Sisi ndio wanaume bwana!

Sisi ndio wanaume bwana!

Habari zenu waungwana.....

Huu ni waraka kwa vijana/wavulana wanaokaribia kuwa WANAUME. Kuwa MWANAUME si mchezo na si lelemama. Ushawahi kusikia Chama cha Wanaume, Umoja wa Wanaume, Umoja wa Wanasheria Wanaume, Umoja wa Madaktari wanaume etc?........ Hii inamaanisha MWANAUME ni Taasisi inayojitegemea.
Mwanaume kamili aliyekamilika si kama yule aliyozungumzia Bishanga kwenye sredi yake (kwa makusudi siweki link yake hapa)
Ili uwe MWANAUME yakupasa kwanza kabisa kumshukuru Mungu kwa kuumbwa jinsia ya kiume. Umepewa upendeleo lazima ushukuru. Halafu:

1. Uwe RIJALI na MMILIKI (hili halihitaji ufafanuzi) Ukishakuwa rijali unapaswa uwe na UMILIKI. Umiliki wa mwanaume rijali ni umiliki wa MWANAMKE/WANAWAKE. Iwe rasmi au vinginevyo. (Umiliki wa watoto pia ni muhimu japokuwa hili lategemea zaidi mapenzi ya Mungu). Ikumbukwe kuwa Mwanamke ni MALI ya mwanaume lakini watoto ni mali ya Mwanamke na Mwanamme.

2.Uwe na MAAMUZI. Usilegelege katika maamuzi yako. Mwanaume ndiyo kichwa cha familia, kichwa hakipaswi kuyumbishwa na mabega.....sawa? Kumbuka wewe ni taasisi!

3. MWAJIBIKAJI: Ni wajibu wako kuhakikisha Mwanamke UNAYEMMILIKI anatosheka na na kuridhika na huduma zako. Bioloji yake ipate habari yake sawa sawa, tumbo lake lipate chakula cha kutosha, mwili wake upate mavazi na miguu viatu. Mkipata watoto na mwanamke wako ni wajibu wako kuhakikisha wanapata mahitaji yote wanayostahili. Kama huna uwezo kwanini uzae kama kuku? Kulaaaleki!

4. Ukishafanikiwa kuyamudu yooote hayo hapo juu, usisahau kuwa duniani kuna wanaume wenzako. Tafuta muda wa kukutana na wanaume wenzako uongeze ujuzi na maarifa ya kuuishi uanaume. Hapo valuu, biya na nyama choma vinaruhusiwa kusikiliza maongezi yenu. Ukishapiga haya makitu rudi kwa mwanamke wako kampe haki yake kulaaleki. Ikumbukwe kuwahi kurudi nyumbani si sifa ya mwanaume. Mwache Mwanamke wako awe na muda wa kuwa huru na kulea watoto.

5. Inapotokea kwa namna yoyote na kwa sababu yoyote ile necha ikashika kasi ukajikuta unaenda nje ya MWANAMKE WAKO, hakikisha unaenda kwa uangalifu. MWANAMKE WAKO asijue! Kosa kubwa sana akijua, na hii si sifa ya mwanaume. Huo ni uvulana. Na huko ufanye kwa UANGALIFU. Usijemletea maradhi MWANAMKE wako.

Kuna wakongwe wenzangu, WANAUME wenzangu kibao wako hapa jamvini wanaweza kuendeleza huo mlolongo.

Au kama vipi, leo ni ijumaa, twaweza panga mkakati wa kukutana ili tuzungumzie uanaume wetu.

SISI NDIO WANAUME BANA! Wanaume ndio SISI.

Sasa babu we si ushazeeka afu mwalimu wa somo la sayansi alitufundisha kuwa ufanisi huwa unapungua mtu akishafikia stage ya kuitwa babu. Au globolaizesheni inateki place? Au ndo ile wanasema Mbuzi anazeeka maini... lolz
Address piliz ya mahali kikao kitakuwa...):behindsofa:
 
Hawalipiwi lakini wapo pia ambao hawadaiwi hata robo shilingi. Na wengine wanapewa mahari hizo hizo na hao wanawake zao wanaoenda kuwaoa so mwanamke anajinunua mwenyewe!

Kama mwanaume amepokea pesa kwa mwanamke ili amuoe huyo mwanamke huyo ni mwanaume suruali sio kidume. Kwa hali hiyo na kwa tamaa ya pesa basi hata Cameroon anaweza akampatia msaada mwishowe akarudisha fadhira huyo hafai.
 
Wanaume wengi kwa kweli wanatabia za wafanyama wa porini! Nisiulizwe kitu
 
Gee aliyekuamsha leo kesho asirudie....khaaaa!!!!

Bee....hivi kweli watununue kisha wasilipe kodi kweli? Taifa lile hasara hivi hivi khaaaa!

Hivi mahari ikipokelewa anakabidhiwa mwali au wazazi? Kama wanapewa wazazi maana yake ni kuwa wazazi "wameniuzia" umiliki wa binti yao. gadem! Mi sitapokea mahari ya binti zangu wallah!

Mahari anakabidhiwa mwanamke, akitaka anawagawia wazazi wake wa enjoy zawadi pamoja :]
 
Mj1,kwani hujawahi kusikia mtu amekopeshwa gari na hajatoa hata mia na gari analo?Achilia mbali kutoa nusu!
 
Aaaah Mwanajamii1

Siku hizi mambo ni kuwa Ms mwanzo mwisho wa maisha yako. Akikuoa akikuacha akikuletea kimada, hawara na nyumba ndogo atajijua mwenyewe! lol

Hahahah Gaijin si ndio hapo sasa na wao wanakuona mkorofi kisa hujabadili to their Prefixes: Mie nakumbuka nililazimishwaga kubadili nikaletewaga hadi ile nioniliu ya mahakamani, nikasainishwa but vyeti vya elimu na official names za kazini; zikabakia with Ms. Nlikuwaga naitumia Mrs kwenye vikao vya arusi na vitchen parties tu!! mwe!!
 
Halafu Babu nikuulize mtu anawezajiita mmiliki wa kitu ambacho hajamaliza kukilipia? Si wanasemaga mahari haimaliziwagi?? Hata sijui kwa nini na sisi tunakimbiliaga kujibatiza majina yenu ilhali wengine hatukutolewaga mahaari na wengine bado wamekopeshwa
Hahahaha umiliki mama si lazima uwe kwa 100% Mahari haiishi kwa kuwa hatutakiwi kuondoa umiliki wa wazazi kwa binti yao.

Hahahaha mambo ya HISA! Mwenye hisa kubwa ndo mwenye mamlaka. Mme anamiliki 75% Wazazi wanabakiwa na 25%. Hii ndio siri ya mahari kutomalizwa. wazee waliona mbali bana.
 
Hizo 20% zitawatoka wenyewe mifukoni mwenu, kama tunataka milioni 10 tutawadai 12 ili tumuachie JK chake cha 2 M

khaa tena!! Kmbe hyo 10 ni exclsv, bsi bana yameisha maana naona inazd kla kw2
 
Hahahah Gaijin si ndio hapo sasa na wao wanakuona mkorofi kisa hujabadili to their Prefixes: Mie nakumbuka nililazimishwaga kubadili nikaletewaga hadi ile nioniliu ya mahakamani, nikasainishwa but vyeti vya elimu na official names za kazini; zikabakia with Ms. Nlikuwaga naitumia Mrs kwenye vikao vya arusi na vitchen parties tu!! mwe!!

Huuu! Silazimishiki hata kidogo! lolz .......
 
Halafu Babu nikuulize mtu anawezajiita mmiliki wa kitu ambacho hajamaliza kukilipia? Si wanasemaga mahari haimaliziwagi?? Hata sijui kwa nini na sisi tunakimbiliaga kujibatiza majina yenu ilhali wengine hatukutolewaga mahaari na wengine bado wamekopeshwa
Pamoja na hayo yote, sheria inasema huwezi uza kitu ambacho hauna umiliki, sasa swali kwa ODM ikiwa una full umiliki naomba uniuzie makoloni yako na ile ownership of property i pass kwangu?
Kama upo tayari nijuze fasta.
 
khaa tena!! Kmbe hyo 10 ni exclsv, bsi bana yameisha maana naona inazd kla kw2

bei ya mahari haiwezi kuwa VAT inclusive bana, inashusha value ya mke sasa...lol
 
Sasa babu we si ushazeeka afu mwalimu wa somo la sayansi alitufundisha kuwa ufanisi huwa unapungua mtu akishafikia stage ya kuitwa babu. Au globolaizesheni inateki place? Au ndo ile wanasema Mbuzi anazeeka maini... lolz
Address piliz ya mahali kikao kitakuwa...):behindsofa:
Hahahaha....... mkuu kaunta ya juu lazima ihusike. Mitaa ya Sinza na haka kamvua, nyagi litapata habari yake. Huo ndio uanaume sasa!

Pamoja na hayo yote, sheria inasema huwezi uza kitu ambacho hauna umiliki, sasa swali kwa ODM ikiwa una full umiliki naomba uniuzie makoloni yako na ile ownership of property i pass kwangu?
Kama upo tayari nijuze fasta.
Makoloni ni mali ya mtawala......... turudi kwenye hoja tafazali .LOL
 
Tena nini! Mchakato wa katiba mpya ni sasa. Wanaume kama mnataka kutambulika kisheria kuwa mmenunua wanawake wakati wenu ni huu.

Sheria ikiwatambua, mlipe kodi. Mla huliwa

halafu basi siku hizi wengi 'wanakopa' mahari

n sheria ikiwatambua ili walipe kodi ndo watajuta...cash bin cash, hakuna cha 'wazee kwa sasa mchukue tu hela ya blanketi la babu kisha mahari baada ya ndoa.

Lipeni cash bana kwanza hazina haina hela, hizo kodi zitasaidia sana serikali kuu
 
bei ya mahari haiwezi kuwa VAT inclusive bana, inashusha value ya mke sasa...lol
Sasa nyie si mmeamua kukaba hivi hauoni Gaijin anaziba mianya yote umebakia huo mmoja tu ambao ni VAT Inclusive ila nimeomba sheria hii isipitishwe wakati JK bado yuko madarakani.
 
Teh,teh,teh,teh,mtapinga sana mwisho wa siku wanawake wote wanajua wapo kwaajili yetu vidumee!
 
Sasa nyie si mmeamua kukaba hivi hauoni Gaijin anaziba mianya yote umebakia huo mmoja tu ambao ni VAT Inclusive ila nimeomba sheria hii isipitishwe wakati JK bado yuko madarakani.

Shida tuliyonayo sasa kama taifa kisha unataka serikali iendelee kukosa pato halali kwa kipindi cha miaka minne ijayo! Tungekutwisha che cha fisadi nyangumi lakini bahati mbaya kina mmiliki tayari......😛
 
Wanawake wote wa JF wanawakilishwa na Gaijin na bht kwenye hili timbwili.MJ1 kagusa akaona pa moto amesepa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom