Sishauri Forker 50 na Forker 28 ziwe 'Branded' kama Ndege za Kibiashara za ATCL

Sishauri Forker 50 na Forker 28 ziwe 'Branded' kama Ndege za Kibiashara za ATCL

Mkuu umemaliza kila kitu
Mtanzania unampa kitabu chenye kurasa mia moja, yeye anakisoma mpaka ukurasa wa nne halafu anakiweka kabatini. Akiingia mtaani anaanza kubishana na mtu ambaye amekisoma kitabu mpaka mwisho.

Tunapata wanasiasa wa chini ya kiwango, tunapata wahasibu wa chini ya kiwango, kila sekta ipo chini ya viwango kwa sababu ya huu ufa wa kutotaka kukamilisha kila tukifanyacho.

Ni rahisi sana kuwaongopea wabongo kwa sababu ni watu tunaopenda mteremko, tunapenda kitonga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata angesema ziuzwe bado wakosoaji ungewaona humu. Ndiyo maana binafsi wakati mwingine naunga mkono rais kutoondekeza siasa za mlango wa demokrasia. nchi maskini kama hii inahitaji mkono wa chuma ili isonge mbele.
Ni kweli kabisa maskini haihitaji mijadala mingi ya kisomi isiyo na tija. Maskini anazo fursa kibao zimemzunguka, badala ya kuzifikiria anaishia kumezwa na mawazo ya wanaharakati.
 
Kama mbuzi zilikuwa ni mzigo kama mzigo mwingine sawa hiyo DREAMLINER zaidi ya mzigo wa mbuzi ilibeba mizigo gani mingine na walibeba abiria wangapi? Na DREAMLINER wakati inarudi ilibeba nini kama cargo na ilikuwa na passengers wangapi? Kuweni wakweli ndio mtalisaidia Taifa hili badala ya KUWA kama chiriku!!
wewe mliaji ndio ulete facts kama kubeba mbuzi kulikuwa kwa faida ama hasara.....plus yote uliyouliza
 
Huu uamuzi wa kuzipeleka ndege hizi kwa ATCL ili zifanye biashara umefikiwa baada ya mkuu kupewa paper maalum na jamaa wa ATCL mwaka jana. Sio uamuzi wa kukurupuka, wakati mwingine hilo neno kukurupuka ni aina fulani ya kejeli au dharau.
Mimi nimemnukuu tu mwandishi. Haimaanishi kuwa nakubaliana na kila neno au lugha aliyolitumia katika andiko lake. Kiufupi hata mimi sijawahi kumwambia mtu yeyote (mkubwa au mdogo kwangu) kuwa amekurupuka.
 
Una matatizo, hivi upate taarifa zote ili iweje? Hivi mtu baadala ya kusaka noti unapoteza ubongo wako katika hili

Wanaohusika wanajua umuhimu wa tarifa nilizoulizia, wewe kichwa mbuzi kwa upumbavu wako unaona napoteza ubongo!!
 
Acha Kudanganya na rudi tena ukamsikilize alichokisema tafadhali. Hakusema kuwa Ndege moja itabaki na zile mbili ndiyo zibebe Abiria bali alisema ni Ndege zote. Siku zingine kama huna uhakika na Kitu au labda hujasikia vizuri Mtu kasema nini jiridhishe Kwanza kuliko kuwahi kuja ' Kupopomika ' hapa Jamvini sawa?
Nikirejea hotuba ya Mh.Rais....yeye alisema ndege zitakazokuwa branded ATCL logo ni mbili tuu aina ya forker kati ya ndege tatu za Rais zilizopo...rudi kasikilize tena hotuba yake kwa umakini zaidi
 
Mbuzi kama wewe unatakiwa ukae kimya tu sio lazima uoneshe upumbavu wako!
sasa matusi ya nini? Nani alikutuma uandike utumbo? Ama kwavile comments ni bure? Andikeni vya maana 😀😀
Ili watu watoe comments za maana nashauri tuanze kulipia comments... Comment za bure pumba nyingi
 
Usijali. Rais anatumiaje ndege 3 kwa mfano? Kumbuka hata ndege 6 zote zilizonunuliwa ni mali ya serikali kupitia wakala wa ndege. ATCL amekodishwa tu
 
Ungekuwa mwanamke walah dushee ungelila sema basi tu, we mbea sana
Hii ni ' dharau ' kubwa kwa Marais waliopita kuanzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na Mzee Kikwete kwa Mtu mmoja leo kuamua kwa ' Kukurupuka ' tu kuwa Ndege za Rais Forker 50 na Forker 28 ziwe ' Branded ' kama ' Commercial Planes ' za ATCL.

Hili halipo na halijawahi kutokea nchi yoyote ile duniani na naamini hata tungekuwa Mbinguni Kwake Mwenyezi Mungu hata Yeye pia asingefanya hiki ' Kituko ' ambacho GENTAMYCINE nakiita ni cha Kufungulia mwaka huu ambao bado ni mbichi kabisa wa 2019.

Hoja kwamba zipakwe rangi kisha zichuke Abiria kwakuwa huwa zinakuwa ' grounded ' tu na kwamba hata mwenye Kuhusika nazo huwa hazitumii kwakuwa hasafiri mara kwa mara kutolewa na ' PhD Holder ' kidogo ni kutaka Kuwadhalilisha ' Intellectuals ' wote nchini Tanzania.

Wasaidizi wa Rais hebu fanyeni Kazi zenu vyema Kwake kwa Kumshauri mnaogopa nini? Hivi Sekta ya Anga ya leo au ATCL ya leo inahitaji kweli hadi hata Ndege za Marais nazo ziwe ' branded ' na zijumuishwe kama Ndege za Biashara na Kubeba Abiria? Je kuna hilo hitaji kweli?

Ningeambiwa au ningesikia Hoja kwamba labda Ndege hizo ziuzwe na ibaki moja kisha hizo Hela zitumike Kuimarisha Sekta ya Kilimo au nyinginezo ambazo zinahitaji msaada na ungalizi mkubwa ningemwelewa Mheshimiwa Rais na ningekubaliana nae kwa 100% ila kwa hii Hoja yake ya leo nampinga na naona ni kama vile ' Tusi ' kwa Watangulizi wake.

Wengine tumeumbwa kuwa wakweli na wawazi hivi hivyo mtusamehe tu na tuvumiliane. Tuache Kukurupuka na kuwa na ' Mihemko ' isiyo na Tija wala Mantiki. Halafu akina Donald Trump ' wakitutukana ' Waafrika huwa tunalalamika na kuona labda anatuonea wakati kumbe huwa yuko sahihi tena kwa 100% zote kutokana na ' Madhaifu ' yetu ya asili.

Nimesikitika!

Nawasilisha.

Gentamycine
Kwenye hili, kidogo tunatofautiana.
Ukweli ni kwamba ndege hizi zimekuwa zikitumika chini ya kiwango kwa kipindi kirefu hivyo kuzifanya zake ardhini bila kuruka kwa muda mrefu kitu ambacho ni hasara kwa ndege yenyewe na hata marubani kukosa masaa.
Leo serikali ikiamua kuziuza, itakula hasara maana re-sale value ukilinganisha na value halisi ya ukijumuisha matengezo kodi yetu itakuwa imeliwa.
Wakati TGFA ilipoundwa moja ya shughuli ambazo ilipasha kuzifanya ni ukodishaji wa ndege hizo [charter] na hata leseni kwa shughuli hiyo wanayo hadi leo.Tatizo ni kuwa kutokana na ukubwa wa ndege hizo na gharama za uendeshaji kwa saa, gharama za ukodishaji ni kubwa kuliko uwezo wa wateja wengi.
Hivyo kuzi-incorporate ndege hizo kwenye scheduled flights za ATC, zitakuwa na tija sana kwani mapato yatakayokuwa yanapatikana yataweza kuzi-maintain ndege hizo [badala ya kutegemea hazina]na vile vile itawavutia marubani wengine kutaka kurusha ndege hizo na kufaidika na masaa ya kurusha ndege.
 
Back
Top Bottom