Ilionyeshwa na TV nyingi tu za nje. Kwa UK, walionyesha ESPN ambayo ni TV ya kulipia ya michezo na inaonyesha michezo kwenye nchi mbalimbali za Europe na Amerika ya Kusini.
Kuwaleta Brazili ilikuwa lazima uwalipe vinginevyo wasingelikuja. Siku hizi michezo ni biashara. Rais wetu si anasema ukitaka kula lazima uliwe kwanza?
Kwa watu ninaowafahamu mimi, walishangaa kuona Tanzania tuna uwanja mzuri hivyo na pia kushangaa kuona timu ambayo iko kwenye sijui 108 kumbe inaweza kuwa na wachezaji wazuri tu.
Huwezi kujua matokeo ya hiyo ziara mpaka baada ya muda. Kikubwa ni kwamba huku Ulaya zaidi ya nusu ya watu hawajui Tanzania iko wapi, ingawaje wanajua Kenya iko wapi. Juhudi yeyote ya kuitangaza nchi lazima ipongezwe lakini pia lazima tuangalie je hiyo njia tuliyotumia ndio ilikuwa bora zaidi katika kutumia hizo pesa zote?
Mleta maada naona kaongeza na chumvi kwenye hilo la bill kwenda Ikulu maana kaangalia pesa za viingilio tu na ku ignore pesa za TV mbalimbali kuonyesha hiyo match pamoja na matangazo kibao.
Wacha tusubiri Tenga atupatie mahesabu kamili.