A REJOINDER:
Preamble:
Katika utangulizi wako Aspirini unadai eti mwanaume ni Taasisi,my foot,apparently hata Adam katika bustani ya Eden thought so,see where he ended!
Aidha unadai kuwa mwanaume kapendelewa kuumbwa,hivi aliyelaaniwa akaambiwa kwa jasho lako utakula ni nani sio kidume Adam? na alitenda kosa gani by the way?
Tuje kwenye mada sasa pweint kwa pweint:
1.Urijali/umiliki:
Hivi wewe ukawazia kummiliki mwanamke amekuwa gari au nyumba.Is a woman a 'thing'?Hata katika lugha ya kijerumani mwanamke ni 'die' ,mwanaume ni 'der' na vitu vyote vilivyobaki ni 'das' au mwanamke unamuweka kundi la 'das'?
2.Maamuzi:Maamuzi yapi unayaongelea hapa yale yanayotolewa na kichwa cha juu ya kuamua kujenga,kufungua duka ,kununua gari?au yale unayoamua kwa kukutumia kichwa cha chini ya kuamua kulala na hausgel,kuzaa nje ya ndoa,kumjengea hawara n.k?
3.Uwajibikaji: Wangapi siku hizi wanalishwa na kuvishwa na wake zao? wanaume kibao wanatunzwa na wake zao na si kwamba hawataki kutunza kaya zao la hasha,ni circumnstances mme anajikuta ana kipato kidogo kuliko mkewe.Do you become less of a man kwa kuwa mke ana mshahara mkubwa kukuzidi? Learn to be humble.
Na hili la kudai mwanaume wa ukweli ni yule anayemridhisha mkewe kitandani,kama kigezo ni hicho basi duniani wanaume ni wa kuhesabu maana takwimu zinaonyesha ni wanawake wachache kwenye ndoa ambao huwa wanapata orgasm za kiukwelikweli.Wapo kinamama hadi wanapata vitukuu orgasm hawaijui.
4.Muda wa kukutana na wanaume wenzio: Hivi huko vijiweni la kuongea ni nini hasa kama sio kupapasa makalio ya mabaamedi? Na sio hilo tu, vijiweni huko ndo centre ya kudanganyana...oh mwanamke asikubabaishe bana akikujibu tia makofi...kumbe anayekushauri hayo akifika nyumbani kwake ni magoti chini mke wangu samahani nimechelewa kurudi.
5.Kwenda nje: Eti mradi mkeo asijue.Kumbe mnawaogopa? na kimada ukimpa mimba huo uso utauweka wapi,au ndo yale ya watoto kukutana makaburini kwenye msiba wa baba?
6. Uangalifu: tungekuwa waangalifu tungezaa nje?
'Sisi ndio wanaume bana'.......hahahahahahaa...usijisifu subiri usifiwe otherwise tutasema:
DEBE TUPU HALIACHI KUSHINDA
mwisho nasema:
Mwanamke akiwezeshwa anaweza!
Big up kinamama,yes you can!!!!!!
Yours sincerely,
Bishanga Abashaija.
Ahsante sana Bashaija kwa kudadavua pointi kwa pointi thread yangu. Umetumia nguvu nyingi kushabikia hoja zako. Na ma-likes ya kinamama umeyakamata kiukweli. Kiukweli pointi ulizoziandika hapo hazimzungumzii mwanaume! huyo atakuwa gumegume!!
Tukirudi kwenye hoja, sikuwa na nia ya kuwadhalilisha wanawake au kuonyesha uanaume wa mwanaume hauna mkono wa mwanamke. Mbu, MJ1 na wengine kama mngesoma thread kwa makini mngeliona hilo. Ulikuwa ni shauri kwa vijana wanaokaribia kuwa wanaume wasidhani uanaume ni lelemama! Ni zaidi ya hapo. Kutimiza au angalau kujitahidi kutimiza matakwa ya uanaume ndo hasa lilikuwa lengo langu.
Ukizoma kwa makini hoja za bishanga hapo juu ilikuwa ni kujaribu kukrashi points zangu na kuzitafutia mbadala wake kwa ubaya. Bishanga, ikiwa mtu anayatimiza yote niliyoyaandika, hapaswi kuwa mwanaume wa mfano wa kuigwa? Sasa huo si uanaume?
Sasa ndugu yangu Bishanga:
1. Kuwa rijali siyo sifa ya mwanaume? Kumridhisha mkeo siyo sifa ya UANAUME?
2. Mwanaume hapaswi kuwa na maamuzi
3.Mwanaume hapaswi kuwajibika?
4. Mwanaume hapaswi kubadilishana mawazo na wanaume wenzake?
5. Kwa hali halisi bila kudanganyana, hizi cheatings tunazishuhudia kila uchao. Mwanaume akicheat anapaswa afanye hadharani mpaka mkewe aone?
Anyway, kiukweli na bila kutafuta attention za wanawake, Kama Mwanaume hafanyi niliyoyataja na waliyoyataja wanaume wenzangu na nikayaunganisha kwenye thread, basi mi ntaendelea kuwa na msimamo ule ule kuwa huyo SI MWANAUME! kiukweli atakuwa amezaliwa mwanaume kwa bahati mbaya!
Narudia tena, sikuwa na nia ya kuwadhalilisha wanawake na wala sikuwa na nia ya kutamba kuwa UANAUME wa mtu hauna mkono wa mwanamke nyuma yake.
Baada ya kusema hayo, sasa nategemea kupata ma-LIKES ya kufa mtu toka kwa kina mama.
Ahsanteni kwa kunisoma.
Sisi ndio wanaume bana!
Naruhusu maswali matatu.