SIRI YAFICHUKA: Deni la 2 billion/- latua Ikulu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SIRI YAFICHUKA: Deni la 2 billion/- latua Ikulu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, Jun 9, 2010.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Asalaam Aleykum,

  Taarifa nilizonazo ni kuwa TFF walienda benki ya NMB kuomba mkopo kwa njia ya overdraft ili waweze kuwalipa Brazil appearance fees za kuja Tanzania. Sina uhakika na exact figure ya mkopo ila taarifa ni kuwa it was $2.5 million (kama shilingi bilioni 3 hivi). NMB wakijua fika kama sponsors wa TFF kuwa shirikisho hilo halina uwezo wa kulipa mkopo huo, walikataa kutoa fedha hizo. Waziri wa Michezo, George Mkuchika, akaiandikia barua NMB kuunga mkono ombi la mkopo huo. Baada ya ku-assess risk za mkopo huo kwa TFF ambao NMB inawajua fika kuwa hawana pesa na kila siku wanatembeza bakuli la kuomba msaada, walimgomea Waziri Mkuchika na kusema hawamtambui. Uongozi wa NMB ukasimama kidete na kusisitiza kuwa kamwe hautatoa mkopo kwa TFF kuwalipa Brazil waje Tanzania mpaka Rais Kikwete au Waziri Mkuu Pinda aandike barua ya serikali kutoa guarantee kwa mkopo huo. Hapo ndipo baada ya kupata baraka zote za Ikulu, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, akaiandikia barua NMB kuwa serikali inaweka commitment ya kubeba deni lote iwapo TFF watashindwa kulipa deni hilo. Baada ya kupata guarantee hiyo kutoka kwa Waziri wa Fedha, NMB wakakubali kutoa overdraft kwa TFF.

  Business plan ya TFF ilikuwa kwamba kwa wastani wa bei ya ticket ya 50,000/- x watu 60,000 = shilingi bilioni 3. Matokeo yake ni kuwa tiketi za VIP tu ndiyo zilikuwa sold out huku zile za walala hoi ambao ndiyo walitarajiwa kujaa uwanjani zikabaki wazi. Sijasikia TFF ikitangaza mapato, lakini sidhani kama itafika hata shilingi bilioni 1. Hii ina maana kuwa serikali italazimika kubeba deni la zaidi ya shilingi bilioni 2 kutokana na guarantee iliyoiwekea TFF.

  It seemed like a good idea at that time. Ujio wa Brazil unge raise profile ya soka la Tanzania, ungeutangaza Uwanja wa Taifa duniani, ungevutia watalii na wawekezaji Tanzania na ungemjengea sifa JK kwa umma wa Watanzania kama "Mpenzi mahiri wa michezo" kama mabango makubwa yenye picha ya Rais akibusu Kombe la Dunia yalivyopambwa uwanjani siku ya mechi. Ninaambiwa kuwa Rais Kikwete alifurahia sana mpango wa kuileta Brazil nchini na kuamuru serikali itoe kila ushirikiano kwa TFF kufanikisha jambo hili.
  Matokeo yake ni kuwa kulikuwa na maelfu ya viti vitupu uwanjani baada ya wananchi kushindwa kulipa kiingilio.

  Hii ni ishara tosha ya kuwa serikali hii iliyo ahidi kuleta Maisha Bora kwa kila Mtanzania kumbe wala haijui umasikini halisi wa wananchi wake yenyewe! Hicho kiingilio cha chini cha elfu 30 ni mapato ya mwezi mzima ya Watanzania walio wengi ingawa its just pocket change kwa viongozi wetu.

  HII NDIYO NCHI YETU NA HAWA NDIYO VIONGOZI WAKE.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  I'm exhausted of words!!!! Naipongeza NMB kwa msimamo wake wa awali na swali lin alokuja hapa mara moja -- kwa nini serikali isiende kwa watu wao wa madili -- CRDB? Remember Richmond, Kagoda?

  Even though this TFF-NMB deal was not ufisadi, lakini ni onyesho tosha jinsi serikali yetu inayokuwa so mindless na carefree when it comes to strict financial administration kuhusu matumizi nya fedha za umma..

  Anyway ikulu itapata tu hela za kulipa deni hilo -- wakwepa kodi wakubwa wawili au watatu (wadosi hasa) wataagizwa ku-settle the bill.
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sisi wengine bado tunaisubiri REAL MADRID! Hili la Brazil limeshaisha! TFF walisahau tu kuwatumia ma-brainwashers wa Clouds FM akina Gerald na Ephraim.
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Teh teh teh teh waungwana wanajua kugawana kodi zetu? hivi Brazil wametoa risiti ya hiyo billion $2.5?
   
 5. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  TFF wapumbavu.......kuweka viingilio vikubwa namna ile walitarajia nini?
   
 6. JS

  JS JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimependa msimamo wa NMB ni mzuri sana. Mkullo, lipa deni la NMB fasta
   
 7. b

  buckreef JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mapato makubwa kwenye mipira hayatokani na kiingilio, bali pia vitu kama mikataba na TV pamoja na matangazo.

  Hiyo mechi imeonyeshwa na TV nyingi tu hapa duniani, huenda pesa za huko zikapunguza deni hata kama sio lote.
   
 8. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  safi sana NMB. ILA SASA UCHUNGU WA HELA YA MTANZANIAAAAA,HII NI AKILI KWELI???
   
 9. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #9
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tusubiri tuletewe Naomi Cambel kiingilio kitakuwa 300,000/=
  atakuja wewe subiri tuu.
  alishaongea nae kule kweupe siku ileee anakumbuka mwenyewe.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Clouds kuna vilaza wengine pale!!!

  Huwa wanaongea utafikiri wako kwenye chupa. Hawaangalii ukweli wa mambo ulivyo bali ni ushabiki tu na kujidanganya kwamba they know a lot. Wameipigia debe na kuisifu sana hii trip ya Brazil. What value does it add to Tanzania? Ni kula hela za walipa kodi tu!!

  Hivi hizi barabara zilizojaa mashimo baada ya mvua zitatengenezwa lini ilhali tunasikia Tanroads inadaiwa zaidi ya bilioni 300 na makandarasi. Halafu bila aibu hela za walipa kodi zinaenda kuluipia mpira eti sisi tunapenda burudani.

  Tukiiharibu hii nchi hivi tunafikiri nani ataharibikiwa au Clouds wao wana dual citizen kwa ajiri ya vipindi wanavyovirusha?

  Inanifanya nivute pumzi na kuwakumbuka Fina na Masoud Kipanya. Nao hao walikuwepo kisha wakaondoka.
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Jun 9, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  HEHEHEHE
  hahahaha
  thats is futibo
   
 12. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #12
  Jun 9, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  jamani naomba mie mnisaidie kuyajua haya yafuatayo kuhusu mechi ya brazili na tanzania
  1:- tuliambiwa wakija nchi itajitangaza kitalii maana itaonekana katika television za nchi 160....je ni television zipi zilizoonyesha mechi hiyo zaidi ya hii ya tido mhando?
  2:- kwanini tuliwalipa brazil?...inamaana kila mechi wanayocheza brazil wanalipwa na nchi waliyocheza nayo?
   
 13. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kuiletaa Brazil ni wazo zuri ila timing mbovuuuu..inasikitishaa kuwa na uongozii unaofanya maamuzii kishabikii zaidiii kulikoo tathiminii ya kinaa..Serikali ilikuwa ina uwezoo wa kukataa upuuzii huu wa kuweka guarantee ya $2.5m kwa ajili ya kuilipaa brazili tuu bila tathiminii ya cost benefit analysis...

  nchi haiendeshwii kama duka kwa kuwa tuu muungwanaa ana furahiaa jambo hilo basi lazima lifanyikee..hili ni taifa na mustakabali wake ni kwa wananchii wakee..

  sioni kama kiongozii mpendaa michezoo ndani ya miaka 5 ameshindwa kushawishi kuwa na miundo mbinu ya michezo ukiachilia sualaa la kuajiriwaa maximo ambaloo kama mkuu wa taifaa sio kigezoo cha ufanisii..kumbukeni tumekuwaa na makocha wa kigeni kwa muda mrefuu tuuu...

  naaminii deni hiloo la tff kwa niaba ya serikalii ni mzigoo mwinginee kwa walipaa kodii kwa upuuzii wa wachache wasiona mbele ila wenye dhamana ya umma.

  hivi ile kamati ya kuimarket TZ kwenye WC 2010 katika mipango yake imetekelezaa mangapi ukiondooaa jambo hilii la hasaraa la kuileta brazil kutokana na rush hrs negotiations???????? wajifunzee hata kwa Zimbabwe!!!!
   
 14. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Bilioni 2 mmewapa na kinyago juu.

  Kudadadeki!
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mfanyabiashara huyo anaeleza kwamba kwa hali halisi iliyopo kwenye mfumo wa ukusanyaji kodi, ni vugumu kukwepa ushuru kwa kudanganya kiasi (idadi) cha mali kilichomo kwenye kontena (false declaration) au kuweka bei ndogo au ya chini ya ile bei halisi (under invoicing), lakini kwa kampuni hiyo hilo linawezekana kwa kuwa mfumo mzima tangu serikalini, Tiscan na TRA umekuwa nyuma yao kutokana na nguvu kubwa waliyonayo vijana hao.
  Imeelezwa kwmaba kwenye kampeni za mwaka 2005 kampuni hiyo ilichangia chama tawala Sh. Milioni 200 na kwamba katika mwaka huu wameahidi kuchangia milioni 500 huku ofisini kwao zikiwa zimejaa picha walizopata kupiga na viongozi wa juu wa chama tawala na Serikali katika hafla za uchangiaji kampeni.

  From: Ufisadi wa kutisha ushuru wa forodha

   
 16. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa kiingilio cha 30,000/= ulitegemea viti vingejaa?Kwa kua wao wanagawana mamilioni pale TFF wanadhani elf 30,000/= ni 300/= matokeo yake wanaitia serikali hasara kubwa hivi, kuna mambo yanakera kwa kweli.
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  hapo tumeshaliwa, hakuna jipya ni yale yale ya matumizi yaliyokosa nidhamu, CAG upo?
   
 18. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2010
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Angalizo: sikuona tangazo lolote la kutangaza utalii mfano mbuga zetu...zaidi ya matangazo ya kisiasa na mambo ya kilimo kwanza. namalizia kwa kusema:

  "You're not supposed to be so blind with patriotism that you can't face reality. Wrong is wrong, no matter who says it" Malcolm X
   
 19. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  katka filamu hii sijui nani ndio starring!......but am enjoying it japo staki :(
   
 20. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Ilionyeshwa na TV nyingi tu za nje. Kwa UK, walionyesha ESPN ambayo ni TV ya kulipia ya michezo na inaonyesha michezo kwenye nchi mbalimbali za Europe na Amerika ya Kusini.

  Kuwaleta Brazili ilikuwa lazima uwalipe vinginevyo wasingelikuja. Siku hizi michezo ni biashara. Rais wetu si anasema ukitaka kula lazima uliwe kwanza?

  Kwa watu ninaowafahamu mimi, walishangaa kuona Tanzania tuna uwanja mzuri hivyo na pia kushangaa kuona timu ambayo iko kwenye sijui 108 kumbe inaweza kuwa na wachezaji wazuri tu.

  Huwezi kujua matokeo ya hiyo ziara mpaka baada ya muda. Kikubwa ni kwamba huku Ulaya zaidi ya nusu ya watu hawajui Tanzania iko wapi, ingawaje wanajua Kenya iko wapi. Juhudi yeyote ya kuitangaza nchi lazima ipongezwe lakini pia lazima tuangalie je hiyo njia tuliyotumia ndio ilikuwa bora zaidi katika kutumia hizo pesa zote?

  Mleta maada naona kaongeza na chumvi kwenye hilo la bill kwenda Ikulu maana kaangalia pesa za viingilio tu na ku ignore pesa za TV mbalimbali kuonyesha hiyo match pamoja na matangazo kibao.

  Wacha tusubiri Tenga atupatie mahesabu kamili.
   
Loading...