SIRI YAFICHUKA: Deni la 2 billion/- latua Ikulu!

SIRI YAFICHUKA: Deni la 2 billion/- latua Ikulu!

Mgomo wa JF na kiingilio ghali vilisaidia nini? Mana ukiangalia chati ya makadirio+mapato kule michuzi inaonyesha ticket kibao zilidoda!..
Naomba TFF iwaalike Argentina wakimaliza WC!..ha ha ha

hii nchi inatia hasira sana, yaani kila kitu kipo shaghala bhaghalaa...wakimaliza hapo wahamie kwenye wrestling kabisa.
 
hii nchi inatia hasira sana, yaani kila kitu kipo shaghala bhaghalaa...wakimaliza hapo wahamie kwenye wrestling kabisa.

Nilikwambia mapema subiri uone TFF watakavyo tangaza kuwa wamepata hasara.
Wkt hili lilikuwa linajulikana mapema.
 
Tusubiri tuletewe Naomi Cambel kiingilio kitakuwa 300,000/=
atakuja wewe subiri tuu.
alishaongea nae kule kweupe siku ileee anakumbuka mwenyewe.

poleni ndugu zangu...inaitwa serikali ya mwafrika.......and by the way I had profesied! how do you get a loan to pay off pple for their appearance? East african football has gone to the dogs...Harambee stars in kenya is like a political party! nyinyi wamashariki mkiongeza siasa kwa michezo we will never get money from our studiums.
 
Tunaomba TFF watupe taarifa za mapato na matumizi kama ilivyo kawaida yao. Mbona hapa wako kimya?
 
inasemekana Brazil waligaramia wenyewe na wafadhiri wao,ndio maana ata uwanjani matangazo ya wafadhiri wao yalibandikwa....
TFF walitodanganya kuwa wanawalipia brazil,so Far timu ambayo TFF inatakiwa kuilipia 100% ni RealMadrid ambao wanafadhiriwa na Elsalat ambaio ni baba wa Zantel apa Tanzania,ndio maana ata BBC wanatushangaa sisi kuwalipa Brazil.
tenga anajua ukweli
 
Asalaam Aleykum,

Taarifa nilizonazo ni kuwa TFF walienda benki ya NMB kuomba mkopo kwa njia ya overdraft ili waweze kuwalipa Brazil appearance fees za kuja Tanzania. Sina uhakika na exact figure ya mkopo ila taarifa ni kuwa it was $2.5 million (kama shilingi bilioni 3 hivi). NMB wakijua fika kama sponsors wa TFF kuwa shirikisho hilo halina uwezo wa kulipa mkopo huo, walikataa kutoa fedha hizo. Waziri wa Michezo, George Mkuchika, akaiandikia barua NMB kuunga mkono ombi la mkopo huo. Baada ya ku-assess risk za mkopo huo kwa TFF ambao NMB inawajua fika kuwa hawana pesa na kila siku wanatembeza bakuli la kuomba msaada, walimgomea Waziri Mkuchika na kusema hawamtambui. Uongozi wa NMB ukasimama kidete na kusisitiza kuwa kamwe hautatoa mkopo kwa TFF kuwalipa Brazil waje Tanzania mpaka Rais Kikwete au Waziri Mkuu Pinda aandike barua ya serikali kutoa guarantee kwa mkopo huo. Hapo ndipo baada ya kupata baraka zote za Ikulu, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, akaiandikia barua NMB kuwa serikali inaweka commitment ya kubeba deni lote iwapo TFF watashindwa kulipa deni hilo. Baada ya kupata guarantee hiyo kutoka kwa Waziri wa Fedha, NMB wakakubali kutoa overdraft kwa TFF.

Business plan ya TFF ilikuwa kwamba kwa wastani wa bei ya ticket ya 50,000/- x watu 60,000 = shilingi bilioni 3. Matokeo yake ni kuwa tiketi za VIP tu ndiyo zilikuwa sold out huku zile za walala hoi ambao ndiyo walitarajiwa kujaa uwanjani zikabaki wazi. Sijasikia TFF ikitangaza mapato, lakini sidhani kama itafika hata shilingi bilioni 1. Hii ina maana kuwa serikali italazimika kubeba deni la zaidi ya shilingi bilioni 2 kutokana na guarantee iliyoiwekea TFF.

It seemed like a good idea at that time. Ujio wa Brazil unge raise profile ya soka la Tanzania, ungeutangaza Uwanja wa Taifa duniani, ungevutia watalii na wawekezaji Tanzania na ungemjengea sifa JK kwa umma wa Watanzania kama "Mpenzi mahiri wa michezo" kama mabango makubwa yenye picha ya Rais akibusu Kombe la Dunia yalivyopambwa uwanjani siku ya mechi. Ninaambiwa kuwa Rais Kikwete alifurahia sana mpango wa kuileta Brazil nchini na kuamuru serikali itoe kila ushirikiano kwa TFF kufanikisha jambo hili.
Matokeo yake ni kuwa kulikuwa na maelfu ya viti vitupu uwanjani baada ya wananchi kushindwa kulipa kiingilio.

Hii ni ishara tosha ya kuwa serikali hii iliyo ahidi kuleta Maisha Bora kwa kila Mtanzania kumbe wala haijui umasikini halisi wa wananchi wake yenyewe! Hicho kiingilio cha chini cha elfu 30 ni mapato ya mwezi mzima ya Watanzania walio wengi ingawa its just pocket change kwa viongozi wetu.

HII NDIYO NCHI YETU NA HAWA NDIYO VIONGOZI WAKE.

Pamoja na shutuma nyingi zinazotolewa na wale wasioitakia mema nchi yetu, Tanzania haiwezi kuishi kama Kisiwa na ikaendelea kupoteza umaarufu wake kwa sababu ya kuogopa gharama mbalimbali ikiwa ni pamoja na za kifedha. Dakika tisini zilizotumika kuitangaza Tanzania kupitia televisheni zaidi ya sitini duniani zina thamani kubwa kuliko Bilioni 1 ambazo WanaJF wanaziona nyingi mno kulipwa na Tanzania.

Nchi za Rwanda, Uganda na Burundi zinatumia pesa nyingi kutangaza taarifa za sokwe mtu wanaoishi kwenye misitu ya Virunga ili kuvutia Watalii lakini sina uhakika kama mapato yao ya muda mfupi yanalingana na gharama wanazotumia. Tanzania haijafanya kosa kuitangaza Tanzania kupitia timu ya Brazil. Kocha wa Timu ya Brazili alifurahia mchezo wa Taifa Stars. Timu nyingine kubwa duniani zitapenda zije zione hiyo timu iliyofanikiwa kumfunga mlinda mlango wa Brazil, Julius Ceaser goli. Mlinda mlango huyo anapewa nafasi ya kwanza kwa ubora duniani, lakini kafungwa na Taifa Stars. Wenye roho za kimaskini wanaona Tanzania imepoteza fedha nyingi kwa mpira tu, lakini lazima tuipongeze Serikali na TFF kuliko kuilamu. Hata kama ni deni kubwa kiasi gani, lazima tukubali kwamba madeni hayaui. Deni hilo linaweza kulipwa na watu kama akina MENGI, DEWJI, MANJI au hata MADEGA, cha msingi ni kwamba wageni wameondoka wakiwa wameridhika na wataendelea kuimwagia sifa Tanzania. WanaJF wenyewe wanasema mkono mfupi haulambwi. Mlitegemea nini kwa kujiwa na timu kubwa kama Brazil.

Nina uhakika kwamba nchi jirani za Rwanda, Burundi, Uganda au Kenya, zingeona fahari kubwa kucheza na Brazil kwa gharama yoyote. Zilisema kwa nini Tanzania. Ilikuwa bahati ya mtende. Nina uhakika pia kwamba nchi hizo pasi na kusema wazi zingetaka bahati hiyo ya kucheza na Brazil iwaangukie. Bahati kama hiyo haiji mara mbili, na miaka mingi itapita bila timu ya Brazil kuja tena Afrika.

Pamoja na umaskini na hali mbaya ya uchumi ya Zimbabwe walikubali Brazil ije. Labda tujiulize, hivi Tanzania ingekataa ‘offer’ ya Brazil, ingeelewekaje?

Ingawa sisi wachangiaji wengi wa safu hii hatuna mazoea ya kuisifia serikali mimi nafikiri kwa hili tumpongeze Rais KIKWETE kwa kutuletea timu ya Brazil. Tumewaona wachezaji ambao tumezoea kuwaona kwenye picha za Luninga. Ahsante sana Rais KIKWETE. Kwa wachangiaji wa safu hii tuanze kukosoa na kusifia kila inapostahili na tusiione serikali kwamba kila siku inafanya madudu.
 
Dakika tisini zilizotumika kuitangaza Tanzania kupitia televisheni zaidi ya sitini duniani zina thamani kubwa kuliko Bilioni 1 ambazo WanaJF wanaziona nyingi mno kulipwa na Tanzania.

hypothetically - very sad

Nchi za Rwanda, Uganda na Burundi zinatumia pesa nyingi kutangaza taarifa za sokwe mtu wanaoishi kwenye misitu ya Virunga ili kuvutia. Watalii lakini sina uhakika kama mapato yao ya muda mfupi yanalingana na gharama wanazotumia

Kama huna uhakika kwanini unafanya "comparison" - very sad indeed

Timu nyingine kubwa duniani zitapenda zije zione hiyo timu iliyofanikiwa kumfunga mlinda mlango wa Brazil, Julius Ceaser goli. Mlinda mlango huyo anapewa nafasi ya kwanza kwa ubora duniani, lakini kafungwa na Taifa Stars.

Kama kumfuga kipa wa Brazil ni "DEAL" nadhani "Korea DPR - North Korea" itapata watalii wengine sana baada ya Kombe la Dunia Mwaka huu - very sad indeed

Pamoja na umaskini na hali mbaya ya uchumi ya Zimbabwe walikubali Brazil ije. Labda tujiulize, hivi Tanzania ingekataa ‘offer' ya Brazil, ingeelewekaje?

Kuelewekaje na nani? Alitoa "OFA" ni Brazil au ni Tanzania (Serikali via TFF via Kamati ya Rais ya Kombe la Dunia) - very sad indeed

Tumewaona wachezaji ambao tumezoea kuwaona kwenye picha za Luninga.

Nilifikiri suala la msingi lilikuwa ni "kutangaza" nchi? Kumbe ni kuwaona akina "Maicon and Co"? - very sad indeed
 
Walitegemea faida wakati viti kibao vilikuwa tupu.Hawakutunia akili kabisa ni bora wangeweka kiingilio cha kawaida watu wengejaa na wengeweza kupata zaidi ya hizo.
Hakuna cha ajabu bili hiyo kutuwa ikulu kwani ni jambo la kawaida ukimdhamini mtu, hata mahakamani, atakapotakiwa aonekane na asionekane, polisi watatua mlangoni kwako.
Kosa la TFF ni kusikiliza kelele za Watanzania bila kuangalia ukweli purchasing power yetu wengi ni ndogo ( Wamuulize Mrema 1995 ALISHAPATA URAIS KWA KUVUTA WATU KWENYE KAMPENI!!). Lilikuwa kosa la kibiashara kutofanya uchaambuzi yakinifu objectively without passion. Labda linear programming ingewasaidia kutafuta scenario ambayo ingewapa watu wengi kiingilio nafuu na vuvuzela nyingi kuliko hicho walichopanga kwa walala hoi. Bila shaka TFF wamejifunza kuwa kiingilio cha milangoni hakiendeshi biashara ya mpira bali matangazo ya TV, radio na biashara. Kwa hiyo hesabu ya kiingilio ya shs. 1.6 bilioni si mbaya, sasa wajumuishe na mapato toka TBC na TV zilizoonyesha mchezo huo, upungufu hautafika bilioni mbili. Tenga na wenzake waonyeshe ujasiri kueleza mapato ya mechi kutoka kwenye vyanzo vyote na si viingilio tu!!!
 
Uionee uchungu yako?!hiyo pesa kama isingewaleta brazili, basi ingetumika kuwarejesha madarakai wateule!! Mkuluuuuuuuuuuuuuu, tuletee na ile real madrid ambayo ulituahidi!!!! Au ilikuwa ni staili ya nitoke vipi mheshimiwa?! Huu ni ufisadi, lakini ni ufisadi mzuri kwavile angalau nami nimefaidika kuliko ule wa richmond na epa!!!!
 
Bado wanajumlisha mapato maana mpaka leo kimya.
 
Back
Top Bottom