Siri za moyoni zilizojificha za wanawake

PENZI SALAMA Ndugu zangu akina kaka Wenzangu nataka tujifunze hili leo.


Mwanamke anapenda kupendwa! Mara nyingi wanawake ndiyo hasa huwa na mapenzi ya dhati zaidi kuliko wanaume. Mwanamke anapoamua kuwa na mpenzi wake, humpenda kwa moyo wake wote, hivyo hupenda kuwa salama katika penzi la dhati kwako.


Anapenda uhuru, anapenda kujisikia wazi kwako mahali popote. Mwanamke anajisikia vibaya sana anapokuwa hana uhuru hata wa kukushika mkono mnakuwa barabarani pamoja. Anapenda penzi la uwazi!


Maana mwingine utakuta akikutana na rafiki yake, badala ya kumtambulisha vizuri kama mpenzi wake, anaanza kupatwa na kigugumizi. Utamsikia akisema: “Ah! Huyu ni rafiki yangu bwana, anaitwa Latipha....” hili ni kosa kubwa linalofanywa na wanaume wengi bila kujua ni kosa.


Mwanamke anakosa amani ya moyo kutokana na unavyomtafsirisha mbele ya rafiki zako. Anahisi hayupo salama. Lazima atajiuliza maswali, kwanini hataki kunitambulisha? Kwanini anashindwa kusema mimi ni mpenzi wake? Sifananii? Sina mvuto au nina tatizo gani?


Hayo yanaweza kuwa maswali yatakayomuumiza sana kichwa mpenzi wako, ambaye si ajabu akafanya maamuzi ambayo hutayapenda. Kidonda hiki hubaki moyoni mwa mwanamke, huwa vigumu sana kuonyesha wazi kwamba amechukia kutokana na uliyomfanyia, lakini atabaki akiugulia moyoni mwake kwa uchungu.


Hata hivyo, kinachokuja akilini mwake ni kutafuta mwanaume mwingine ambaye atakuwa wazi kwake ili aweze kufurahia mapenzi badala ya kuendelea kuumia moyoni mwake. Ni dhahiri kwamba uamuzi huu hautaufurahia hakika.


UNAVYOJALI...


Mwanamke anapenda awe wa pekee kwako, umsikilize, umjali na umpe kipaumbele katika kila unachokifanya. Wanawake wengi wanapenda kudekezwa, lakini hawapendi kuweka hilo wazi kwa mwanaume wake. Kwa kumtazama tu utagundua mpenzi wako anahitaji nini zaidi kwako!


Wakati mwingine anaweza kukupa mitihani ili kupima kiwango cha penzi lako. Anaweza kukuambia anaumwa au anauguliwa na mtu wake wa karibu, lengo ni kuangalia ni jinsi gani unakuwa makini anapokuwa na matatizo. Vile utakavyochukulia tatizo lake kwa ukaribu, uchungu na kuona kama lako, ndivyo utakavyomfanya aone thamani la penzi lako kwake, ikiwa vinginevyo basi humuacha na machungu moyoni, huku akijutia kuwa na mpenzi wa aina yako.


Hii ni siri ambayo si rahisi mwanamke wako akueleze moja kwa moja. Atatumia lugha ya ishara kuonesha jinsi ambavyo anahitaji kuwa wa pekee kwako.


JIFUNZE SIRI HIZO!


Hapa ndipo mwanaume mwerevu anatakiwa kuwa makini, ni lazima ufahamu siri zilizopo moyoni mwa mpenzi wako. Jifunze kusoma hisia za mpenzi wako kwa nje, kabla ya kufanya kitu, fikiria mara mbili, lakini baada ya kufanya, msome kupitia uso wake.


Analifurahia au umemchukiza?
Ni vizuri kugundua hilo ili uweze kufunga hisia za kumfanya aanze kufikiria kukusaliti. Hata mnapokuwa faragha ni vizuri kuwa makini na kila unachokifanya! Chunguza kama anafurahia penzi lako na manjonjo yote unayomfanyia.


Kumbuka kwamba ni vigumu sana mwanamke kukueleza moja kwa moja kwamba hujamfurahisha au kuna kitu umekikosea, hii husababishwa na hofu ya kuogopa kukufanya ujisikie vibaya.


Kwa maneno mengi WEWE mwanaume ndiye mwenye kazi ya kuangalia mwanamke wako anapenda nini na nini hapendi ili uweze kuwa MWANAUME wake bora, maana hata hisia zake za ndani utakuwa unazifahamu.
Ni rahisi sana, soma kupitia macho yake kila unachomfanyia, utaujua ukweli. Unajua hata ukimwita kwa jina ambalo hana msisimko nalo lakini ukiwa unamtazama usoni ni rahisi sana kugundua kitu fulani, kama hajakipenda utaona kwenye macho na akikipenda pia utaona.


Unapokuwa naye faragha, tumia uwezo wako wote, lakini kumbuka kwamba si kila utakachokifanya utamfurahisha. Hii inamaanisha kwamba, baada ya kumchunguza jinsi anavyosisimka, utaweza kugundua wapi kuna msisimko zaidi kuliko sehemu nyingine.


Hapo sasa unaweza kuibuka MSHINDI maana utakuwa umeziweka siri zake hadharani, kwa maneno mengine kama yeye aliona siri, basi umeweza kuzigundua na angalau umeanza kuzifanyia kazi. Nawapenda sana rafiki zangu. Wiki ijayo nitakuja na mada nyingine mpya na nzuri zaidi

Hivi hawa wenzetu ni Delicate kiasi hiki, Asprin , as Bramo yupo kwenye Bann, hebu njoo na uwaite na kina pretta, Kongosho waje kuthibitisha haya
 
Last edited by a moderator:
Hayo yote naunga mkono hoja!!! Ila KUBWA LAO umelisahau! WANAWAKE HAKUNA KITU TUNAPENDA KAMA KUPEWA GO AHEAD YA KUCHOP CHOP YOUR (MANS) MONEY AS IF YOU DONT CARE!!!! Hapo utakuwa umemmalizaaa!
kama zipo why not? lakini kama hazipo na yeye ndo true love utampenda tu
 
haswaa mapenzi bila pesa wapi na wapi.
ni sawa na kukamata mop kujipa moyo kuwa utadeki bahari, wapiiiiiiiiiiiiii??? Utakamua sana hiyo mop, sana sana ikifika jioni maji yanajaaaaaaaaa, unashangaa tu! Mijanaume mibahili, inipitie kando kwa kweli!
 
ni sawa na kukamata mop kujipa moyo kuwa utadeki bahari, wapiiiiiiiiiiiiii??? Utakamua sana hiyo mop, sana sana ikifika jioni maji yanajaaaaaaaaa, unashangaa tu! Mijanaume mibahili, inipitie kando kwa kweli!

Sasa Asprin nna hakika sio bahili, ila mlivyo wengi kila mtu ana atm card yake? Hako kasalare ka ukuli ina maana ana standing order ya mgawanyo? Naomba unieleweshe manake nafikiria ku-recruit mume wa pili
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom