Siri yafichuka viungo vya Albino

Siri yafichuka viungo vya Albino

Katibu wa Chama chakavu huvaa hirizi kubwa kiunoni inabidi kujua kama hiyo haina viungo vya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi

Ha ha ha ha Masanilo alisahau kuchomeka vuzuri alivyokuwa ananyanyuanyanua mikono ukaiona nini? Maana hawa jamaa na siasa ilivyokuwa biashara ngumu kwao mwaka huu kama una albino kamfiche nje ya nchi baada ya uchaguzi mkuu umrudishe
 
Hawa waganga wa kienyeji ni waongo kama baba ya shetani alivyo muongo ni matapeli tu waganga njaa wenye kutumia ujanja ujanja kupata mkate wa kila siku, ukiangalia magazeti ya udaku kuna mengine page mbili yamejaa matangazo yao. Kuna kijana mwanafunzi yalimkuta ya kumkuta, uwezo wake darasani haukua wa kutisha, demand ya his performance iko kubwa, si akakutana na kipeperushi eti mganga sijui toka sumbawanga ana dawa ya kuongeza akili ya darasani. Dogo kaenda kajieleza mwisho wa siku mganga anamueleza dawa itaingizwa kwa njia ya haja kubwa, kijana akaingizwa dawa zaidi ya mara 4 siku tofauti, mwisho wa siku kawa shoga akaaanza kuwarubuni wenzake shule, walipokamatwa na kuhojiwa dogo akasema alivyoanza. Walimu ikabidi wawaite wazee wote wa watoto husika na kuwaeleza kilichojiri.

Kama ni waongo wasingekuwa na wateja mkuu. mambo yao ni uhakika.
 
baada ya kuwa dili unafanyiwa nini?
huu ni muda watanzania hatutakiwi kuiachia serikali pekee hili swala..
tusiishie kusikitika tu hawa watu wapo na wengine hata serikalini wapo lakini sisi wananchi tukiamua tunaweza...
binafsi nimeamua kuchukua hatua kuhusu hili swala gumu..
mungu awe pamoja nami.

Watu kama hao kuwaweka mahakamani ni kuongeza msongamano na jam ya kesi tu.
wananchi tuchukue hatua
 
Kwa nini hatutapata Ufumbuzi wa janga hili la mauaji ya Albino!

Nimefuatilia upelelezi wa mauaji ya Albino nchini na kugundua kwamba vyombo vya usalama wamejikita zaidi kutafuta wauaji badala ya kuwatumia hao watu kuwakamata wenye kuhitaji viungo hivyo. Utakamata wangapi ikiwa wahitaji wapo radjhi kutoa mabillioni? maana ukweli ni kwamba fedha zinazoahidiwa kutolewa na hawa wanunuzi ni zaidi ya meno ya Tembo na kutokana na njaa ya Utajiri nchini wamewapata wengi.

Hivyo pamoja na kuendelea kuwakamata hawa majangili wa viongo vya binadamu ni muhimu sana askari wetu wa upelelezi wawatumie hawa wauaji kuwapata wanunuzi maana siku zote Mahitaji (Demand) ndio hujenga Usambazaji (Supply). Na ndio maana hata baada ya kuwakamata hawa wachache, mauaji bado yanaendelea kwa sababu soko la viungo vya binadamu bado lipo na linazidi kukua.

Ikumbukwe tu kwamba miaka ya 90 kulikuwa na mauaji ya watu wenye vipara, na kwa sababu hiyo hiyo ya Uganga wa Uheshimiwa (Power) ili kujenga Utajiri wakauawa watu wengi tu hadi ilipobainika kwamba sii kweli nguvu ya kuogopwa (uheshimiwa) na Utajiri hautokana na Uchawi wa viungo vya watu wenye vipara. Utafiti wa kichawi ukageuza deal na kuwa viongo vya Albino ili mradi watu waamini kama walivyoamini maji ya babu wa Loliondo!

Na kikubwa zaidi tufahamu kwamba hata katika taratibu za kimfumo wa wenzetu waloendelea wanaamini japo sii kwa uchawi ya kwamba ili uwe na nguvu ya kuheshimiwa (power) na kuogopwa unahitaji kwanza UTAJIRI ambao utakujengea jina na heshima, na ukisha kuwa na power basi dunia ni yako. Formula hii inatumiwa kote duniani na kwa bahati mbaya sana sisi bado imani zetu za Kichawi ndizo suluhisho.

Nitashauri vyombo vyetu vya upelelezi wabadilishe mfumo wa kufuta mauaji haya kwa kuwatumia hao hao wauaji wawataje wanunuzi wanunuzi wa viongo vya binadamu, ili kuondoa soko lake na tukifanikiwa hakuna Albino atakaye uawa kwa sababu hakuna mhitaji...
 
mganga wa jadi alikuwa mbunge wakuteuliwa wa bunge maalum la katiba- akaweke kifungu kipi? ona sasa ndo kwaanza wanalaumiwa- sawa na 'angeenda na mbunge wa kuteuliwa akawakilishe wezi, au mwakilishi wa machangu,madawa ya kulevya,mashoga,,nk.nk
 
Nimeona kuna wazungu nao kwamba wanahusika, ni wazungu wazungu ama wazungu weusi?
 
Naomba kuuliza, ulemavu wa ngozi (albino) ni ugonjwa wa kurithi? Au unatokea tu?
 
Hawa waganga wa kienyeji ni waongo kama baba ya shetani alivyo muongo ni matapeli tu waganga njaa wenye kutumia ujanja ujanja kupata mkate wa kila siku, ukiangalia magazeti ya udaku kuna mengine page mbili yamejaa matangazo yao. Kuna kijana mwanafunzi yalimkuta ya kumkuta, uwezo wake darasani haukua wa kutisha, demand ya his performance iko kubwa, si akakutana na kipeperushi eti mganga sijui toka sumbawanga ana dawa ya kuongeza akili ya darasani. Dogo kaenda kajieleza mwisho wa siku mganga anamueleza dawa itaingizwa kwa njia ya haja kubwa, kijana akaingizwa dawa zaidi ya mara 4 siku tofauti, mwisho wa siku kawa shoga akaaanza kuwarubuni wenzake shule, walipokamatwa na kuhojiwa dogo akasema alivyoanza. Walimu ikabidi wawaite wazee wote wa watoto husika na kuwaeleza kilichojiri.

We acha tu, wanadhani shetani atawahurumia. Wao wapo kazini na mawakala wao. Malengo yao makubwa ni kuikamata dunia yote waitumikishe. Unadhani wata share information na yeyote atakaewakosesha mfuasi wao hata mmoja? Ndiyo maana mambo yao yote yana mislead kila kukicha. Waombaji wa kweli wa Mungu wanapaswa kukesha ili kuweza kurudisha akili za watu vichwani mwao, kwani wakati mwingine hawa watenda Unyama kuna Roho zimewavaa na pengine hawajitambui. Kwanini Waganga wasikamatwe na kunyongwa maana ndiyo wanaowasukuma watu kuua kama si kuwatuma?
 
Hivi haya mauaji ni Danganyika tu au na nchi zingine za africa yapo?
 
Nimeshtuka kusikia wanunuzi ni pamoja na wazungu wa geita gold mining.
 
CHADEMA hawawezi kufanya siasa bila ushirikina, CCM ilikuwepo tokea miaka ya 60 lakini hatukuwahi kusikia mauaji ya dizaini hii.
 
CHADEMA hawawezi kufanya siasa bila ushirikina, CCM ilikuwepo tokea miaka ya 60 lakini hatukuwahi kusikia mauaji ya dizaini hii.

Kwanza jina lako linarandana na Mganga moja yupo bukombe, nakumbuka ccm waliwaminishaga watanzania kua Albino afagi wanapotea
 
Unapo sema wateja wa biashara hiyo ni wazungu kutoka Geita ndio nini sasa uzungu ni nini na kwa nini unaficha wanunuzi ni akina nani wataje kwa majina serikar inalea hii hali wanajua @ kinacho endelea washenzi hao
 
Dawa ya hao wauaji wa albino ilishasemwa na Pinda siku nyingi sijui tunashindwa wapi kuitekeleza.

Pinda alisema wauwawe...lakini hawauwawi....eti sheria na haku za binadamu.

Lakini pinda huyohuyo alisema Piga tu...na watu wanapiga tu.
Kuna haja sasa wananchi waamue kuwapiga tu waganga. Hao ndio chanzo kikuu cha haya mambo.
Mi nasema wapigwe tu....
 
Ni vizuri ukijikita kwenye mada kkuliko kuhusisha vyama kwenye suala mtambuka kama hili Musa alan
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom