Siri yafichuka viungo vya Albino

Siri yafichuka viungo vya Albino

Chademakwanza

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2014
Posts
6,346
Reaction score
1,873
Kila kiungo kimoja cha ‘albino', huuzwa kwa bei kubwa, hali inayotajwa kuwa kiini cha kukithiri kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, mahakama mkoani Geita ilielezwa jana.Ingawa bei ya viungo vya albino ilitajwa jana mahakamani, lakini Mwananchi haliwezi kutaja thamani hiyo ili kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi.

Akitoa ushahidi katika kesi namba 43/2009 ya mauaji ya albino, Zawadi Magimbu, mkazi wa Kijiji cha Nyamaruru wilayani Geita, shahidi wa 12 ambaye ni polisi wa upelelezi kutoka Makao Makuu ya Polisi, Dar es Salaam aliibua mambo lukuki ya ajabu yanayofanywa na wauaji wa albino.

Mambo hayo ni pamoja na thamani ya fedha wanazolipwa watu kwa kila kiungo kimoja cha albino kiasi cha (tunahifadhi)katika Kanda ya Ziwa, huku viungo hivyo pia vikitofautishwa ubora kwa kupimwa na redio, wembe na Sh1 ya zamani.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Masaru Kahindi, Ndahanya Lumola, Nassoro Charles na Singu Siantem. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 5 itakapotolewa hukumu.

Akitoa ushahidi mbele ya Jaji Joacqiune Demello, shahidi huyo (jina linahifadhiwa), alidai upelelezi wa polisi ulibaini kuwa wakati wa mauaji ya mwaka 2008, watuhumiwa walikuwa wanashawishiwa kulipwa kiasi kikubwa kwa kila kiungo kimoja cha albino.

"Nilitoka Dar es Salaam kuja Mkoa wa Shinyanga kufanya upelelezi wa mauaji ya albino. Nikiwa Shinyanga, tulipata taarifa kutoka kwa msiri wetu aliyetueleza kuna watu wanafanya biashara ya viungo vya albino," alidai shahidi huyo.

Alidai baada ya kupata taarifa hizo, waliamua kuweka mtego ili kuwakamata watu hao waliokuwa wakijishughulisha na biashara hiyo.

"Tulitafuta albino wawili kwa ajili ya mtego na kafanikiwa kuwakamata watu wawili, ambao ni Robert Magoma na Ndahanya Lumola waliokuwa wakijishughulisha na biashara hiyo," alidai shahidi huyo.

"Katika uchunguzi wetu, tuligundua kuwa kuna mganga aliyetajwa kwa jina la Gerald Mazuri, mkazi wa Kijiji cha Kakoyoyo, Kata ya Ushirombo, Wilaya ya Bukombe kuwa anafanya biashara hiyo na Wazungu kutoka Wilaya ya Geita (hawakutajwa).

Alidai kuwa wembe, redio na shilingi hutumika kama vipimo vya kujua ubora wa viungo vya albino.

"Niliendelea kuwadadisi, wakasema walipeleka mifupa hiyo kwa Mganga wa Jadi, Mussa Ally wa mjini Katoro, mkoani Geita ikapimwa kwa kutumia wembe, redio inayozungumza na Sh1 ya zamani," alidai shahidi huyo na anamnukuu mmoja wa washtakiwa:

"Ukichukua wembe ukauweka kwenye mfupa wa albino na kunasa, basi mfupa huo ni dili, kinyume chake hauna ubora. Pia, ukichukua Sh1 ukaiweka kwenye mfupa na kunasa, nao ni bora na redio inayozungumza ukiisogeza kwenye mfupa huo na kuzima, ujue kiungo hicho ni dili."

Desemba 27 mwaka jana, mtoto Pendo Emmanuel (4), alitekwa na watu wasiojulikana katika Kijiji cha Ndami, Wilaya ya Kwimba.

Februari 15, mwaka huu, mtoto Yohana Bahati (1), alitekwa kabla ya kuokotwa akiwa amekufa na miguu na mikono yake kukatwa.

Hivi karibuni, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, ilipiga marufuku waganga wa jadi kupiga ramli.


Chanzo: Mwananchi
 
redio inayozungumza ukiisogeza
kwenye mfupa huo na kuzima,
ujue kiungo hicho ni dili.”...,...dooh
 
kwa uovu watu inatakiwa kumrudia Mungu,ikiwa damu Abil ilimtesa kaini itakuwa hivyo kwa yeyote anaye mwaga damu isiyo na hatia
 
Dawa ya hao wauaji wa albino ilishasemwa na Pinda siku nyingi sijui tunashindwa wapi kuitekeleza.
 
Huu ni ushetani uliopitiliza, kwanini tusipige marufuku uganga wa kienyeji tu?
 
baada ya kuwa dili unafanyiwa nini?
huu ni muda watanzania hatutakiwi kuiachia serikali pekee hili swala..
tusiishie kusikitika tu hawa watu wapo na wengine hata serikalini wapo lakini sisi wananchi tukiamua tunaweza...
binafsi nimeamua kuchukua hatua kuhusu hili swala gumu..
mungu awe pamoja nami.
 
ndo maana viongozi wengi wa ccm ni matajiri sana kumbe hivi viungo vya albino ndo dili zao
 
redio inayozungumza ukiisogeza
kwenye mfupa huo na kuzima,
ujue kiungo hicho ni dili."...,...dooh
mkuu huu utafiti umefanyika wapi mfupa wowote wa binadamu ukiuweka kwenye radio inazima au ni albino tuu.
 
Kumbe CCM ndivyo walivyo, Komba tu kielelezo miaka ya nyuma alishakuwa na Shule na Nyumba kubwa ya thamani ya Bil. 1. pale kwa komba Mbezi-Kawe, kumbe haya maccm ni Uganga kwa kwenda mbele.
 
Wateja wakuu wa waganga wa Kienyeji si ccm? Ndio maana lumumba kuna vibuyu vingi sana
 
Ccm wasifanye mazingaombwe hapa km hawahusiki kwanini wasilete wahusika? Mbona mambo magumi mazito yanaibuliwa lakini limeshindikana? Miaka nenda rudi. Km kweli viongozi wa ccm hawahusiki watuletee wahusika. Wasilete za leheba kuchezea uhai wa ndugu zetu km wanavyochezea hela zetu.
 
Hawa waganga wa kienyeji ni waongo kama baba ya shetani alivyo muongo ni matapeli tu waganga njaa wenye kutumia ujanja ujanja kupata mkate wa kila siku, ukiangalia magazeti ya udaku kuna mengine page mbili yamejaa matangazo yao. Kuna kijana mwanafunzi yalimkuta ya kumkuta, uwezo wake darasani haukua wa kutisha, demand ya his performance iko kubwa, si akakutana na kipeperushi eti mganga sijui toka sumbawanga ana dawa ya kuongeza akili ya darasani. Dogo kaenda kajieleza mwisho wa siku mganga anamueleza dawa itaingizwa kwa njia ya haja kubwa, kijana akaingizwa dawa zaidi ya mara 4 siku tofauti, mwisho wa siku kawa shoga akaaanza kuwarubuni wenzake shule, walipokamatwa na kuhojiwa dogo akasema alivyoanza. Walimu ikabidi wawaite wazee wote wa watoto husika na kuwaeleza kilichojiri.
 
Kumbe CCM ndivyo walivyo, Komba tu kielelezo miaka ya nyuma alishakuwa na Shule na Nyumba kubwa ya thamani ya Bil. 1. pale kwa komba Mbezi-Kawe, kumbe haya maccm ni Uganga kwa kwenda mbele.

Ndani ya Ccm kuna mbunge wake ni Mganga wa Kienyeji yeye anafanyaje Kazi zake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom