa na kero moyoni hiyo kitu huwa haipandi.

Kwa vyovyote utakuwa umeshaongea nae sana kuhusu tabia yake. Sasa kilichobaki ni kumpa msimamo wako kuwa uko tayari kumsubiri kwa muda gani aweze kubadilika, na asipobadilika utafanya nini na umaanishe. Kama wasimamizi wako wa ndoa ni wenye hekima basi washirikishe kuhusu hilo tatizo, msimamo wako na deadline. Kama hutaweza basi we piga tu kimya, endelea kuwa single married mom walau mtoto amuone one baba. Au na nyumbani pia anarudi usiku sana? tehe..Zingatia ushauri ulopewa huko juu wa kuzingatia uzazi wa mpango na kujipanga kiuchumi wakati unashughulikia tatizo lako maana hii shughuli ndo ishakuhusu. Pole sana.

Umeongea ukweli, kuishi na mwanme wa spirit hii ya ufujaji kunaleta sana umaskini hapo ajipange kuanza upya

Kutokuwa na hekima na busara bado atahitaji heshima km mume,:what:::what:
 
Back
Top Bottom