Sitaisahau CHRISTMAS ya mwaka 1997

Sitaisahau CHRISTMAS ya mwaka 1997

kingunge wa jf

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2013
Posts
466
Reaction score
467
Basi ilikuwa trh 24 siku 1 kabla Christmas kama kawaida maza na mshua wakaniambia twende mjini kununua nguo. Basi nikajiandaa fasta huku akili yangu ikijua lazima kile kiatu ninunue.
Basi tukazunguka duka la kwanza la pili mpk karibia maduka yote. Si unajua tena pale wilaya kipindi kile ni sawa tu na kijijini.
Shauku yangu kubwa ili Christmas itimie lazima nivae *MOKA* ndo kiatu kilichokuwa kwenye chati. Hili pia lilichangiwa na kuona mtoto wa tajiri mmoja pale kijijini kanunuliwa MOKA huku mzee na ndo vile alikuwa hataki mtu akatize mbele kizembekizembe. Lakini km kawaida yetu wasukuma sare sare ndo maisha yetu ya kila siku.
Tukaendelea na kusaka viatu vile, Mara paaap! Tukaingia duka la Mangi mmoja hivi. Jamani Tuwaache wachaga wawe tu mbele kwa sabb wameanza kufight kitambo, kujilinganisha na hawa watu ni sawa na kulinganisha Tanzania na Marekani. Kama Tanzania ingekuwa na wachaga wote basi tungekuwa sawa na Angalau South Africa kabisa
Tulipoingia tukaona MOKA nyeusi nzuri ngozi ngozi kweli! Sio za siku hizi mara pale ngozi huku carpet mchanganyiko km rangi ya Mkwele aliyejichubua.
Nikajaribishia ile MOKA lakn ilikuwa kubwa. Wakagoma kununua lkn mie nkalazimisha huku nikilia.
Basi mshua akasema tuendelee kutafta ili wanitoe pale dukani. Tulitafta kila sehemu lkn hatukupata wakaniambia ninunue viatu vingine... nikagoma. Duuuh maza akavimba! Akataka anishushie kipigo pale pale. Lkn mzee kamzuia.
Kumbuka tumefika mjini saa 3 mpk saa 10 sasa tunatafta kiatu changu. Basi ikabidi wamenitema. Wakaanza kufanya yao. Badae maza akasema 'atavaa vya zamani'. Hapo ndio mambo yote yaliharibika. Heeee! Nilijawa na hasira nkalia kwa nguvu badae wakanibembeleza nkanyamaza.
Badae nikaona mzee anachukua pikipiki tukapanda kurudi home aisee nilianza kulia njia nzima hakuna aliyenijali. Nafika home nashuka kwny pikipiki nalia tu.
Mzee alipo park pikipiki yake, maza alipoingia ndani kurudi. Baada ya Dakika 3 sikujua nilifikaje kwa jirani huku nikiwa na manundu kila sehemu afu kesho Christmas.
Basi usiku wakanifata kumbe mzee alikrudia ile MOKA kwa Mangi.
Wakaniambia nijaribishe nikavaa suti yangu na ile MOKA huku MOKA inanizidi mbali sn.
Basi kesho yake kwenda kanisani huku usoni manundu na domo limevimbaa, dada zangu na majirani wananicheka, huku MOKA kubwa nashindwa kutembea. Daaah! Basi Christmas ile ilikuwa tabu sana kwangu.
Watu walinijua kwa kupiga viwalo pale kijijini lkn siku ile pamoja na kuwa vitu vilikuwa bei kubwa lkn kiatu over size na manundu juu. Safari hii Nilikula sikukuu ile nikiwa mnyonge na mwenye kutengwa na jamii.

Je, ipi ilikuwa sikukuu mbaya kwako au nzr?
 
Mara nyingi kila ikifika mwisho wa mwaka nilikua nawakomalia wazee niende kwa babu na bibi,nakumbuka nguo na viatu vya Christmass mara zote vilitumwa nikiwa niko mkoani tayari ingawa mara zote nilikua nawapa machaguo yangu duh sasa nikachagua suti nyeupe na moka moja matata sana alafu nikasepa kwa babu balaa likaja siku zinaenda na mzigo wangu wa kuwakomesha watoto wenzangu haufiki na miaka ile hakuna simu (za mkononi) mawasiliano ni barua tu nikawa najipa moyo tu kuja kushtuka sikukuu imefika pekee angu sina nguo mpya na wenzangu walinicheka kinoma maana nilitamba sana hasa kila nikiona famba zao nikijua zangu zitafunika[emoji23][emoji23] kama ingekua kuna laana ya mtoto basi wazazi wangu siku wangegeuka machizi maana nililia na sikutoka ndani kwa siku mbili nakumbuka tarehe 3 ya mwaka mpya ndio kondakta wa bus anakuja kwa babu na vitu vyangu eti alipewa kitambo ila alipata matatizo
 
Sitasahau Christmas ya mwaka 2016. Nikiwa na rafiki yangu asubuhi kunakucha hatuna hili wala lile tunajipa moyo na kusogea gengeni kulikuwa na mama mmoja alikuwa anatuuzia mboga, ndani tulikuwa na mia 3 ila unga tulikuwa nao tatizo kubwa lilikuwa ni mboga, safari ya kwenda gengeni ikaanza taratibu huku tukiwa na matumaini ya kumkuta mama dah! Kufika tunakuta wapo tu wauza nyanya hapo tuna njaa ya ya siku moja maana usiku hatukula, ikabidi tupumzike pale gengeni tukawa tunasubiri labda mama angekuja atupatie mboga ila wapi.

Dakika chache nikamuona mpenzi wangu na rafiki yake wanatoka salon kutengeneza nywele, alishangaa mimi kuwa pale akauliza vipi huko kwenu sikukuu vipi nikamwambia poa tu hapa tumekuja kuchukua nyanya tukapike karibuni wakasema asante. Nikamuuliza wapi mbona mmetoka salon akasema tunajiandaa kutoka (nikajua tayari naenda kugongewa) nikamwambia kila la kheri uwe makini wakaanza safari ya kwenda huko kwenye mtoko wao.

Basi jamaa yangu akaniambia twende kwa shangazi yupo hapa mjini najua tutakula na kurudi home tukiwa vizuri bhana safari ya kwenda kwa shangazi ikaanza wakati huo nilikuwa nina jipu kwenye paja yaani maumivu ya jipu njaa na hela hakuna nilikuwa naona kama maisha yanatutania sana, basi tukafika kwa shangazi tulikuta kuna foleni ya watu maana wengi walikuja pale pia kujumuika nao hvyo msosi wetu ukawa haupo kwenye mahesabu wakaugawanya gawanya hatimaye na sisi tukapata kidogo tukala na jioni tukarudi nyumbani.

Ile tunafika tukakuta majirani wanapika pilau kuku aisee nikaingia ndani nikamwambia mshikaji mimi nalala (tulikuwa vyumba tofauti) kabla sijasinzia akaja kugonga mlango akaniomba sufuria kubwa nikampa baada ya muda akaja na pilau limejaa sufuria likiwa na nyama aisee tulikula siku 2 pilau haliishi hadi tukamwaga.

Siku hiyo niliamini Mungu ndiye anajua nini utakula hata kama huna pesa. MUNGU ATUFANIKISHE SANA.
 
Mara nyingi kila ikifika mwisho wa mwaka nilikua nawakomalia wazee niende kwa babu na bibi,nakumbuka nguo na viatu vya Christmass mara zote vilitumwa nikiwa niko mkoani tayari ingawa mara zote nilikua nawapa machaguo yangu duh sasa nikachagua suti nyeupe na moka moja matata sana alafu nikasepa kwa babu balaa likaja siku zinaenda na mzigo wangu wa kuwakomesha watoto wenzangu haufiki na miaka ile hakuna simu (za mkononi) mawasiliano ni barua tu nikawa najipa moyo tu kuja kushtuka sikukuu imefika pekee angu sina nguo mpya na wenzangu walinicheka kinoma maana nilitamba sana hasa kila nikiona famba zao nikijua zangu zitafunika[emoji23][emoji23] kama ingekua kuna laana ya mtoto basi wazazi wangu siku wangegeuka machizi maana nililia na sikutoka ndani kwa siku mbili nakumbuka tarehe 3 ya mwaka mpya ndio kondakta wa bus anakuja kwa babu na vitu vyangu eti alipewa kitambo ila alipata matatizo
Daaah huyo alikuwa wakuroga kabisa haahhaaaaaaa
 
Mi nakumbuka 1999 nilikua a town tukaenda na maza na mzee tunaingia duka moja mzee alishatupiga biti kila mtu bajet yake ya kila kitu ni elfu 50000 yaani hapo ni shati suruali sox na viatu, ila baada ya kununuliwa kila kitu kasoro viatu bajet yangu ikiwa imebaki elfu 12 tukaingia kwenye duka la mhindi mmoja nikaona kiatu kikali kujaribu mpaka mwisho, mhindi kataja bei Laki mwisho elfu 80 mimi nang'angania kidogo kaingia jamaa wanafanya kazi na mzee kamwambia bro acha ubahili mpe kijana kiatu elfu 80 unalia nini akampa mzee 15 ongezea hapo, ikabd mzee kwa shngo upande anunue, mi kwangu ushindi ila njiani 2ko kwenye gari tunarudi home nilikula masingi na misonyo... Ile kufika hme tukakuta kuna wageni wamekuja toka dar wako kibarazani Basi tukaanza kutoa vitu tukijaribisha kila mtu na vyake mara si mbwa wetu mmoja kapita na kiatu changu kimoja kumkimbiza akapita geti la nyuma kuna shamba huko kuja kumkuta anakirarua kiatu hakifai narudi nalia nimeshika kiatu kimekuwa tambara mzee alicheka sana sana akasema usijali utavaa kilchobaki sitasahau xmas hiyo sikutoka ndani
 
Haa haaa haaa wakuu, poleni Duuuuuuh.
 
Nilichojifunza hapa,ni kwamba kuna wa2 tumepitia maisha ya kuungaunga mpaka tumefika hapa tulipo...,magari,majumba na Mali nyingine nyingi zinatufichia Mapito yetu mabaya
Pia,Mungu anapaswa kutukuzwa kwa hali yoyote!
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Mimi nikizunguka nawewe nusu saa mjiini unachagua chagua bila kununua sinaga uvumilivi, nakuuliza unachitaka na bei unaenda mwenyewe au na mtu mwingine, huwa sina uvumilivu kuzungukia maduka ...huyo mshua 100% kama wangu (RIP) angekutia mabanzi hukohuko kila mtu anarudi kivyake...mpaka wanakuuliza , " ivi huyo ni baba yako kweli?[emoji3]
 
Mi nakumbuka 1999 nilikua a town tukaenda na maza na mzee tunaingia duka moja mzee alishatupiga biti kila mtu bajet yake ya kila kitu ni elfu 50000 yaani hapo ni shati suruali sox na viatu, ila baada ya kununuliwa kila kitu kasoro viatu bajet yangu ikiwa imebaki elfu 12 tukaingia kwenye duka la mhindi mmoja nikaona kiatu kikali kujaribu mpaka mwisho, mhindi kataja bei Laki mwisho elfu 80 mimi nang'angania kidogo kaingia jamaa wanafanya kazi na mzee kamwambia bro acha ubahili mpe kijana kiatu elfu 80 unalia nini akampa mzee 15 ongezea hapo, ikabd mzee kwa shngo upande anunue, mi kwangu ushindi ila njiani 2ko kwenye gari tunarudi home nilikula masingi na misonyo... Ile kufika hme tukakuta kuna wageni wamekuja toka dar wako kibarazani Basi tukaanza kutoa vitu tukijaribisha kila mtu na vyake mara si mbwa wetu mmoja kapita na kiatu changu kimoja kumkimbiza akapita geti la nyuma kuna shamba huko kuja kumkuta anakirarua kiatu hakifai narudi nalia nimeshika kiatu kimekuwa tambara mzee alicheka sana sana akasema usijali utavaa kilchobaki sitasahau xmas hiyo sikutoka ndani
Duhh....50,000 ya mwaka 1999 kwa sasa ni 500,000....SIKU HAZIGANDI
 
1982 nimeuza mpunga wangu tukabebana na wife hao mpaka mjini kila mtu akachagua vyake nikanunua zangu raizon ngazi 3 safi kabisa tukarudi nyumbani nikaziweka uvunguni mwa kitanda siku ya sikukuu ilitakiwa tuanzie kwa babu tafuta viatu sivioni namuuliza wife hajui niliishiwa pozi ikabidi niende kwanza mtoni wakati nateremka nyumba ya jirani namuona jirani anajaribishia raizon ile ile yangu na mfuko uleule niliokuwa nimebebea aisee nilirudi nduki mpaka kwangu zama ndani beba jambia nikarudi kwa jirani ile natokezea tu jirani akaanza kupiga mayowe jirani usiniue chukua viatu vyako niliiba kwa kupitia dirishani nisamehe mshenzi sana alitaka kuniharibia siku
 
Duuuuh hahaaaaa aiseee mngekipika kile kilichoharibika
 
Nilipoaminiwa kupika pilau siku ya Christmas nilijiona princess. Tena niliambiwa niende miss ya kwanza ili niwahi kuanza kupika. Mama alipika vingi usiku lakini pilau na salad niliandaa.

Wageni walipokuwa wanakula nilitamani niwaambie Mimi ndiye mpishi wa pilau, lakini credits zote zilikwenda kwa mother house.
 
1982 nimeuza mpunga wangu tukabebana na wife hao mpaka mjini kila mtu akachagua vyake nikanunua zangu raizon ngazi 3 safi kabisa tukarudi nyumbani nikaziweka uvunguni mwa kitanda siku ya sikukuu ilitakiwa tuanzie kwa babu tafuta viatu sivioni namuuliza wife hajui niliishiwa pozi ikabidi niende kwanza mtoni wakati nateremka nyumba ya jirani namuona jirani anajaribishia raizon ile ile yangu na mfuko uleule niliokuwa nimebebea aisee nilirudi nduki mpaka kwangu zama ndani beba jambia nikarudi kwa jirani ile natokezea tu jirani akaanza kupiga mayowe jirani usiniue chukua viatu vyako niliiba kwa kupitia dirishani nisamehe mshenzi sana alitaka kuniharibia siku
Shikamôo mzee wetu
 
Nilichojifunza hapa,ni kwamba kuna wa2 tumepitia maisha ya kuungaunga mpaka tumefika hapa tulipo...,magari,majumba na Mali nyingine nyingi zinatufichia Mapito yetu mabaya
Pia,Mungu anapaswa kutukuzwa kwa hali yoyote!
Kweli Aisee
 
1982 nimeuza mpunga wangu tukabebana na wife hao mpaka mjini kila mtu akachagua vyake nikanunua zangu raizon ngazi 3 safi kabisa tukarudi nyumbani nikaziweka uvunguni mwa kitanda siku ya sikukuu ilitakiwa tuanzie kwa babu tafuta viatu sivioni namuuliza wife hajui niliishiwa pozi ikabidi niende kwanza mtoni wakati nateremka nyumba ya jirani namuona jirani anajaribishia raizon ile ile yangu na mfuko uleule niliokuwa nimebebea aisee nilirudi nduki mpaka kwangu zama ndani beba jambia nikarudi kwa jirani ile natokezea tu jirani akaanza kupiga mayowe jirani usiniue chukua viatu vyako niliiba kwa kupitia dirishani nisamehe mshenzi sana alitaka kuniharibia siku
Hahahaaaaa 1982????
 
Basi ilikuwa trh 24 siku 1 kabla Christmas kama kawaida maza na mshua wakaniambia twende mjini kununua nguo. Basi nikajiandaa fasta huku akili yangu ikijua lazima kile kiatu ninunue.
Basi tukazunguka duka la kwanza la pili mpk karibia maduka yote. Si unajua tena pale wilaya kipindi kile ni sawa tu na kijijini.
Shauku yangu kubwa ili Christmas itimie lazima nivae *MOKA* ndo kiatu kilichokuwa kwenye chati. Hili pia lilichangiwa na kuona mtoto wa tajiri mmoja pale kijijini kanunuliwa MOKA huku mzee na ndo vile alikuwa hataki mtu akatize mbele kizembekizembe. Lakini km kawaida yetu wasukuma sare sare ndo maisha yetu ya kila siku.
Tukaendelea na kusaka viatu vile, Mara paaap! Tukaingia duka la Mangi mmoja hivi. Jamani Tuwaache wachaga wawe tu mbele kwa sabb wameanza kufight kitambo, kujilinganisha na hawa watu ni sawa na kulinganisha Tanzania na Marekani. Kama Tanzania ingekuwa na wachaga wote basi tungekuwa sawa na Angalau South Africa kabisa
Tulipoingia tukaona MOKA nyeusi nzuri ngozi ngozi kweli! Sio za siku hizi mara pale ngozi huku carpet mchanganyiko km rangi ya Mkwele aliyejichubua.
Nikajaribishia ile MOKA lakn ilikuwa kubwa. Wakagoma kununua lkn mie nkalazimisha huku nikilia.
Basi mshua akasema tuendelee kutafta ili wanitoe pale dukani. Tulitafta kila sehemu lkn hatukupata wakaniambia ninunue viatu vingine... nikagoma. Duuuh maza akavimba! Akataka anishushie kipigo pale pale. Lkn mzee kamzuia.
Kumbuka tumefika mjini saa 3 mpk saa 10 sasa tunatafta kiatu changu. Basi ikabidi wamenitema. Wakaanza kufanya yao. Badae maza akasema 'atavaa vya zamani'. Hapo ndio mambo yote yaliharibika. Heeee! Nilijawa na hasira nkalia kwa nguvu badae wakanibembeleza nkanyamaza.
Badae nikaona mzee anachukua pikipiki tukapanda kurudi home aisee nilianza kulia njia nzima hakuna aliyenijali. Nafika home nashuka kwny pikipiki nalia tu.
Mzee alipo park pikipiki yake, maza alipoingia ndani kurudi. Baada ya Dakika 3 sikujua nilifikaje kwa jirani huku nikiwa na manundu kila sehemu afu kesho Christmas.
Basi usiku wakanifata kumbe mzee alikrudia ile MOKA kwa Mangi.
Wakaniambia nijaribishe nikavaa suti yangu na ile MOKA huku MOKA inanizidi mbali sn.
Basi kesho yake kwenda kanisani huku usoni manundu na domo limevimbaa, dada zangu na majirani wananicheka, huku MOKA kubwa nashindwa kutembea. Daaah! Basi Christmas ile ilikuwa tabu sana kwangu.
Watu walinijua kwa kupiga viwalo pale kijijini lkn siku ile pamoja na kuwa vitu vilikuwa bei kubwa lkn kiatu over size na manundu juu. Safari hii Nilikula sikukuu ile nikiwa mnyonge na mwenye kutengwa na jamii.

Je, ipi ilikuwa sikukuu mbaya kwako au nzr?
Dah nimecheka sana. Dah aisee Jf oyeee
 
Back
Top Bottom