Mukubwa sitetei, lakini nimeambiwa wafanyakazi wengi wa BOT wamekuwa seconded sehemu mbalimbali wakiretain uajiri wao endapo watarudi baada ya kutumikia hizo sehemu nyingine. Ni utaratibu wa Central banks specificaly kama ilivyo "sabbatical leave" kwa vyuo vikuu.
Mfanyakazi huyo anaweza kuondolewa jina lake endapo ataamua yeye kuopt kuhamia moja kwa moja kwenye hiyo institution nyingine.
Utaratibu huu ni tofauti na taratibu za Utumishi wa Umma tunazozifahamu na mishahara yao inabaki kama ilivyo kwa ajili ya mafao ya kustaafu na siyo kwamba wanapewa hiyo mishahara kila mwezi ilhali huko walipo nako wanalipwa, au kuna wafanyakazi hewa kama inavotafsiriwa sasa mitaani. Ingekuwa hivyo ni kesi ya jinai na Rais asingesita kutumbua jipu.
Kwa kuzingatia hayo, ninachoona ni kwamba mkuu anataka utaratibu huo ubadilike kwani Benki Kuu yetu siyo "closed shop" au too special kuwa na taratibu tofauti kabisa na utumishi wa umma.