Sitaki kuchanganyikiwa, naomba ushauri wenu wana MMU

Sitaki kuchanganyikiwa, naomba ushauri wenu wana MMU

Lolipop

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2013
Posts
349
Reaction score
81
Natumaini mu wazima, ni mwaka 1 sasa toka tumefunga ndoa na mwenza wangu na tumejaliwa mtoto mmoja.

Na sote ni wafanyakazi, tatizo huyu mume wangu hanishirikishi katika kila analolifanya, mfano aliwahi kuchukua mkopo bila mimi kujua lakini hakufanyia kitu chochote, alijipangia bussines plan mwenyewe na kumweleza rafiki yake kuwa anataka kufanya kitu flani badala yake huyo rafiki yake kamzidi akili, kafungua biashara aliyotaka kufungua mume wangu.

Kiufupi amenidanganya na kunificha mambo mengi sana ambayo nikikumbuka naumia sana moyoni sasa jana kuna baba kanipigia simu kuwa anamdai mume wangu hela ndefu tuu, na mume wangu kamwachia huyo baba ATM Card yake ili hela zikiingia akazitoe lakini kila akienda kutoa mwisho wa mwezi hakuti hata cent, akataka niilipe mimi nikamwambia siwezi.

Kiukweli mimi ndo nimebeba jukumu la kulea familia na kila kitu kinachohusu familia lakini mwenzangu hana habari na hajawahi kutoa matumizi yoyote
huwa najaribu kumwelekeza namna ya kuishi lakini ni kama nampigia mbuzi gitaa.

Sasa nahisi kuchanganyikiwa lakini sitaki kuchanganyikiwa naombeni ushauri wenu tafadhali.



 
hebu kuna kitu hujagusia kwan mnaishi wote au tofauti na unaposema hajishughulishi na familia una maana matumizi yote unatoa wewe!!!
na kama unao uwezo basi shusha windows7 weka windows 8 yaan mpige chini.....!!!!
 
Nilichepuka naye ni mke was Ntuzu.
Sijaweka herufi....@,... halafu jifanye unaweka kumention...humu hamna hiyo

Mshaanza kuharibu uelekeo wa mada. Wakati mwingine muwe mnafikiri. Kama mnataka chat nenden chit chat. Huyo mdada ana shida na anaomba mawazo hajaomba chat,kama huna wazo unaskip.
 
Last edited by a moderator:
Mshaanza kuharibu uelekeo wa mada. Wakati mwingine muwe mnafikiri. Kama mnataka chat nenden chit chat. Huyo mdada ana shida na anaomba mawazo hajaomba chat,kama huna wazo unaskip.

Mbona povu mkuu we ndo Mme?
 
hebu kuna kitu hujagusia kwan mnaishi wote au tofauti na unaposema hajishughulishi na familia una maana matumizi yote unatoa wewe!!!
na kama unao uwezo basi shusha windows7 weka windows 8 yaan mpige chini.....!!!!
Umenichekesha sana,eti shusha window7 weka window 8 haaaaaa sijui ataufanyia kazi
 
Mna mwaka mmoja tu yameshaanza hayo?!
Kinachoonekana hamkuchukua muda wa kutosha kusomana tabia, na kumbadilisha mtu tabia huwa sio sio kazi rahisi,

Now, you are in for it, kuvunja ndoa sio suluhu, inabidi ukomae tu, jaribu kukaa nae, tumia watu unaowaamini n.k
 
Nafikiri umuulize kwanza pesa hizo kapeleka wapi kabla ya kuanza kupata presha pengine kafanyia tuu kitu cha maana.
 
mwallu Viol nshafika sasa ata km hamjaniita! Aya niambieni?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom