Hapa mwisho umekengeuka.
Lakini nimekusoma hadi mwisho na yafuatayo ndio maoni yangu.
CCM kama chama kusema kweli haipo sasa hivi, kilichopo ni jina la chama na kundi la watu wanaojiita wanachama wa chama hicho kutokana na maslahi binafsi wanayoyapata kwa kuwa katika kundi hilo.
CCM, kama ilivyo sasa nchi yetu Tanzania, ni mateka wa mtu mmoja aliyechaguliwa na wananchi (sijui uhalali wa uchaguzi huo, lakini kiongozi huyo alipewa uhalali huo baada ya yote yaliyofanyika kumkabidhi madaraka.
Baada ya kupewa madaraka kwa hatua zote zilizopaswa kufanyika, huyu mtu akajimilikisha vyombo vyote vya kimadaraka ili vyombo hivyo vitimize matakwa yake, na sio matakwa ya wananchi. Ndio maana nasema kapata mateka, hata sisi raia na CCM iliyomweka hapo ni mateka wake kwa kutumia nguvu za vyombo alivyokabidhiwa ili vimsaidie kutufanyia kazi.
CCM hawana uwezo juu yake, kama sisi wananchi tusivyokuwa na uwezo juu yake kwa wakati huu.
CCM chini ya Kikwete ilikuwa imeoza, lakini bado ilikuwa na muundo wake wa tokea zamami enzi za Mwalimu; kwa hiyo ingeweza kubadilika kama ingempata kiongozi aliyekuwa hataki ubovu aliouvumilia Kikwete.. Lakini aliyechukua akaona autumie ubovu huo kujimilikisha jina la chama. Chama chenyewe hasa hakipo. CCM ni Mwenyekiti wake sasa hivi
Kama huamini, kawaulize Kinana na akina Nnauye, Makamba na wengineo wakitaka kukueleza watakupa ukweli.
Kwa hiyo, hayo yote uliyoyaandika kwenye mada yako hapo juu, ya kufarakanisha na mengineyo, haya yameshamiri zaidi kwa sababu ndio tabia ya mwenye chama.
Hila nyingi zidi ya wapinzani, nieleza, pamoja na kwamba zilikuwepo chini ya Kikwete, lakini hazikufika huku tulikofika sasa hivi chini ya mwenye chama.
Mabeberu wamekuwa marafiki wa wapinzani, kwa hiyo maadui wa waTanzania, hiki ni kibwagizo kinachopendwa sana kutumiwa wakati huu
Ngoja nisikuchoshe sana kwa kumaliza na yafuatayo.
Udhaifu mkubwa unaoonyeshwa na wapinzani wote sasa hivi ni kushindwa kwao kueleza kwa wananchi hii tabia mpya, mbaya kabisa ya kuligawa taifa letu katika makundi mbalimbali.
Wapinzani wameshindwa kabisa kujenga hoja juu ya jambo hili na wakalipeleka kwa wananchi kulieleza ili wananchi walielewe vizuri.
Kazi hii haiwezi kuwa ngumu, kwa sababu huko nyuma umoja wetu ulijulikana duniani na ndiyo iliyokuwa nguvu yetu pamoja na umaskini wetu wa mali.
Hapa wapinzani wanatakiwa wachambue kwa kina kabisa matendo yote, tena yapo mengi mno yaliyofanywa na mwenye chama ambayo yanafanywa kwa maksudi kwa kutugawa waTanzania. ili azidi kututawala kwa raha zake.