Introduction to Facebook and Instagram Ads (Matangazo ya sponsored) 2020

Introduction to Facebook and Instagram Ads (Matangazo ya sponsored) 2020

Max Marketer

Member
Joined
Oct 13, 2020
Posts
46
Reaction score
50
Salute once again guys, hope kila mtu yuko vizuri

Well, leo nimekuja kuanza kuelezea mada hii nilosema nitaileta hapa, sababu naamini kuna fursa kubwa sana kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kufahamu vizuri MATANGAZO YA FACEBOOK/INSTAGRAM

Ukiangalia kwa biashara na kampuni za wenzetu huko, wanatumia haya matangazo na kupata ROI (return on investment) kubwa sana, wanapata wateja wengi zaidi,mauzo zaidi na kukuza Brand.

Hata hapa kwetu naamini wapo, japokuwa ni wachache, huku wengi naskia wanasema "Tunaishia kupata likes tu, na sio wateja"

Hii inaweza kuchangiwa na vtu vingi, mojawapo ni ufahamu wa jinsi matangazo haya yanavofanya kazi, na ni kwa namna gani uyatumie kutimiza lengo lako (kibiashara, personal etc)

Kama kweli unataka kufanikiwa ktk biashara yako kwa kutumia ads, Lazima ufahamu vitu kama

=> CREATIVE (picha /videos/Graphics) zipi utumie ili kuvutia watu wengi zaidi,

=> AD COPY( maelezo sasa yenye ushawishi baada ya mtu kuona picha/video),

=> HEADLINES zipi utumie kucatch attention

=> PLACEMENTS ZA TANGAZO (wapi tangazo lako uweke mfano newsfeed, stories, messenger etc)..

=> AUDIENCES & TARGETING (watu gani unalenga waone tangazo lako, wapi wasilione,..)

=> CALL TO ACTION (yani mtu akishaona tangazo afanye nini: akupigie, akutumie message whatsapp, ajoin group lako la whatsapp,atembelee website yako/IG,akutumie DM,Apakue app yako nk)

=> BUDGET (uweke bajeti gani ktk tangazo ili kupata results unazotaka, mfano mm tangazo moja tu la dola 5 lilileta mteja wa 60k,..that's 12x return),

Sasa jiulize biashara yako inaweza kufaidika vp kama utaweza kuzingatia vitu vyote hivi

Unaambiwa TEST,DON'T GUESS, ukitaka kupata mafanikio na paid ads

Lakini utatesti vp kama hufahamu hata kidogo?.. Kila sku ww ads zako unafanyia kupitia Instagram kule kule kwenye PROMOTE button

Nmeanzisha series hii, nitakuja kushea hapa all the tips, how to's, na vtu nnavofahamu ktk ulimwengu huu wa social media marketing and paid ads ..VTU AMBAVYO UKIZINGATIA utafanikiwa ktk sponsored ads

STAY TUNED

Naamin wapo wataalam wengine pia watachangia hapa, uzoefu wao na kwa pamoja tutasaidia watu kufahamu na kutumia fursa hii kukuza biashara zao

Aya tuchangamshe mada zaidi

Comment apo chini

-Ungependa kufahamu nini ktk ads?
-Umekutana na changamoto zipi?
- Experience yako ulivopata wateja zaidi kupitia ads

_________________________________

By: Max Marketer TZ
- I BELIEVE IDEAS THAT SPREAD WIN,

- I HELP Businesses WIN by spreading their ideas through - Social media marketing | Content creation (photo & videos) | Graphics

- 0752226475 , ask me anything about marketing your business
Screen-Shot-2019-11-15-at-2.51.03-PM-696x417.jpg
 
Mimi naomba kujua jinsi ya kujitangaza kwa kupitia hayo matangazo.
Karibu sana mkuu, ungependa kufaham nn exactly?.. Au kuanzia mwanzo kbs mpaka kuweza kufanya matangazo?

Hatua ya kwanza kabisa ni kuwa na Instagram business account

Kisha utaiconnect account yako na facebook, kupitia facebook page

Then utaweka njia ya malipo (credit card au PayPal)

Kisha utaweza kuanza promotion, hapa ss inategemea lengo lako ni nini haswa

Nimetoa intro kdg mkuu, kama una swali au ungependa kufaham zaidi,.. KARIBU
 
Kaka naomba maelezo kdg,namna gani naweza kutengeneza android app na nikatumia Facebook adds kupata pesa.
Boss kutengeneza App hapo lazima utafute mtaalam wa app /developer anaweza kukusaidia...

Kuhusu facebook ads, ni kwamba unatumia ads kuwafahamisha watu kuhusu app yako na kuwashawishi waidownload... So unapata installs zaidi kulingana na bajeti na pia tangazo likoje

Then utaweza kuingiza hela ktk app yako kama iko monetized.. Kama kuna ads, au services za kulipia

Apo ndipo utaweza kuingiza hela
 
which means kama unaifaham biashara yako vizuri ,..yani vitu kama CUSTOMER ACQUISITION COST na CUSTOMER LIFETIME VALUE

una uwezo wa kugenerate sales maradufu, mfano kama bajet ya dola 5 inakupa mteja mmoja wa 60k

Ukiweka dola 50 unaweza kufikisha wateja wenye kubuy total 600k*

*All terms and conditions applicable
 
Ningependa kufahamu kuhusu Search engine marketing.
 
Shukran mkuu.

Kuna utofauti gani kati ya boost na promote ads
Boost inapatikana facebook page and promote button inapatikana instagram account

Boost lengo lake ni kuamplify Post yako au kuiboost ionekane zaidi na kupata engagement kama likes, comments and shares

Promote inakupa options ya kugenerate traffic like watu waende ktk insta page yako, ktk website yako, YouTube... AU wakutumie DM.

Lakini hizi zote ziko limited, if you want to explore the full potential of facebook ads, inabidi utumie Facebook ads manager, huku ndo madini yote yalipo
 
Nilitumia inst kuweka matangazo nilikuwa nalipia 5 usd per day na nilitumia kama miezi miwili lakin outcome haikuwa nzur, nafikir kuna mambo hayakuwa sawa, nahitaji kupata elimu zaidi namna ya ku catch up wateja.
 
Ningependa kufahamu kuhusu Search engine marketing.
Search engine marketing is an act of promoting your business websites and increase the traffic through paid ads

Hapa unalipia zile PPC (pay per click) ads za Google kwa certain keywords watu wanazosearch

Mtu akisearch keyword flan, website yako inatokea ktk top results.. Which means mtu ana chance kubwa ya kuvisit

Na atakapoclick ndipo unakatwa hela hence "pay per click "

Lazima ufahamu vizuri potential clients wako, mfano keywords wanazotumia ktk search engines... Ili uweze kubid vizuri

Mwisho site yako inabd iwe inazingatia SEO practices pia
 
Nilitumia inst kuweka matangazo nilikuwa nalipia 5 usd per day na nilitumia kama miezi miwili lakin outcome haikuwa nzur, nafikir kuna mambo hayakuwa sawa, nahitaji kupata elimu zaidi namna ya ku catch up wateja.
Of course hapo lazima kulikua na ishu, kuna principles 2 nazitumia ktk situation kama hii

1. WHAT'S YOUR PURPOSE /INTENT/GOAL

Kabla ya kusponsor any post, lazima uwe na idea kichwani unalenga ktu gani

Awareness, engagement, traffic,leads OR sales ambayo kila mtu anataka

2. CREATIVE, COPY, OFFER

Umetumia nini ktk tangazo as a creative (yani picha au video au graphics)?

Ad copy... Yani tangazo lako maelezo yamekaaje, yana ushawishi?.. Au unaweza boresha zaidi

OFFER.. Mwisho wa sku je unawapa watu OFA gani itakayofanya wakutafute?..au you're Just plain selling in a boring way kama ambavo kila mtu anafanya?

Nadhan umepata insights kidogo boss,kama una swali or anything to share you can add here

More lessons coming
 
Salute wakuu, naiman kila mtu yuko vizuri na harakati zinaendelea ktk biashara na ujasiriamali.

Leo tunaendelea na mada nliyohaidi kuleta humu kuhusu " KUFAHAMU VIZURI MATANGAZO YA FACEBOOK & INSTAGRAM, NA NAMNA UNAVYOWEZA KUYATUMIA KUPATA WATEJA ZAIDI & KUKUZA BIASHARA YAKO"

Baada ya kutoa Intro ktk uzi uliopita, Leo nitaendelea kwa kushea nawewe vitu 3 muhimu zaidi kuvifahamu na kuvizingatia unapotaka kuanza matangazo..

Au umekua ukifanya mara kwa mara, sasa unataka KUONGEZA IMPACT ya matangazo yako, sio kutoa hela na kuishia kupata likes tu na sio wateja

Mimi naamini ktk knowledge, yani mtu akiwa na ufahamu mzuri ktk kitu flan, basi anaweza kukifanya kwa ufanisi na kupata mafanikio makubwa.. Kuliko mtu anayekosa knowledge,

Ndio maana naleta post hizi hapa, ili wafanyabiashara & wajasiriamali waweze kufahamu, na kuweza kutumia fursa hii ya matangazo ya kulipia kukuza biashara zao,

Just imagine una uwezo wa kuonyesha biashara yako kwa watu elfu 10 na zaidi, Tanzania nzima.. Kwanini ukose wateja?.. Kwanini biashara yako isikue?..

Well, kama hufahamu nini ufanye, unaweza kuonesha watu na bado wasinunue,

That's why ni muhimu kufahamu strategies za kutumia unapofanya ads, usiende kichwa kichwa,..

Hapo unakuwa umejiweka ktk hali ya kupata mafanikio kupitia ads, na unaweza kukuza biashara yako kuliko competitors wako.

Twende ktk mada ya Leo, KABLA HUJAANZA KUTENGENEZA TANGAZO LOLOTE LILE,.. Nakushauri uzingatie vitu hivi 3.

1.AD OBJECTIVE
- Hapa naamini eventually kila mtu anataka kuuza bidhaa/huduma yake na kupata wateja wengi zaidi

- Lakini kulingana na aina ya biashara unayofanya (bidhaa/huduma), lazima ukubali ukweli kwamba sio kila mtu anayeona tangazo lako atashawishika kununua hapo hapo.

-Kuna baadhi ya bidhaa mtu anaweza ona na kununua hapo hapo, especially bei ikiwa rahisi na risk ikiwa ndogo, but ikiwa unauza au kutoa huduma yenye gharama au risk kubwa au mteja inabidi apate ufahamu zaidi Kwanza., lazima uende kwa steps (sales funnel, multiple ads for different folks)
.
- Na hapa ndipo concept ya AD OBJECTIVE inapokuja,.. Facebook wanakupa objectives mbali mbali ambazo unaweza kuzitumia ktk stages mbali mbali za mauzo yako ili uweze kufanikisha lengo lako

- Objectives zipo mbali mbali kama Reach & Brand awareness, Traffic to your website /instagram page, Video views, Lead generation, conversion etc

-Tutaingia ndani hapa tuzichambue hizi objectives vizuri, na namna unavoweza kuzitumia ktk Kuitangaza biashara yako


2.AUDIENCES

- Ili ufanye tangazo, lazima liwe na audience AKA watu unaowalenga waone tangazo lako, kwa lugha rahisi hawa ndio TARGET MARKET yako, na humu ndio unategemea kupata wateja

- Facebook wana option ya audiences 3, ingawa wengi wetu wanatumia aina moja ya audience inayoitwa CORE AUDIENCE

- CORE AUDIENCE ndo ile unatengeneza kwa demographics data kama vile umri wa watu, jinsia, location walipo na interests zao ...unaweka data na facebook inakupa idadi yao maybe Laki 4,5,milion 1,2 nk

- Sana Sana kwenye Instagram kule, kama ushapromote post kupitia IG, utakua unafahamu hapa namaanisha nini.

- Ni audience nzuri na inaweza kukuletea matokeo mazuri tu,LAKINI kama core audience itakuletea matokeo mazuri.. Basi Hizi aina 2 zingine zitakuletea MATOKEO MAZURI ZAIDI.

-Aina hizi ni CUSTOM AUDIENCE na LOOKALIKE AUDIENCES

- Tutazichambua kwa kina, ila nikuulize utajiskiaje pale unapoweza kuweka tangazo lionekane na wale waliovisit profile yako ya insta tu au wale walioangalia video yako mpaka mwisho tu?.. Au wale waliotembelea website yako tu?

- Kiuhalisia hao ndio wanakuwa watu wenye interest na biashara yako.. Na ukiweza kuwachambua hao tu na kuwaonesha matangazo yako.. UNA CHANCE KUBWA ya kuuza zaidi kuliko kuonesha matangazo kwa watu wote hata wale wasiokua interested.

- Take note hapa, tutaendelea kuzichambua vizuri

3. AD/TANGAZO LENYEWE

- Hapa nazungumzia sasa tangazo lenyewe utakalolitumia kwa maana Ya CREATIVE and COPY

- AD CREATIVE ni picha, video au graphics utakayoitumia ktk tangazo lako. Lengo kubwa ni kucatch attention ya mtu anayescroll Insta/FB aache na aangalie sasa tangazo lako

- Usitumie picha/video ilimradi tu, kama kweli unataka kufanikiwa lazima ujitofautishe na wenzio

- AD COPY ni maelezo sasa ya Tangazo lako. Tambua mwisho wa siku maneno yana nguvu zaidi ktk kumfanya mtu anunue au asinunue baada ya kuona Tangazo lako.

- Hapa kwny Ad copy kuna mengi ya kuongelea, tutajifunza zaidi ktk post zangu zinazokuja

Naomba tuishie hapa kwa Leo, kama una swali lolote lile kuhusu mada, karibu

Hujaelewa sehemu unahitaji ufafanuzi, karibu

Au umeshafanya ads na unahitaji ushauri uboreshe wapi, karibu pia

---------------------------------------------------------------
By :- Max Marketer Tz

=> "I believe ideas that spread WIN "

=> Social media marketing | Content creation for Brands | Graphics | Simple website design

=> PM me or Text/Call/Whatsapp. 0752226475
IMG_20201029_111847.jpg
IMG_20201029_111925.jpg
IMG_20201029_112003.jpg
IMG_20201029_112035.jpg
IMG_20201029_112131.jpg
IMG_20201029_112238.jpg
 
Unatoa hii huduma ya kuwekea watu matangazo kwa usahihi?
Yes... Consultation ni FREE, nitakupa maelekezo na nini cha kufanya, ni PM au text whatsapp 0752226475, biashara yako na username ya Instagram..tunaweza anzia hapo
 
Back
Top Bottom