Mtu wa Kwao
JF-Expert Member
- Jan 15, 2008
- 258
- 21
Walitegemea faida wakati viti kibao vilikuwa tupu.Hawakutunia akili kabisa ni bora wangeweka kiingilio cha kawaida watu wengejaa na wengeweza kupata zaidi ya hizo.
umeipenda??what do u mean??
I mean nimeipenda taarifa ya kuhus TFF kupata hasara................Wamejitakia........again,nimeipenda sana hii
Nadhani hii blog ya Michuzi siyo ya kutegemewa sana bora tusubiri source ya maana!Guys nimesoma kwa Mr Michuzi kuwa tff wamekula hasara kwenye mechi kati ya TZ na Brazil.
Tff wamepata tsh 1.6bn wakati walitegemea kupata tsh4bn,katibu mkuu wa tff ndg Mwakalebela kasema haya hivi punde tu.
nadhani hii blog ya michuzi siyo ya kutegemewa sana bora tusubiri source ya maana!
Hukupenda Brazil walivyo kuja Tanzania....vichwa vyote vilivyotoa hiyo idea.
Katibu Mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela kasema sasa hivi jijini Dar kwamba Shirikisho hilo linajiandaa na mikakati ya kufunika hasara hiyo pamoja na kuweka mambo sawa.
Hakutaka kwenda kwa undani ni shilingi ngapi walikopa na toka wapi lakini kasema Brazil walilipwa pesa yao kwa muda uafaka na kwamba watoa huduma wote walishalipwa na hakuna mwenye kuidai TFF.
Kasema, hata hivyo, mechi hiyo na Brazil ilikuwa na faida kubwa ya muda mrefu, ikiwa ni pamoja ya wachezaji takriban 6 kufuatwa na mawakala wa timu za ulaya kuwataka. Pia amesema utalii utakuwa sana kwani wengi wanaulizia Tanzania.
sawasawa mkuu....naamini kabisa unajua nani mzigo huu unamwangukia....
Kweli ni mzigo wetu, lakini hii itawafundisha kitu TFF. Mpira haupandi kwa kucheza mechi moja na brazil bana, halafu hiyo hasara ya Tshs 1.3bil kama wangewekeza katika timu si ingekuwa bora zaidi?
Asalaam Aleykum,
It seemed like a good idea at that time. Ujio wa Brazil unge raise profile ya soka la Tanzania, ungeutangaza Uwanja wa Taifa duniani, ungevutia watalii na wawekezaji Tanzania na ungemjengea sifa JK kwa umma wa Watanzania kama "Mpenzi mahiri wa michezo" kama mabango makubwa yenye picha ya Rais akibusu Kombe la Dunia yalivyopambwa uwanjani siku ya mechi. Ninaambiwa kuwa Rais Kikwete alifurahia sana mpango wa kuileta Brazil nchini na kuamuru serikali itoe kila ushirikiano kwa TFF kufanikisha jambo hili.
Matokeo yake ni kuwa kulikuwa na maelfu ya viti vitupu uwanjani baada ya wananchi kushindwa kulipa kiingilio.
Hii ni ishara tosha ya kuwa serikali hii iliyo ahidi kuleta Maisha Bora kwa kila Mtanzania kumbe wala haijui umasikini halisi wa wananchi wake yenyewe! Hicho kiingilio cha chini cha elfu 30 ni mapato ya mwezi mzima ya Watanzania walio wengi ingawa its just pocket change kwa viongozi wetu.
HII NDIYO NCHI YETU NA HAWA NDIYO VIONGOZI WAKE.