Sisi Vijana wa CCM tumebaki wakiwa

Nov 18, 2020
81
125
Ilizoeleka tukiwajibu wapinzani ndo tunaonekana zaidi, pia wakati wa uchaguzi tumefanya kampeni kuwapigania wagombea wetu wapite kwa kishindo.Walipita kwa kishindo.

Lakini sasa hali imekuwa ngumu hakuna wa kumjibu wapinzani wamejifanya kukaaa kimya kama Nchi siyo Ya kwao. Hata ile buku saba hapa lumumba imekata.

Ajira za chama zimekata pia, tulizoea kila mwaka sisi vijana makada watiifu kutuma vyeti vyetu kupangiwa kazi afisa tarafa, utendaji wa kijiji, na wale waliosomea msmbo ya uandisi walipangiwa kufanya kazi katika wizara husika. Mimi nilitegea kwa sababau nilitaka kuwa DED, DAS, RAC, DC au RC.

Sasa vyote nimevikosa nimebaki na piga miayo. Wapinzani jamani liamsheni dude ili nasi vijana tuwajibu kwa maneno ili tupate mkate wa kila siku.

Wanajamvi msinichukie hali ni mbaya huku ground, nawasilisha.
 

Bengal

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
2,221
2,000
Kama yakweli pole, ila kama janja janja iliyotufikisha hapa kwa ajili ya uzalendo maslahi, basi nasema safi sana, ili wakati ujao mbongo zifanye kazi na sii kukabidhi akili pale getini ili tupate mlo wa siku.
 

mwanateknolojia

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
813
1,000
CCM imara inategemea UPINZANI imara! Kipindi wapinzani wakiwa imara sana kipindi hicho katibu mwenezi akiwa Nape Nnauye, Ccm ilifanya harakati na amsha amsha kila sehemu. Bodaboda walipakiliwa mafuta, vijana mikoa mbalimbali walilishwa na kulipwa posho, maisha yalikuwa fresh!

Vijana wakasahau kuwa hawa uwepo wa wapinzani ndio unaofanya maisha yao yabebwe na mambo yaonekane mepesi, haohao vijana wakatumika kufanya kila lililofanywa na CCM kuhakikisha upinzani unafutwa kwenye ramani ya uongozi wa nchi yetu, hivyo wakabaki kuwasakama na kuwasingizia wapinzani kila aina ya ushetani wa kisiasa, na mwishowe wakakoroga uchaguzi na hatimaye upinzani ukalazimishwa ukubali kushindwa hata pale waliposhinda, Sasa mmelikoroga wenyewe linyweni!
 

Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
1,084
2,000
Ilizoeleka tukiwajibu wapinzani ndo tunaonekana zaidi, pia wakati wa uchaguzi tumefanya kampeni kuwapigania wagombea wetu wapite kwa kishindo.Walipita kwa kishindo....
Nyie ndo mlisaidia kubeba kura za wizi wakati wa Uchafuzi na huko nyuma ndo mlikuwa "wasiojulikana" sasa mnaanza kujulikana baada ya kuona hamuwezi kuwamaliza Wapinzani na kugundua kumbe ndio binadamu. Mtajiju, wageuzieni kibao mashetani wa CCM!
 

Zawadini

JF-Expert Member
Feb 2, 2012
1,452
2,000
Angalau umeuchangamsha ukumbi. Ulikuwa umedorora tangu ule USHINDI WA KISHINDO. By the way; mchuma janga hula na wa kwao. Huenda siku nyingine tutafikiri kabla ya kutenda. Ubarikiwe sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom