Sirudii tena kuangalia mpira na wanawake

Sirudii tena kuangalia mpira na wanawake

vichekeshoo vichekeshoo vichekesho leo....... viiichekesho vichekesho vichekesho leooooooooooo....( just singing)
 
Kuangalia mpira na
Wanawake.
Wana maswali.....
>Mbona hawa Brazil
hawamchezeshi Neymar ??
:aliumia mechi iliyopita, hawezi
kucheza
>mbona hawajamkodi MESSI??
:hairuhusiwi kukodi..
>kwann asihamie Brazili?,..
:izo sio nyumba za kupanga
kwamba anahamia tu,mpaka uwe
una uraia wa Nchi yako.
>mbona hadi wanawake
wanacheza umo uwanjani?
:wapo wapi hao wanawake
>sihawo wa Brazil wenye nywele
ndefu?
:hapana hawo ni Wanaume,mmoja
anaitwa David Luiz,na huyo
mwingine WILLIUM
>Mbona hao wengine wanapiga
Penalty tano wenyewe?eti Refa
anapendelea?
:hakuna Penalty hapo ni
magoli,Brazil wamezidiwa
wanafungwa..
>Eti mbona Goli 7 ni nyingi na ni
Dk ya 80, kwann refa hamalizii tu
hapo si bingwa alishajulikana.
::sheria ya mpira mpaka Dk 90
zitimie..
>Huu si mpira wa miguu??
::Ndio we,nyie mnaonaje?
>mbona huyo mwingine anadaka
na mikono?
:huyo ni kipa
>kwann huyu Kipa wa Brazil
asikimbie na mpira adi goli
jingine alafu afunge apunguze
magoli au hajui huo ujanja?
Aaaaaaa jamani

Wanawake siku hizi mpira wanaujua sana mpaka wamezua misamiati. Mwanaume mwenye wivu anaitwa kiungo mkabaji. Anayefuatlia kila kitu wanasema anakaba mpaka kwenye penati.
 
Huyo demu wako atakuwa anaamkia watu kwenye wa kwenye tv lazima...
 
Alisahau tu kukuuliza
.......... na yule mchezaji wa brazil mwenye mwanya yuko wapi siku hizi?............
 
Hivi Luna timu za wanawake za mpira wa miguu uarabuni?? Wanavaa kininja?? Na baibui juu wakiwa wanacheza??
 
Huyo msupuuu wako atiii anatokea ushagoo gani?
 
Back
Top Bottom