ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 24,944
- 61,076
Hili kwangu sio suala la mashaka tena. Nimejaribu mwenyewe na kuthibitisha kwamba AI inaweza kutengeneza picha ya mkeka ambao haujawahi kuwepo, lakini ukaonekana kama mkeka halisi.
Nimeipa AI maelekezo, ikanitengezea betting slip yenye namba ya mkeka, tarehe, timu, odds, stake, potential winnings na status ya WIN/PAID OUT.
Hapo ndipo nilipogundua udhaifu mkubwa wa hizi screenshot za mikeka tunazoonyeshwa Instagram. Leo mtu hahitaji kushinda milioni 5 ili awe na screenshot inayoonyesha ameshinda milioni 5. AI inaweza kuitengeneza.
Kwa hiyo screenshot ya mkeka yenye “WIN” au “PAID OUT” sio ushahidi wa kutosha tena kwamba fedha hizo zilishindwa kweli.
Nitaweka hapa chini mfano nilioutengeneza kwa AI. Mkeka huu haukuchezwa kabisa AI ndiyo imeutengeneza.kwa hiyo hawa wakamaria waendelee kuwala Wajinga waendelee kupata commision zao kwenye makampuni