Siri za moyoni zilizojificha za wanawake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siri za moyoni zilizojificha za wanawake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Sep 18, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  PENZI SALAMA Ndugu zangu akina kaka Wenzangu nataka tujifunze hili leo.


  Mwanamke anapenda kupendwa! Mara nyingi wanawake ndiyo hasa huwa na mapenzi ya dhati zaidi kuliko wanaume. Mwanamke anapoamua kuwa na mpenzi wake, humpenda kwa moyo wake wote, hivyo hupenda kuwa salama katika penzi la dhati kwako.


  Anapenda uhuru, anapenda kujisikia wazi kwako mahali popote. Mwanamke anajisikia vibaya sana anapokuwa hana uhuru hata wa kukushika mkono mnakuwa barabarani pamoja. Anapenda penzi la uwazi!


  Maana mwingine utakuta akikutana na rafiki yake, badala ya kumtambulisha vizuri kama mpenzi wake, anaanza kupatwa na kigugumizi. Utamsikia akisema: “Ah! Huyu ni rafiki yangu bwana, anaitwa Latipha....” hili ni kosa kubwa linalofanywa na wanaume wengi bila kujua ni kosa.


  Mwanamke anakosa amani ya moyo kutokana na unavyomtafsirisha mbele ya rafiki zako. Anahisi hayupo salama. Lazima atajiuliza maswali, kwanini hataki kunitambulisha? Kwanini anashindwa kusema mimi ni mpenzi wake? Sifananii? Sina mvuto au nina tatizo gani?


  Hayo yanaweza kuwa maswali yatakayomuumiza sana kichwa mpenzi wako, ambaye si ajabu akafanya maamuzi ambayo hutayapenda. Kidonda hiki hubaki moyoni mwa mwanamke, huwa vigumu sana kuonyesha wazi kwamba amechukia kutokana na uliyomfanyia, lakini atabaki akiugulia moyoni mwake kwa uchungu.


  Hata hivyo, kinachokuja akilini mwake ni kutafuta mwanaume mwingine ambaye atakuwa wazi kwake ili aweze kufurahia mapenzi badala ya kuendelea kuumia moyoni mwake. Ni dhahiri kwamba uamuzi huu hautaufurahia hakika.


  UNAVYOJALI...


  Mwanamke anapenda awe wa pekee kwako, umsikilize, umjali na umpe kipaumbele katika kila unachokifanya. Wanawake wengi wanapenda kudekezwa, lakini hawapendi kuweka hilo wazi kwa mwanaume wake. Kwa kumtazama tu utagundua mpenzi wako anahitaji nini zaidi kwako!


  Wakati mwingine anaweza kukupa mitihani ili kupima kiwango cha penzi lako. Anaweza kukuambia anaumwa au anauguliwa na mtu wake wa karibu, lengo ni kuangalia ni jinsi gani unakuwa makini anapokuwa na matatizo. Vile utakavyochukulia tatizo lake kwa ukaribu, uchungu na kuona kama lako, ndivyo utakavyomfanya aone thamani la penzi lako kwake, ikiwa vinginevyo basi humuacha na machungu moyoni, huku akijutia kuwa na mpenzi wa aina yako.


  Hii ni siri ambayo si rahisi mwanamke wako akueleze moja kwa moja. Atatumia lugha ya ishara kuonesha jinsi ambavyo anahitaji kuwa wa pekee kwako.


  JIFUNZE SIRI HIZO!


  Hapa ndipo mwanaume mwerevu anatakiwa kuwa makini, ni lazima ufahamu siri zilizopo moyoni mwa mpenzi wako. Jifunze kusoma hisia za mpenzi wako kwa nje, kabla ya kufanya kitu, fikiria mara mbili, lakini baada ya kufanya, msome kupitia uso wake.


  Analifurahia au umemchukiza?
  Ni vizuri kugundua hilo ili uweze kufunga hisia za kumfanya aanze kufikiria kukusaliti. Hata mnapokuwa faragha ni vizuri kuwa makini na kila unachokifanya! Chunguza kama anafurahia penzi lako na manjonjo yote unayomfanyia.


  Kumbuka kwamba ni vigumu sana mwanamke kukueleza moja kwa moja kwamba hujamfurahisha au kuna kitu umekikosea, hii husababishwa na hofu ya kuogopa kukufanya ujisikie vibaya.


  Kwa maneno mengi WEWE mwanaume ndiye mwenye kazi ya kuangalia mwanamke wako anapenda nini na nini hapendi ili uweze kuwa MWANAUME wake bora, maana hata hisia zake za ndani utakuwa unazifahamu.
  Ni rahisi sana, soma kupitia macho yake kila unachomfanyia, utaujua ukweli. Unajua hata ukimwita kwa jina ambalo hana msisimko nalo lakini ukiwa unamtazama usoni ni rahisi sana kugundua kitu fulani, kama hajakipenda utaona kwenye macho na akikipenda pia utaona.


  Unapokuwa naye faragha, tumia uwezo wako wote, lakini kumbuka kwamba si kila utakachokifanya utamfurahisha. Hii inamaanisha kwamba, baada ya kumchunguza jinsi anavyosisimka, utaweza kugundua wapi kuna msisimko zaidi kuliko sehemu nyingine.


  Hapo sasa unaweza kuibuka MSHINDI maana utakuwa umeziweka siri zake hadharani, kwa maneno mengine kama yeye aliona siri, basi umeweza kuzigundua na angalau umeanza kuzifanyia kazi. Nawapenda sana rafiki zangu. Wiki ijayo nitakuja na mada nyingine mpya na nzuri zaidi
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Sep 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Mwanamke anapenda kupendwa! Mara nyingi wanawake ndiyo hasa huwa na mapenzi ya dhati zaidi kuliko wanaume. Mwanamke anapoamua kuwa na mpenzi wake, humpenda kwa moyo wake wote, hivyo hupenda kuwa salama katika penzi la dhati kwako.


  Anapenda uhuru, anapenda kujisikia wazi kwako mahali popote. Mwanamke anajisikia vibaya sana anapokuwa hana uhuru hata wa kukushika mkono mnakuwa barabarani pamoja. Anapenda penzi la uwazi!
   
 3. salito

  salito JF-Expert Member

  #3
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Kaka ulichosema ni kweli,me niliwahi kuachwa hivyo hivyo,tena nilikuwa natania tu..nilikutana na rafiki yangu nikasema huyu ni dada yangu,huwezi amini niliachwa pale pale,nilibembeleza mpk nikachoka,nimekoma kabisa huu mchezo
   
 4. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #4
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  dryroots doh!umeugusa mtima wangu!
   
 5. s

  sindo Senior Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kaka mbona ya kina baba huleti
  lete mambo tuone
   
 6. s

  sindo Senior Member

  #6
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  nimeipenda siku ya leo
   
 7. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  mkuu hata mie hii cha kuachw kisa staili za kutambulishana imentokea mara tatu sasa mkuu.......
   
 8. awp

  awp JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,714
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  mpangaji wangu mmoja akitoka na mkewe alikuwa anamtambusha kuwa ni mdogo wake, nipomwuliza akasema amezidi kuwa mchafu. ufundishe awe msafi ni mbishi khaaa niliona kituko.
   
 9. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #9
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Hayo yote naunga mkono hoja!!! Ila KUBWA LAO umelisahau! WANAWAKE HAKUNA KITU TUNAPENDA KAMA KUPEWA GO AHEAD YA KUCHOP CHOP YOUR (MANS) MONEY AS IF YOU DONT CARE!!!! Hapo utakuwa umemmalizaaa!
   
 10. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #10
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mngejua nasi twazijua siri zilizojicha ndani ya mioyo yenu, msingekuwa mnafundishana kutufahamu kwa undani.
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Sep 18, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  huo uchafu alianzaga kabla ama baada ya ndoa? Mbinafsi wa hedi! Anashindwa kuuliza wanawake wa ofisini wapi pa kusuka nywele. Abebe mke jumamosi akambwage saluni awaambie nisukieni wife nampitie saa ngapi. Apitishie boutique kununua kivazi na atoke nae jioni! Kuna mwanaume anaenda kulala gesti kwa sababu kwake kuna mbu, asinunue wavu wa mbu au kufanya fumigation?
  mtaula wa chuya kwa uvivu wa kupembua! Msome LARA1 hapo juu. Hamtaki kugharamia mnataka vinavyoelea eeh!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Mzalendo wa ukweli

  Mzalendo wa ukweli JF-Expert Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 562
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha binti.com hebu ziweke wazi hizo siri za wanaume ambazo unazijua,acha sisi tujifunze siri zenu ili tujue how to love you guys vzr!!!!!!
   
 13. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #13
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Siri moja common kwa wanaume wote ni "kuwa very weak" kwa mwanamke. Hakuna mwanaume yeyote mwenye ujanja kwa mwanamke, hilo halina ubishi.
   
 14. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #14
  Sep 18, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  lara 1, we r sailing together! utamkuta mwanaume mbahiliiiiiiiii lakini papa lako anataka kulichop mara 9 na nusu kwa siku, ila kugharamia nehi, ataisubiria sana meli airport! wekeni ATM zenu mezani waume zetu, lol! tutawapeni mpaka mtakinai, lol!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. m

  mymy JF-Expert Member

  #15
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  aiseee.....Mzizi mkavu u touched me. mbona kama unayesoma akili yangu....!!!!
   
 16. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #16
  Sep 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,123
  Trophy Points: 280
  Umeoonaaaa! Jitu halikutunzi, afu ukifubaaaa linakukana na kukuita dada! Mwanamke ukiwa na mume design hiyo usipohangaika utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchambu!!!!!
   
 17. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,175
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  umeona enh,hao wanaowawekea ATM zao mezani ndo mana wanawaona wanameremeta kila wanapokutana,kila wakiwatembelea hom wanakuta pochopocho za kufa mtu!
   
 18. m

  mymy JF-Expert Member

  #18
  Sep 18, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 245
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  usemavyo bint.com ni kweli wanaume ni dhaifu sana mbele ya mwanamke.
   
 19. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #19
  Sep 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,858
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  mwanamke matunzo, unakuta unamwambia unataka kwenda salun anakupa msimbazi. hata hautoshi kufumua nywele lol!
   
 20. chameli

  chameli Senior Member

  #20
  Sep 18, 2012
  Joined: Jul 23, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haswaa mapenzi bila pesa wapi na wapi.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...