hovyohovyo
JF-Expert Member
- Jul 8, 2012
- 547
- 157
Kwani Makinda mlimchagua au mlichaguliwa?? Ukishaweka hapo sahihi, kesi hakuna tena. Nadhani suala si kuwa Makinda anashindwa kwa sababu ni mwanamke. Kushindwa kwake hakuhusiani na yeye kuwa mwanamke. Hana uwezo tu kama ilivyo kwa baadhi ya wanaume wenzetu walioko ktk ngazi za uongozi. Wanawake wajifunze kutumia nguvu zao katika kupata nafasi za kuongoza, Ni hapo tu watakapoweza kuwa imara na kuonyesha wanaweza pasi na hofu. Ni sawa na mwanamke anayepewa ukuu wa wilaya au ukurugenzi nk kutokana na her "bottom power" na stupidly 'anahesabika' kama sehemu ya programu maalumu ya kuwa-empower wanawake. Ni matusi kwa wanawake kabisa. Amkeni.