jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Baada ya kuandika jinsi tabia ya uchakachuaji na uongo ya CCM inavyoendelea kuligharimu taifa. Nimeona pia ccm wakiendeleza siasa zao za migawanyiko(politics of division). Ile mbinu ya mkoloni ya “divide and rule”, wameiadapt kwa umahiri wa hali ya juu kabisa!
Kama ilivyo kwa uongo wao na propaganda, politics of division ni hatari zaidi wakati tunakabiliana na janga hili la corona.
Mbaya zaidi, kwasababu siasa zao ni zile za abracadabra, “now you see it, now you don’t “, ambapo wameachiwa wazitumie nyakati hizi zinazohitaji wataalam kwenye kufanya maamuzi, kutoa taarifa nk. Wao ndo waliotakiwa kuwa msitari wa mbele na wakati wa utoaji wa taarifa, wanakuwa bega kwa bega na viongozi wao, ili kwamba maswali yoyote muhimu yatakayojitokeza, yapatiwe majibu pasina “bureacracy”. Hawa wangetutolea majibu sahihi kabla ya uamuzi wa kupima papai, kondoo, mbuzi na kupima oil.😏
Kuanza kuwabagua wale viongozi walioamuwa kuchukuwa hatua za kujilockdown kwa siku 14 baada ya baadhi ya wabunge wenzao kudhurika, ni siasa hatarishi kwa taifa letu. Siasa zinazoleta chuki na migawanyiko, ni siasa za ccm. Sisi sote ni ndugu tunaotakiwa kuwa pamoja kama Taifa kwenye vita hivi.
Kitendo cha kusema wanaopoteza maisha yao ni kwasababu ya “changamoto ya upumuaji”, imenisikitisha sana, na ikanikumbusha kauli za uongo uongo za ki ccm, mfano “kitu chenye ncha kali”, badala ya kusema risasi, “watu wasiojulikana”, badala ya kusema ni watu wa usalama...watu ambao polisi haiwezi kuthubutu kuwafuatilia. “Maagizo kutoka juu” nk
Kitendo cha katibu Mwenezi Pole pole kudai chadema ni kama covid-19, kinaondoa ule udugu wetu, na kuonyesha tabia ya ccm ya uongo uongo, uzandiki, na kutokuwa serious na Taifa hili. Maana wamedekezwa na kodi zetu toka uhuru. Na kulindwa na dola hivyo kujisahau.
Kitendo cha ccm kusema watatoa barakoa kwa wanachama wao peke yake pia kinaonyesha uwepo wa matabaka kwenye taifa letu yaliyoasisiwa na ccm.
Ni wazi kwamba tukiiweka ccm pembeni kidogo tutapiga hatua, na wao watajipanga watakapokosa na kutambuwa kwamba uongozi ni dhamana na wala siyo fursa. Watajirekebisha, kuleta ushindani wa kweli kwa kujituma na kujifikirisha. Bila ya kuona kana kwamba nchi inatawaliwa na tabaka moja na mawazo ya kiimla.
Hata hili suala la uchunguzi wa vipimo vya corona, lingefanyika kwa siri pasina kutangaza mbinu, kusingeongeza mkanganyiko ambao unaweza kupelekea upuuzwaji ama uzembe kwa wananchi wa kawaida wasio na uelewa mkubwa kutokana na uongozi mbovu wa ccm toka uhuru.
kauli hii ni courtesy of chriss Lukosi